Ugonjwa wa Bidhaa Za Maziwa kwa Watoto: Jinsi ya Kuugundua na Kuutibu

Ugonjwa wa Bidhaa Za Maziwa kwa Watoto: Jinsi ya Kuugundua na Kuutibu

Irrespective of the type of lactose intolerance in baby, it can occur anytime. Therefore, always keep a close eye on its symptoms to catch it at the onset.

Unaweza kuwa unafahamu lactose ni sukari ulioko kwenye bidhaa za maziwa ikiwemo maziwa ya mama. Na ingawaje hivi vyakula ni vya kumnawirisha mdogo wako, ugonjwa wa lactose unaweza kumfanya mtoto wako kuwa na shida kubwa katika kusaga chakula.

Ugonjwa wa bidhaa za maziwa kwa watoto ni hali ambayo mtu hushindwa kusaga lactose iliyoko kwenye bidhaa za maziwa. Ingawaje mlo wa wanga ni chakula cha umuhimu kwa watoto, lazima kisiagwe na kimeng’enya kinachoitwa laktati.

Kwa hivyo, iwapo mwili wa mtoto wako hauna laktati kwa kiwango cha kutosha, haitaweza kusiaga bidhaa za maziwa ama kupata nguvu inayotokana na bidhaa hizi.

Hii inaweza kusababisha visa vilivyokithiri vya shuzi, msokoto, kuhara iwapo itaendelea bila kuzingatiwa.

Kwa kawaida, ugonjwa wa bidhaa za maziwa huwa ya aina tatu

bidhaa za maziwa kwa watoto

 • Ugonjwa wa kuzaliwa nao: Hii aina hutokea kwa sababu ya upungufu wa kimeng’enya laktati ambacho husaga bidhaa za maziwa ambazo mtoto hula.
 • Ugonjwa wa Kimsingi: Hii aina hutokea iwapo mtoto atazaliwa na vipimo vya chini vya laktati.
 • Ugonjwa wa sekondari: Hii hutokea mtoto anapougua kutokana na ugonjwa mwingine kama vile vimbizi au kuhara na hii inasababisha ugonjwa wa bidhaa za maziwa.

Hata na ufahamu huu, wakati mwingine ni vigumu kutambua ugonjwa wa bidhaa za maziwa kwenye watoto kwa mara moja.

Utahitaji kutiliia akilini dalili fulani ambazo huashiria hii hali kwenye mdogo wako.

bidhaa za maziwa kwa watoto

Dalili za ugonjwa wa bidhaa za maziwa kwa watoto

Kwa kawaida, dalili za ugonjwa wa bidhaa za maziwa kwa watoto hutofautiana kutoka kwa mmoja hadi mwingine.  Lakini kwa kawaida, utaweza kugundua hii hali kwa mtoto iwapo ana matatizo haya.

 • Shuzi
 • Maumivu ya tumbo
 • Kuhara
 • Kufungia kwa hewa
 • Choo kilicho majimaji
 • Msokoto
 • Kulia kwa mara kwa mara na kusumbuka
 • Kelele matumbo yanaposonga
 • Kutapika

Moja au nyingi za hizi dalili zinaweza kutokea dakika chache au masaa baada ya kutumia maziwa au bidhaa za maziwa. Hata hivyo, kwa kuwa hizi dalili hutokea sadifu na matatizo mengine ya kiafya kwenye mtoto kama vile joto inaweza kuwa vigumu kutambua kama ugonjwa wa bidhaa za maziwa.

Lakini iwapo una shuku mtoto wako ana ugonjwa wa bidhaa za maziwa, unafaa kumleta kwa daktari wa watoto bila kuchelewa.  Daktari anaweza kufanya uchunguzi kuhakikisha kuwa kwa kweli mtoto wako ana ugonjwa wa bidhaa za maziwa.

Vipimo Vya Kudhibitisha ugonjwa wa bidhaa za maziwa kwa watoto
Ugonjwa wa Bidhaa Za Maziwa kwa Watoto: Jinsi ya Kuugundua na Kuutibu

Unless your doctor specifically asks you not to or the child is highly symptomatic, do not stop breastfeeding. | Image courtesy: Pixabay

Kwa kawaida, daktari atafikia uamuzi kuwa mtoto ana ugonjwa wa bidhaa za maziwa ikiwa atagundua dalili mbili ama tatu. Hii itakuwa kweli kwa aliyezaliwa na ugonjwa wa bidhaa za maziwa.

1. Aliyezaliwa na ugonjwa wa bidhaa za maziwa

Kukosa kuongeza mizani, kutapika kwa mara kwa mara, kuhara na maumivu ya tumbo zaweza kuchukuliwa kwa pamoja kama dalili za ugonjwa wa bidhaa za maziwa.

Sasa, iwapo hizi dalili zimeongezewa mizani na vipimo vya kinyesi itabidi umekoma kumpa mtoto wako bidhaa za maziwa.

Kuna bidhaa nyingi za maziwa sisizo na lactose zanazouzwa unazoweza kujaribu. Lakini kama daktari wako hajakuuliza kuacha kunyonyesha ama mtoto hana dalili nyingi  usiache kumnyonyesha. Kwa kesi nadra, madaktari wanaweza kuuliza kutomnyonyesha mtoto kuchunguza kama dalili zitarejea.

2. Ugonjwa wa Kimsingi wa bidhaa za maziwa

Kwa aina hii ya ugonjwa wa bidhaa za maziwa, daktari anaweza kupendekeza kumpa mtoto wako bidhaa zisizo na lactose kwa muda kumchunguza.

Muda huu unaweza kuwa siku chache ama wiki chache kulingana na shida ilivyokithiri.

3. Ugonjwa wa sekondari wa bidhaa za maziwa

Mtoto anapougua kutokana na hii aina, anaweza kuhara ama kutapika kuzidi mipaka. Huu wakati unaweza shauriwa usimpe bidhaa za maziwa kwa wakati mpaka apate nafuu.

Akipata nafuu, unaweza anza kumpa bidhaa za maziwa. Mara nyingi huu wakati huwawezesha watoto kuongeza mizani na kupata nafuu na wanaweza kusaga bidhaa za maziwa kwa kipindi kirefu kijacho.

Bila kuzingatia ni aina gani ya ugonjwa wa bidhaa za maziwa mtoto wako aliyo nayo, kumbuka inaweza kutokea wakati wowote. Si lazima iwe anapoanza kula vyakula vigumu ama anapotumia maziwa pekee.

Ingawa, mtoto aliyezaliwa na ugonjwa wa bidhaa za maziwa na aliye na aina ya Kimsingi, watakuwa na huu ugonjwa pindi wakiwa wadogo.

Mtoto aliye na aina ya sekondari, hio hali inaweza kuwa sawa kwa wakati. Njia yoyote ile, itabidi unachunguza dalili kwa makini na kumpeleka mtoto kwa daktari kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa.

 

Source: HealthlineIndian Express

Feature and lead image courtesy: Pixabay

Read also: Giving your baby eggs can prevent future allergies

Written by

Risper Nyakio