Orodha Ya Bidhaa Salama Za Kunawa Uso Unapokuwa Na Mimba

Orodha Ya Bidhaa Salama Za Kunawa Uso Unapokuwa Na Mimba

Sio lazima utupilie mbali utaratibu wako wa urembo unapo fuatilia kila siku kwa sababu una mimba. Na hii ndiyo sababu kwa nini unahitaji kutumia bidhaa za kunawa uso katika na mimba. Utahitaji kuboresha utaratibu wako wa kunawa uso kwa sababu mimba huenda ika ibua matatizo ya ngozi kama vile acne, melasma na ngozi iliyo kauka. Bila shaka, nyingi kati ya bidhaa za mimba hazitakuwa sawa unapokuwa na mimba. Unahitaji bidhaa ambazo ni salama kwako na kwa mtoto wako.

Unapaswa kutumia bidhaa za kunawa uso unapokuwa na mimba?

Bila shaka, unaweza! Bidhaa za kunawa uso zitakusaidia kupambana na matatizo ya ngozi. Unapaswa kuwa makini sana unapo fanya hivi. Huwezi tumia bidhaa yoyote ya kunawa uso, ila orodha yetu ya bidhaa bora zaidi za kunawa uso unapokuwa na mimba itakusaidia kufanya uamuzi mzuri. Kama tulivyo taja hapo awali, utaratibu mzuri wa uso unapokuwa na mimba unaweza kusaidia kuwa na ngozi inayo ng'aa unapokuwa mjamzito.

Bidhaa za kujitenga nazo unapo chagua vitu vya kutumia usoni mwako

Tumia bidhaa asili unapo nawa uso wako. Soma maagizo yaliyo andikwa kuhakikisha kuwa ni asili na hazina kemikeli zenye sumu. Kemikali zenye sumu unapokuwa na mimba ni hatari, kwani huenda zikapita kwa mishipa yako ya damu kupitia kwa ngozi. Ni hatari sana kwako na mtoto wako. Iwapo una shaka zozote, wasiliana na daktari wako akushauri zaidi.

Bidhaa za kunawa uso zilizo na mafuta asili ni bora kwa ngozi yako, kwa hivyo wakati wote zichague!

Orodha ya bidhaa salama za kunawa uso unapokuwa mjamzito

Unaweza pata bidhaa hizi za kunawa uso unapokuwa na mimba katika nchi nyingi. Nyingi kati ya hizi hutengenezewa katika nchi ambazo zinapatikana. Unaweza pata bidhaa hizi kwa maduka makubwa ama ya urembo nchini kote.

Ajali Black Soap and Tea Tree Organic Face Soap

bidhaa za kunawa uso katika mimba

Hii ni bidhaa bora kwa kila mtu, iwapo una mimba ama la. Ajali inajulikana hasa katika nchi ya Nigeria, na sabuni hii itaufanya uso wako kung'aa sana unapokuwa na mimba. Hii ni sabuni ya uso asili iliyo tengenezwa kwa kutumia sabuni nyeusi ya Afrika na mafuta ya mti wa chai (tea tree). Inasaidia kutoa acne ya mimba na kuifufua ngozi yako. Unapaswa kuiongeza kwa orodha yako ya utaratibu salama wa uso wako unapokuwa na mimba.

Olay Foaming Face Wash

bidhaa za kunawa uso katika mimba

Hii ni bidhaa nzuri kutoka Olay, na inapaswa kuwa katika orodha yako ya bidhaa salama za kunawa uso unapokuwa na mimba. Ili uwe na ngozi laini, sabuni hii ya Olay inapaswa kuwa katika utaratibu wako wa kunawa uso wa kila siku. Iwapo una tatizika kutokana na acne ya ujauzito, kukauka ama melasma, hii ndiyo sabuni bora kwako!

Bidhaa za kunawa uso unapokuwa na mimba: Mint Organic Care Liquid Wash

List of safe face washes during pregnancy

Kiasi kidogo cha mafuta hii ya uso na mwili kitaiwacha ngozi yako ikiwa laini na iking'aa. Ina patikana katika apricot, bergamot na chai nyeupe, oatmeal na orange. Hii ni lazima kuwa nayo ikiwa una mimba.

Matte Apothecary Liquid Black Soap

bidhaa za kunawa uso katika mimba

Sabuni hii laini huwa na virutubisho muhimu unavyo hitaji kuiweka ngozi yako ikiwa na unyevu na ikiwa safi. Ni sabuni bora kwa ngozi iliyo kauka unapokuwa na mimba. Hutoa seli zilizo kufa na kuboresha ngozi yako na kuwa laini. Kwa matokeo bora, unapaswa kupaka sabuni hii vyema kwa ngozi iliyo na unyevu, kuipiga masi na kuiwacha kwa dakika moja. Sabuni ya Matte Apothecary ya sabuni ya maji nyeusi, ina asali, sharubati ya aloe vera, mafuta ya grape seed, mafuta ya palm kernel, shea butter, mafuta ya jojoba na aina zingine za mafuta.

Adunni Green Tea Face Soap

List of safe face washes during pregnancy
Sabuni hii ya green tea ya uso huwa na moringa, matcha green tea na rosemary. Bidhaa hizi hulinda na kuipa ngozi yako nyepesi ya uso virutubisho unapokuwa na mimba. Unaweza tibu ngozi iliyo kauka na acne ya mimba kutumia sabuni ya uso, na hii ndiyo sababu kwa nini iko katika orodha yetu ya bidhaa salama za kuosha uso unapokuwa na mimba.

Je, una bidhaa zaidi unazo tumia? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi!

Soma pia: Is olive oil good for hair

Written by

Risper Nyakio