Jinsi Ya Kujua Iwapo Mwanamme WaKo Ana Umiliki Wa Sumu

Jinsi Ya Kujua Iwapo Mwanamme WaKo Ana Umiliki Wa Sumu

Ishara hizi za mchumba mwenye umiliki wa sumu zitakusaidia kujua aina ya mchumba unaye paswa kujitenga naye.

Kuwa na bwana mwenye umiliki wa sumu ni mojawapo ya mambo yanayo fanya mwanamke kukosa amani maishani. Pia kukosa nafasi ya kuzungumza mawazo yako huenda yakakufanya uhisi kana kwamba hauna nishati tosha mwilini. Bila ujuzi, uhusiano wa aina hii huanza na mapenzi mengi na kuona kuwa hakuna aliye kama bwanako. Hadi pale ambapo utaanza kuona ishara hasi. Anasahau kuheshimu mipaka yako na kuanza kufanya mambo ambayo yana kufanya uhisi kuwa hau heshimiwi. Hata kama unapaswa kutoka kwa uhusiano ambapo hau heshimiwi, wanao kuwa kwa ndoa na uhusiano kama huu, hukaa kwani baada ya makosa, wachumba wao huomba msamaha, kufanya matendo ya kimapenzi na kufanya wachumba wao waone kuwa matendo yao yali sababishwa na wachumba wao ila sio kutaka ama hiari zao. Kuna ishara bayana za kujua iwapo bwana wako ana umiliki wa usumu ili uondoke mapema kabla ya kuingia kwa mapenzi ya dhati na ambapo unayafungia mambo mengi macho.

bwana mwenye umiliki wa sumu

Mapenzi na ndoa ya afya ni pale ambapo watu wawili wana malengo sawa na mapenzi ya kweli na hawana nia hasi fiche kati yao. Ila kuna imani isiyo ya kweli kuwa mtu anapaswa kutupilia mbali vitu anavyo penda kufanya maishani ili kuwa na mchumba wake. Huenda kukawa na vitu ambavyo utapunguza, ila hata jaribu kukutenga na jamii na marafiki wako. Na ikiwa kuna mabadiliko yatakayo fanyika, ni kutoka kwa pande zote mbili ila sio kwa moja. Makala haya yana kuelimisha zaidi jinsi ya kujua iwapo mchumba wako ana umiliki wa sumu. Soma zaidi upate kujua iwapo ni wakati wa kutoka kwa ndoa yako.

Jinsi Ya Kujua Iwapo Una Bwana Mwenye Umiliki Wa Sumu

how to tell if a man is dominant

  • Hapendi unapokuwa na maoni tofauti

Wachumba wenye umiliki wa sumu hawapendi watu wengine wanapo kuwa na maoni tofauti nao. Jambo hili huenda lika zua ugomvi na vita katika ndoa ama uhusiano. Katika uhusiano wenye afya, kila mtu anapaswa kuwa na maoni yake tofauti na kuwa na uhuru wa kuyasema bila hofu ya huyo  mwingine. Ukigundua kuwa mchumba wako hapendi unapo kuwa na usemi tofauti na wake, jua kuwa na umiliki wa sumu na ni vyema kumweleza kuwa haupendelei jambo hilo ama hata kuondoka kutoka kwa uhusiano huo.

  • Kukuangalia kwa njia fulani ili unyamaze

Jinsi Ya Kujua Iwapo Mwanamme WaKo Ana Umiliki Wa Sumu

Hii ni mojawapo ya ishara maarufu zaidi za mwanamme aliye na umiliki sumu. Huenda kuwa mlikuwa katikati ya mazungumzo yenu unapo sema hisia zako kisha anakuangalia kwa njia fulani. Bila shaka, bila hata yeye kusema, unajua kuwa unapaswa kunyamaza. Inakuwa tendo unalo lifanya tu bila ujuzi wako mara tu anapo kuangalia kwa njia fulani. Aina hii ya umiliki huwa na matokeo hasi kwa hisia zako. Utaanza kuhisi kana kwamba unapaswa kufanya kila kitu anacho kwambia.

  • Haheshimu nafasi yako

Kwa bwana mwenye umiliki wa sumu, unapaswa kuwa naye wakati wowote ule ama anapo kutaka uwe karibu naye. Hupaswi kuwa na marafiki, familia yako ama hata kufanya vitu vinavyo kufurahisha. Unakuwa kama mfungwa wake. Huenda hata akawa anafuata matendo yako ili kuhakikisha kuwa unajua kila kitu unacho fanya ama mahali popote pale ulipo. Iwapo unafanya kitu kisicho mfurahisha, hilo linakuwa ni tatizo. Kulingana na wataalum wa mahusiano, tabia hii ina sababishwa na hofu kuwa huenda ukawaambia watu wengine kuhusu tabia zao za kukumiliki.

Tukianza kuongea kuhusu wachumba wetu na matendo yao kwetu, marafiki wetu watatujulisha iwapo tuko katika mahusiano yenye sumu na huenda wakaanza kutushauri tufunge virago vyetu. Mtaalum yule alizidisha kusema.

  • Jinsi ya kujua una bwana mwenye umiliki wa sumu: kuku rekebisha mnapo zungumza

Hii ni njia bayana ya kujua iwapo bwanako anakumiliki kwa njia isiyo faa. Unapo fanya kosa ndogo tu kwa matamshi yako, hangoji umalize sentensi yako ama ulicho kuwa ukisema. Anaruka na kukurekebisha, na mara nyingi, hafanyi hivi kwa mapenzi na upendo. Jambo hili linakufanya ukose kuwa na uhakika unapokuwa naye. Hata hauna hamu ya kuongea naye. Hii ni ishara kuwa anakumiliki. Hana haja kujua jinsi siku yako ilivyo kuwa.

  • Wewe ni msichana wa kunoa

bwana mwenye umiliki wa sumu

Ishara ingine ya mwanamme mwenye umiliki wa sumu ni kuwa hachukui majukumu ya matendo yake. Matendo yake kwa wakati wote huwa kwa sababu ya jinsi ulivyo fanya, ulichosema ama kwa kukosa kuto fanya kitu fulani. Anapaswa kujua kuwa matendo yake ni jukumu lake anacho fanya. Unapaswa kuwa makini na kusema mipaka ambayo hapaswi kuvuka. Akifanya tendo mbaya, anapaswa kuhakikisha kuwa amewajibika na kuomba msamaha anapo fanya jambo lisilo faa. Kwa njia hii utakuwa na uhakika kuwa ataanza kuwajibika. Ukinyamaza anapo vuka mipaka hii, ataendelea kufanya mambo yasiyo faa kwani hautafanya chochote.

Hitimisho

Bwana mwenye umiliki wa sumu atakuwa na hisia za kuonekana mkubwa katika kila kitu, kihisia, na hata mnapo kuwa nyumbani. Bila shaka huyu ni mchumba ambaye huwezi penda kuwa naye milele. Mchumba mzuri na anaye kupenda wakati wowote angependa uhisi kuwa unapendwa na uko huru kusema na kufanya unacho taka. Watakuwa tofauti ya wachumba wenye umiliki wa sumu. Iwapo una mchumba mwenye umiliki wa sumu, usi site kuomba ushauri na usaidizi kutoka kwa wataalum.

Soma pia: Mambo Ya Kufanya Mchumba Wako Anapo Sema Mambo Ya Kuumiza

Written by

Risper Nyakio