Bidhaa Bora Zaidi Za Kunawa Uso Ukiwa Na Mimba

Bidhaa Bora Zaidi Za Kunawa Uso Ukiwa Na Mimba

Hupaswi kutupilia mbali utaratibu wako wa uso na urembo ambao umekua ukifuatilia kwa wakati mrefu kwa sababu una mimba tu. Na hii ndiyo sababu kwa nini unapaswa kutumia bidhaa za kunawa uso ukiwa na mimba. Unapaswa kuongeza bidhaa za utunzaji wako wa uso kwa sababu mimba huja na changamoto tofauti kama vile acne, ama upele wa uso, melasma na kukauka kwa ngozi. Na pia kwa sababu, nyingi kati ya bidhaa za utunzaji wa uso, hazitakufaa unapokuwa na mimba. Una hitaji bidhaa ambazo hazitakudhuru na ni salama kwako na mtoto wako.

Unapaswa Kutumia Bidhaa Za Kunawa Uso Ukiwa Na Mimba?

Bila shaka, unaweza! Bidhaa za kunawa uso zitakusaidia kukumbana na matatizo ya ngozi. Unapaswa kuwa mwangalifu. Huwezi tumia bidha zozote zile, ila orodha yetu ya bidhaa salama za kunawa uso ukiwa na mimba zitakusaidia. Kama tulivyo taja hapo awali, utaratibu ufaao wa utunzaji wa ngozi unapokuwa na mimba unaweza kusaidia kung'ara ipasavyo ukiwa na mimba. Hiyo ni kama uko miongoni mwa wanawake wasiopata uso wa kung'ara wanapokuwa na mimba.

Vitu Vya Kuepuka Unapochagua Bidhaa Za Uso Unapokuwa Na Mimba

Chagua bidhaa za kunawa uso zilizo na viungo ambavyo havija chakatwa. Soma maagizo na uhakikishe kuwa havina vitu vilivyo chakatwa, kwani huenda vikaidhuru ngozi yako. Kemikali mbaya unapokuwa na mimba hazi ruhusiwi. Hautaki kemikali hizi ziingie kwenye mfumo wako wa damu kwa kupitia kwa ngozi yako.

Huenda zikawa hatari sana kwako na mtoto wako. Iwapo una shuku, uliza daktari wako kuhusu vitu unavyo paswa kukaa mbali nazo. Ili kuwa salama, epuka ama punguza matumizi ya bidhaa zinazo kuwa na retinoids na Hydroxyl acids. Hizi huenda zika sababisha matatizo ya mimba na changamoto unapo jifunguu.

Bidhaa za uso zilizo na mafuta asili ni bora kwa ngozi yako, kwa hivyo hakikisha kuwa unazichagua wakati wote!

Orodha Ya Chapa Za Bidhaa Za Uso Zilizo Salama Za Mimba

Unaweza pata bidhaa nzuri za uso za ujauzito katika duka zilizo idhiniwa kuuza bidhaa hizi. Baadhi ya chapa hizi hutengenezewa nchini. Orodha hii pia ina chapa za nchi zingine, ila unaweza zipata kwenye duka kuu nchini kote.

Ajali Black Soap and Tea Tree Organic Face Soap

face wash during pregnancy

Hii ni bidhaa nzuri kwa kila mtu, haijalishi ama una mimba ama la. Ajali inajulikana katika nchi nyingi za Afrika hasa Nigeria na bidhaa yao ya uso itasaidia uso wako kung'aa. Bidhaa hii asili imetengenezwa kwa kutumia sabuni nyeusi ya Afrika na mafuta ya tea tree. Inasaidia kutoa acne ya ujauzito na kuufufua uso. Bila shaka unapaswa kuiongeza kwenye orodha yako ya bidhaa za uso zilizo salama za kutumia wakati wa mimba.

Olay Foaming Face Wash

face wash during pregnancy

Hii ni bidhaa nzuri kutoka kwa Olay, inahitaji kupata mwanya kwenye orodha yetu ya bidhaa salama za uso unapokuwa na mimba. Ili kuwa na ngozi nyororo, Olay Foaming Face Wash inapaswa kuwa miongoni mwa bidhaa unazo tumia kila siku. Iwapo una tatizika kutokana na acne ya mimba, kukauka ngozi ama melasma, hii ndiyo face wash inayo kufaa!

Bidhaa Za Uso Za Mimba: Mint Organic Care Liquid Wash

bidhaa za kunawa uso ukiwa na mimba
Kiasi kidogo cha bidhaa hii ya mwili na uso itaiwacha ngozi yako iki ng'aa bila shaka. Inapatikana katika aina za apricot, bergamot na white tea, oatmeal na orange. Hii ni bidhaa ambayo kila mama mwenye mimba lazima awe nayo.

Matte Apothecary Liquid Black Soap

bidhaa za kunawa uso ukiwa na mimba

Sabuni hii laini huwa na virutubisho muhimu unazo hitaji kuiweka ngozi yako iwe na unyevu na safi. Ni sabuni bora katika kukabiliana na kukauka ngozi kunako sababishwa na mimba. Kutoa seli zilizo kufa na kuboresha ngozi yako. Ili kushuhudia matokeo bora, unapaswa kujipaka sabuni hii vyema uso wako ungali na unyevu, ipapase kisha uiwache kwa dakika moja. Sabuni ya maji ya Matte Apothecary ina asali, maji ya sharubati ya aloe vera, mafuta ya grape seed, mafuta ya kernel, shea butter,na mafuta ya jojoba.

Adunni Green Tea Face Soap

List of safe face washes during pregnancy
Sabuni hii ya uso ya green tea ina moringa, matcha ya chai ya kijani na rosemary. Vitu hivi vinailinda na kuirutubisha ngozi ya uso wako unapokuwa na mimba, Unaweza tengeneza hali ya kukauka ngozi, acne ya mimba kwa kutumia sabuni hii na hii ndiyo sababu kwa nini iko kwenye orodha yetu ya bidhaa salama za kunawa uso ukiwa na mimba.

Je, unatumia bidhaa zipi? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi!

Soma pia: Is olive oil good for hair

Written by

Risper Nyakio