Ongezeko La Mtindo Wa Kucheza Karata Nchini Kenya

Ongezeko La Mtindo Wa Kucheza Karata Nchini Kenya

Kuna aina nyingi za betting nchini Kenya na kampuni zinazo toa huduma hizi zimeongezeka na kuzidi kuongezeka kadri siku zinavyo zidi kupita. Uraibu huu uko kwa ongezeko kuu nchini na idadi ya watu wanao hijusisha kuzidi kuongezeka. Watu wa umri wote wana cheza betting, kutoka kwa watu wazima hadi kwa watoto wa shule za msingi ambalo lina hatarisha maisha yao ya usoni. Mtindo huu unahusikana vipi na ulezi? Wazazi wanahusika kivipi na tabia na maisha ambayo watoto wao wana amua kuishi? Tuna angazia betting and parenting in Kenya.

Sababu Zinazo Sababisha Ongezeko la Uraibu Huu: Betting and Parenting in Kenya

betting in kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Ulevi Ulio Legemea

Wazazi wengi nchini Kenya wana jihusisha katika uraibu huu. Ni vigumu kuwashauri wanao kuto jingiza kwenye vitendo ambavyo hauoni ubaya wake. Kwa mara nyingi, wazazi hawa hawana wakati wa kutosha na watoto wao. Kwani mara nyingi utawapata wakifanya shughuli hizi za kubet ama kucheza karata. Jambo ambalo linafanya ulezi kupoteza msingi wake, pia watoto wanakosa watu wa kuwashauri kuhusu athari hasi za matendo haya.

Mtindo Ibuka

Betting ni jambo ambalo limekuwa likifanywa kwa miaka mingi, ila, kwa miaka michache iliyo pita, jambo hili limekuwa kwa ongezeko kuu na watu wengi wakilianza ili waweze kupata pesa za kirahisi. Pia watu wengine wanaanza mtindo huu kufuatia shinikizo la rika. Ukiwa kwa kundi la watu ambao wanashiriki uraibu huu, unajipata umeanza pia.

Ongezeko La Mtindo Wa Kucheza Karata Nchini Kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Kukosa Ushauri

Wanao shiriki tendo hili sana ni vijana wa umri wa makamo hasa walio maliza kidato cha nne na walio katika vyuo vikuu nchini. Wana fanya hivi kwani wanakosa ushauri kutoka kwa wakuu wao. Kwa hivyo wanajipata wakifanya uamuzi mbaya. Pia wazazi wao hawakai chini nao na kuwaeleza kinaga ubaga adhari hasi za uraibu huu. Kuna mwanya kwenye ulezi ama betting and parenting in Kenya.

Ongezeko la Kampuni za Kucheza Karata

Kampuni zinazo toa huduma hizi nchini zimeongezeka sana. Na serikali haina kanuni dhabiti za kuhakikisha kuwa kampuni za huduma hizi zinafuata kanuni zinazo hitajika. Pia, kuhakikisha kuwa watoto wanao jihusisha na uraibu huu wamefikisha umri wa miaka 18. Nchi ya Kenya ina aina zote za betting kwa mfano, sportpesa log in,  betting, lotto.

Njia za Kupunguza Uraibu Huu

Ni muhimu kwa wazazi kutahadhari na mambo ambayo watoto wao wanafanya katika wakati wao wa ziada. Huenda wanapo pata wakati wa ziada wanaenda kujishiriki katika mtindo huu wa kucheza karata. Washauri kuhusu adhari hasi za mtindo huu na uwahimize kuyapa masomo yao kipao mbele. Wazazi wanapaswa kuwa na wakati wa kupiga ngumzo na watoto wao ili wahisi wako huru kuongea na wazazi wao kuhusu jambo lolote.

Ongezeko La Mtindo Wa Kucheza Karata Nchini Kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Ni muhimu kwa serikali pia kudhibiti kampuni za huduma hizi, na kuhakikisha kuwa wanao toa huduma hizi wana afikiana na kanuni zilizowekwa. Ili kudhibiti umri wa watoto wanaoshiriki katika betting na kuruhusu walio fikisha umri wa miaka 18. Kwani katika umri huu, mtu ni mzima na ana uwezo wa kufanya uamuzi ulio afikiana.

Uraibu huu, umepelekea katika matokeo duni ya masomo ya wanafunzi hawa. Jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa kina kwani masomo yanapaswa kupewa kipau mbele katika maisha ya watoto. Na masomo duni, maisha yao ya usoni hayatakuwa na mafanikio kwani masomo ndio chanzo cha maisha mema.

Vyanzo: Standard media, webmd

Pia Soma: Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

Written by

Risper Nyakio