Bidhaa Asili Za Kutumia Kwenye Nywele Ya Mtoto Wako

Bidhaa Asili Za Kutumia Kwenye Nywele Ya Mtoto Wako

Katika hatua fulani maishani, wamama hasa kutoka Afrika watafanya uamuzi kuhusu bidhaa za nywele za watoto ambazo atazitumia kwa watoto wake. Wanawake wengi walikua na perms na kutumia bidhaa zilizo kuwa maarifa wakati huo. Katika nyakati hizi, watu wanatumia bidhaa asili na kufanya wanawake wengi wabadili bidhaa za nywele ambazo walikuwa wanatumia. Wamama wengi huenda waka jiuliza iwapo kuna maana ya kutumia bidhaa za nywele ama kuwacha nywele za watoto wao zibaki hivyo.

Bidhaa asili za nywele za watoto:

natural hair products for kids

Je, bidhaa maarufu kama relaxers hufanya kazi vipi?

Relaxers ni krimu zinazo saidia kuinyoosha nywele ama kuifanya kuwa na muundo wa wavu. Zina tengenezwa na kemikali zinazo saidia kubadilisha muundo wa nywele na ikiwa ngumu iwe rahisi zaidi. Kiungo kinacho tumika zaidi kutengeneza bidhaa hizi ni sodium hydroxide.

Nywele itahitaji kuoshwa kwa bidhaa hii mara kwa mara, hadi baada ya wiki 6-9, ili nywele zinazokua pia ziwe laini na rahisi.

Ni vyema kutumia relaxer kwa nywele ya mtoto?

Jambo la kwanza unalo paswa kuelewa ni kuwa ni chaguo lako! Iwapo unafanya uamuzi wa kutumia bidhaa za relaxer kwa watoto wako ama una amua kutumia bidhaa asili kwenye nywele ya watoto wako, unapaswa kuelewa kuwa ni mwito wako. Kwa hivyo, unapaswa kuhakikisha kuwa afya na usalama wa mtoto wako uko sawa, chaguo unalo fanya ni lako. Kitu ambacho unapaswa kuwa na shaka nacho ni jinsi ya kuweka mitindo ya nywele kwenye watoto wako. Nywele safi iliyo na mtindo wa kisasa unatawala, haijalishi iwapo nywele imetumia bidhaa za kuilanisha ama la. Unaweza tumia bidhaa za kulainisha nywele ya mtoto wako ama kuziwacha hivyo, lakini uhakikishe kuwa nywele ina pendeza.

natural hair products for kidsKwa nini wazazi huamua kutumia bidhaa za kulainisha nywele ya watoto wao

Wazazi wengi hukiri kuwa bidhaa za kulainisha nywele hufanya nywele kwa wana wachanga wao ziwe rahisi kusonga. Wanao unga mkono utumizi wa bidhaa hizi husema kuwa nywele ni rahisi kuchana na kuweka miundo tofauti ikilinganishwa na nywele asili. Kwa sababu wazazi hawataki watoto wao walie wanapo sukwa, wanafanya uamuzi wa kutumia bidhaa hizi ili nywele iwe rahisi kusuka.

Nywele asili huenda ikawa ngumu kuchana kwa mama ama iwapo msusi hajazoea kusuka nywele ngumu na kutumia bidhaa asili za nywele za watoto. Na kwa sababu hii, huenda mtoto akahisi uchungu sana anapo jaribu kuichana ama kuiweka mitindo tofauti. Hii huwa ngumu zaidi wakati ambapo nywele ya mtoto ni nene na ngozi ya kichwa chake ni laini.

Unapo paswa kutumia bidhaa za kulainisha nywele ya mtoto wako

Bila hata kusema, kila mama anafahamu kuwa bidhaa hizi hutengenezwa kwa kemikali nyingi ambazo huenda zika athiri ngozi ya mtoto mdogo kwa sababu ngozi yake bado laini. Kwa hivyo hupaswi kutumia bidhaa hizi mapema sana kwenye maisha ya mtoto wako.

Wakati bora zaidi wa kutumia bidhaa za kulainisha nywele ya mtoto wako ni anapo kuwa na umri wa kufanya uamuzi iwapo angependa bidhaa hizi zitumiwe kwenye kichwa chake ama angependa zibaki asili. Ni nywele yao na wana kubalika kufanya uamuzi. Watoto kutoka umri wa miaka 12 wana umri tosha wa kufanya uamuzi. Ikiwa mtoto wako haja timiza umri wa kufanya uamuzi, unaweza endelea kutunza nywele zao kwa kutumia bidhaa asili za nywele za watoto. Lengo ni kuwa na nywele zenye afya.

Mambo muhimu ya kujua kabla ya kutumia bidhaa za kulainisha nywele kwa wana wachanga

• Bidhaa za kulainisha nywele huwa na kemikali nyingi na huenda zikafanya madhara mengi kuliko faida
• Nywele zinazo tumia bidhaa hizi zina hatari za kukauka, kuwa nyembamba ama kukatika
• Wakati wote unapo taka kutumia bidhaa hizi, hakikisha unampeleka mtoto kwa msusi aliye na cheti cha kutengeneza nywele za watoto
• Iwapo bidhaa hii inabaki nyweleni kwa muda mrefu, huenda ika sababisha kuchomeka kichwani ama mtoto kuhisi vibaya
• Tumia bidhaa hasa za watoto kwa sababu hazina kiwango kikubwa cha kemikali ikilinganishwa na bidhaa za watu wazima
• Unaweza tengeneza nywele za watoto wako ziwe mitindo tofauti kwa kutumia bidhaa asili za nywele

Jinsi ya kulainisha nywele ya mtoto wako kwa usalama

• Soma kiji sanduku cha bidhaa hiyo na ufuate maagizo kwa utaratibu
• Mpake mafuta kwanza kwenye ngozi yake ili bidhaa hiyo isiguse ngozi ya mtoto
• Usitumie bidhaa ya kulainisha nywele kwa kichwa kilicho safishwa hivi karibuni (uchafu na mafuta yana ilinda ngozi kuto chomeka)
• Baada ya kuipaka bidhaa ile ya kulainisha nywele, hakikisha kuwa unasafisha mabaki yote ya bidhaa hii kwa kutumia shampoo.

Kumbukumbu: International Journal of Trichology

Soma pia: Mitindo Ya Kusongwa Nywele Za Kurudi Shuleni Inayo Pendeza

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio