Katika mkondo wa ndoa, sio jambo geni kupata mwanamme akijiuliza kinachomfanya bibi kukosa hamu ya ngono. Wanawake wana nyuso tofauti, kwa hivyo jibu la swali hili sio rahisi. Tuna angazia mambo kati ndoa ambayo huenda yanamfanya mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi na bwanaye.
Sababu za bibi kukosa hamu ya ngono

Kadri wanandoa wanavyozidi kuwa pamoja, ndivyo ambavyo baadhi yao hushuhudia punguko katika mara wanazo fanya mapenzi. Maumbile ya wanawake na wanaume ni tofauti. Kwa wanawake, mapenzi sio kitendo cha ngono tu, ni vitendo viinavyo dhihirisha kuwa anapendwa, pamoja na maneno ya kumdhamini.
Kuna baadhi ya wanawake wanao amini kuwa hamu yao ya kufanya mapenzi iliisha walipojifungua. Kuna uwezekano kuwa huenda hamu yako ya ngono imepunguka kwani una aina ya chuki kwa mchumba wako. Unahisi kana kwamba hawajali kuhusu hisia zako baada ya kujifungua, hata unapomweleza kinacho kukumba. Ama kukuwachia majukumu yote ya nyumbani. Hisia hizi huenda zikamfanya mwanamke kukosa hamu ya kimapenzi kwa bwanake.
Jaribu kufahamu mahitaji ya mkeo na kuyatosheleza, hata kama sio yote, asilimia kubwa. Kufanya hizi kutamwashiria kuwa unampenda na nyote mtakuwa na furaha. Wanandoa walio na furaha kwa kiasili hupenda kufanya mapenzi zaidi. Kwa hivyo, mbona bibi yangu hana hamu ya kimapenzi nami? Angekuwa na hamu zaidi ukichukua usukani katika kuhakikisha mahitaji yake yana toshelezwa. Unaweza pia kumsaidia na majukumu ya kinyumbani ili apate wakati wa kupumzika na awe na nishati tosha ya kitendo kile.
Pia, ni vyema kwa mwanamme kuzungumza na bibi yake na kumwuliza jinsi ambavyo siku yake ilikuwa. Kwa kufanya hivi, utaweza kuelewa ikiwa kuna vitu ambavyo vinamsumbua na jinsi unavyoweza kumsaidia.
Kuendelea kukosa mapenzi nyumbani kutafanya wawili wenu mhisi kana kwamba hampendwi. Wakati ambapo watu wanahisi kuwa hawasikilizwi, hawaonekani wala kueleweka, huenda wakaanza kukasirika ovyo, na hamtaki kuwa pamoja. Baada ya siku ndefu, kila mtu anafanya kazi zake kisha anaenda zake kulala. Hivi ndivyo ndoa husambaratika. Mazungumzo kukosa katika ndoa ni ishara hasi inayopaswa kutatuliwa kwa kasi. Uhusiano wa kimapenzi kati ya wanandoa ni muhimu hata baada ya kupata watoto.
Jinsi ya kutatua suala la bibi kukosa hamu ya kufanya mapenzi

Mazungumzo. Chukua muda kila siku baada ya kazi kuzungumza na bibi yako. Kuwa mpole kwake na usaidie anapotaka msaada wako. Kuzungumza mara kwa mara kutamsaidia kuboresha uwezo wake wa kusema anachotaka ikiwa ana tatizika kufanya hivi.
Kufanya mapenzi kupatiwe kipau mbele
Hata kama ratiba zenu hazina muda tosha wa kuwa pamoja na kufanya mapenzi, hakikisheni kuwa mnapata dakika chache kuwa nyinyi wawili peke yenu. Hata kama ni kuwa na siku fulani na wakati fulani wa kitendo hiki.
Rudisha mambo ya kusisimua
Ikiwa uhusiano wenu hausisimui kama ilivyo hapo awali, mnaweza kurejelea mambo yaliyofanya mhisi furaha hapo awali. Kama kuzuru sehemu tofauti na kuenda hoteli tofauti kila wikendi.
Ni muhimu kwa wanandoa kuzungumza. Badala ya kumwambia mwenzio asichokifanya, mweleze kile ambacho ungependa akufanyie. Je, ungependa msaada katika nyanja gani? Hivi ndivyo mtakavyo boresha uhusiano wenu uliosisimua hapo awali.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Njia 4 Za Kumfanya Mume Wako Kuwa Mwaminifu Kwa Ndoa Yenu