Je, Unamfahamu Bibi Yake Ramsey Nouah?

Je, Unamfahamu Bibi Yake Ramsey Nouah?

Mwigizaji huyu amekuwa kwa tasnia ya uigizaji kwa muda mrefu, ila bibi yake hajulikani sana.

Ramsey Nouah ni mwigizaji maarufu kutoka nchi ya Nigeria iliyoko katika bara la Afrika. Kwa muda mrefu, watu wamekuwa wakimtazama kwa runinga anapo igiza katika sinema. Anawapendeza wanawake wengi na wamekuwa wakijiuliza iwapo ana bibi ama la. Ukweli ni kuwa hata kama wengi hawafahamu bibi yake Ramsey Nouah, yuko na wamebarikiwa na watoto pia. Bibi yake anajulikana kama Emilia Philips Nouah ila hawapendi kuweka maisha yao kwenye mitandao, wanapenda kuyaweka maisha yao mbali na wana habari.

Je, Unamfahamu Bibi Yake Ramsey Nouah?

Chanzo: premiumtimesng.com

Swali kuu ni Emilia Philips Nouah ni nani hasa? Na amewezaje kuyaweka maisha yake fiche kwa muda huo wote?

Ramsey Nouah ni nani hasa?

Kabla kuangazia bibi yake Ramsey Nouah, tuna angazia bwanake ni nani, ili wasio mjua vyema wapate ujumbe zaidi kumhusu na pia maisha yake. Ramsey ni mojawapo wa waigizaji walio maarufu sana katika filamu za Nigeria na anapendwa sana na watu. Ila, hakuanza safari yake kisha akatamba tu, alipitia magumu na kujizatiti hadi akafika alipo leo. Safari yake ilianza akiwa kinyozi, kuteseka kuingia kwenye tasnia ya uigizaji hadi alipo fika alipo na kushinda tuzo nyingi za mwigizaji bora Nigeria na hata Afrika kote.

Wazazi wake ni wa kutoka Nigeria na Israeli, huenda hii ikawa sababu kwanini ana ngozi nyeupe. Alikua Lagos na kujiunga na Chuo Kikuu cha Lagos alipo hitimu na shahada katika Mawasialino ya Wingi (Mass Communication). Alianza kuwa maarufu miaka ya 1990 alipo onekana kwenye programu ya runinga iliyo fahamika kama Fortunes na akanyakua mioyo ya wengi sio Nigeria tu mbali Afrika kote.

Anajulikana kwa kuigiza katika sinema kama vile ‘My Love, The Battle of Love, 30 Days in Atlanta, Silent Night, True Love, The Figurine, Guardian Angel na zinginezo.

Tuzo Za Mwigizaji Huyu

Mwigizaji huyu anaye tanbulika duniani kote na ametuzwa tuzo za tabaka la juu kama vile The Africa Movie Academy Awards na zinginezo.

Bibi yake Ramsy Nouah ni nani?

bibi yake ramsey nouah

Ikilinganishwa na wachumba wa waigizaji wengine, huenda ukapitana na Emilia Philips Nouah bila kujua yeye ni nani. Hii ni kwa sababu ndoa yao sio ya vyumba vya habari na mitandao. Ni vigumu sana kupata habari zao kwenye mitandao, na unapo lisikia jina lake ni wakati ambapo bwanake anaongea na vyombo vya habari na kumsifu bibi yake kwa kumwegemeza.

Emilia Philips Nouah amekuwa katika ndoa na Ramsey kwa muda wa miaka 18 sasa. Hii ni kulingana na ujumbe ambao bwanake alisema alipokuwa akiongea na vyombo vya habari.

Alimsifu bibi yake kwa kusema kuwa bibi yake ndiye anaye ishikilia ndoa yao na ana amini kuweka habari za maisha yao mbali na vyombo vya habari.

Kwa hivyo, watu wanapo mwomba siri za ndoa yenye fanaka, anawaambia kuwa bibi yake ndiye aliye ishikilia familia yake pamoja. Wamebarikiwa na watoto watatu.

Soma pia: Baadhi Ya Wanandoa Nchini Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa

Written by

Risper Nyakio