Binti yake amefikisha miezi mitano leo, Corazon Kwamboka alisherehekea hatua hii katika maishani mwa mtoto wake.
Siku ya Jumapili ilikuwa siku ya kusherehekea mama duniani kote. Corazon Kwamboka aliandika ujumbe wa kugusa moyo kwenye kurasa yake ya Instagram.
Ujumbe wa mother’s day
Picha: Corazon Kwamboka Instagram
Binti yangu mrembo anafikisha miezi mitano leo. Nitasherehekea kila mwezi unapoongeza umri, ni hatua kwangu pia. Ulikuwa miezi miwili tu nilipoingia kwa dunia isiyojulikana, kwa kasi, ilinibidi nitambue jinsi ya kukulea na moyo uliovunjika na peke yangu. Ulinipa nguvu nyingi. Ungeniangalia na kulia nami, nilihisi jinsi ulivyohuzunika kwani nilikuwa na huzuni. Kufahamu kuwa ulikuwa unanitegemea kulinipa nguvu za kuamka, kujipanguza na kukuishia. Kukuona ukikaa chini sasa na kucheka ninapokuchezesha huufurahisha moyo wangu. Wewe ni baraka kwetu. Nguvu zangu. Nakupenda kwa dhati. Corazon aliandika.
Kuzaliwa kwa binti yakebinti yake corazon kwamboka Corazon Kwamboka, Koko Kiarie
Picha: Corazon Kwamboka Instagram
Corazon alijifungua binti yake tarehe 8 Disemba mwaka wa 2021. Kwa njia ya upasuaji. Hakupitia uchungu wa uzazi, ila alikaa kwenye chumba cha upasuaji kwa lisaa limoja na dakika 30. Kisha masaa sita ya kulala kwa mgongo akiwekwa matone, bila kuweza kugeuka, kisha akamshika mwanawe mikononi.
Picha: Corazon kwamboka Instagram
Koko Kiarie, mwanawe Corazon Kwamboka na Frank amekuwa akiwavutia watu kwa picha zake rembo ambazo wazazi wake wamekuwa wakiweka kwenye kurasa zao za mitandao. Kwa sasa Corazon amebarikiwa na watoto wawili. Kifungua mimba wake Taiyari Kiarie aliyezaliwa Agosti 3 mwaka wa 2020 na Koko Kiarie mwenye miezi mitano.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Corazon Kwamboka Na Frankie Watengana Baada Ya Kuwa Pamoja Kwa Miaka Mitatu