Wanaume wengi hushangaa kinachoendelea na wake zao baada ya kufunga pingu za maisha. Kabla ya kuikingia katika ndoa, walikuwa wanandoa bora na wenye furaha wakati wote. Bibi alifurahia vitu vidogo ambavyo mwenzi wake alimfanyia wakati huo. Ila punde tu baada ya kuingia katika ndoa, na hasa baada ya kupata watoto, mambo huchukua mkondo tofauti. Bibi kukasirishwa na kila kitu. Hata anaponunuliwa zawadi, hatosheleki na hadhihirishi furaha kama hapo awali.
Je, kipi kinachomfanya bibi kukasirishwa na kila kitu?

Wanawake na wanaume ni tofauti na pia jinsi wanavyo onyesha hasira zao ni tofauti. Mara nyingi wanaume wanapokasirishwa hueleza na kisha kurejelea maisha yao, tofauti na wanawake wanaonyamazia kinachowasumbua. Sote tunafahamu usemi maarufu ambao wanawake wanapenda kutumia, "niko sawa". Ilhali hawako sawa, wakati huo, wanahasira za mkizi.
Mara nyingi unapomkasirisha mwanamke, atakunyamazia na kujitenga na mazungumzo ya aina yoyote kuhusu kilichowakasirisha.
Sababu kwa nini bibi amekasirika wakati wote
Jambo la kwanza kung'amua ni kuwa, ikiwa bibi yako alikuwa mtu mcheshi na aliyependa kutabasamu sana hapo awali na uhusiano wenu ulikuwa na furaha. Kisha akabadilika na kuwa mtu anayekasirishwa na kila kitu, sio maana kuwa alikuwa ameficha utu wake halisi hapo awali. Ng'amua kuwa kuna shinikizo nyingi tofauti maishani zinazo mliwaza mwanamke. Kama vile:
- Kujaribu kufanya kila kitu bila usaidizi
Tofauti na siku za hapo awali ambapo kazi kati ya jinsia ilidhihirika kwa uwazi, mambo ni tofauti. Hapo awali, jukumu la mwanamke lilikuwa kutunza familia na kuhakikisha kuwa watoto wanachungwa. Jukumu la mwanamme lilikuwa kukidhi mahitaji ya familia. Hivi sasa, majukumu yamebadilika, mwanamke anafanya kazi kusaidia kukimu mahitaji ya nyumbani na angali anatarajiwa kuwatunza watoto na kufanya kazi zote za kinyumbani.
Usaidizi wa mwanamme:
- Mkumbushe kuwa sio lazima afanye yote kwa pamoja
- Msaidie kufanya kazi za kinyumbani
- Mpe muda aende likizo
- Tafuta mfanyakazi atakayesaidia na kazi za kinyumbani
2. Kujaribu kuwa mfano wa kuigwa
Kuna shinikizo la kijamii kuwa mwanamke anastahili kuishi kwa njia fulani, kufanya mambo fulani na kujitenga na kufanya ama hata kufikiria kufanya mambo mengine. Hasa anapoingia katika ndoa. Huku maisha ya mwanamme yakiendelea kama hapo awali, mwanamke ana jipata maisha yake yamebadilika kwa kasi. Hana wakati wa kupatana na marafiki zake ama kujumuika na sherehe. Hapati wakati tosha wa kupumzisha akili kwa kubadili mazingira yake.
Usaidizi wa mwanamme:
- Sahau masharti yaliyowekwa na jamii kuhusu wanawake. Mpe muda aende ajumuika na marafiki zake
- Ni sawa kwake kuchukua muda na kufanya mambo yaliyompendeza hapo awali, kwa mfano, kwenda kufanya ununuzi wa manguo
- Mpeleke date mara moja kwa wiki ama mara tatu kwa mwezi

3. Mabadiliko ya homoni mwilini
Homoni huchangia pakubwa katika hisia za mwanamke. Kubadilika kwa viwango vya homoni mwilini mwa mwanamke husababishwa na mambo kama, kutumia njia za uzazi wa mpango kama tembe, kuwa na hedhi ama anapokuwa na mimba. Kwa hivyo unapoona mke wako amekasirika, baadhi ya wakati, huenda ikawa ni kufuatia viwango vya homoni kubadilika mwilini.
Usaidizi wa mwanamme:
- Hutatambu wakati wote chanzo cha mhemko wake wa hisia, kwa hivyo, ni vyema kumwuliza
- Ikiwa angependa kupatiwa muda kuwa peke yake, mpe nafasi
- Mwonyeshe kuwa unamdhamini, mnunulie zawadi ikiwa hiyo ndiyo lugha yake ya mapenzi
Kumbuka kuwa ndoa sio jela, inapaswa kuwa kikao cha mapenzi na furaha. Na uungano huu hauwezi kuwa na furaha ikiwa moja kati yenu hana furaha.
Soma Pia: Fedha Za Kifamilia: Jinsi Ya Kuhifadhi Pesa Za Maisha Ya Usoni Ya Wanao