Je, Kuna Uwezekano Kuwa Bwanako Anakufanya Ugonjeke?

Je, Kuna Uwezekano Kuwa Bwanako Anakufanya Ugonjeke?

Utafiti una dhihirisha kuwa mume wako huenda akakufanya ugonjeka anapo fanya mambo haya. Soma zaidi.

Je, mara kwa mara wewe hugonjeka ukiwa nyumbani? Ama uligundua kuwa tangu ufunge ndoa afya yako imedhoofika? Kuna vitu vingi ambavyo huenda vina sababisha, lakini ushawahi fikiria kuwa, huenda ikawa ni bwanako anakufanya ugonjeke?

Utashangaa kugundua kuwa, hata kama inaonekana kama jambo ambalo haliwezi tendeka, ni ukweli. Hapa kuna njia saba bwanako anaweza kufanya ugonjeke.

Je, bwanako anakufanya ugonjeke?

1.Mume wako anaweza kuvunja roho

bwanako anakufanya ugonjeke

Unafahamu kuwa "kuvunjwa roho" si usemi tu? Kuna uwezekano wa mtu kuwa na matatizo wanapo kosa furaha ama kuwa na huzuni.

Hii hasa ni kweli katika ndoa ambapo kuna matatizo mengi. Utafiti umegundua kuwa wanawake walio katika ndoa zisizo na furaha wako katika hatari ya kuugua maradhi ya moyo ikilinganishwa kwa walio katika ndoa zenye furaha.

Pia, wanawake wana athiriwa zaidi ikilinganishwa na wanaume kwani wanawake huwa na uraibu wa kubeba hisia nyingi. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unaongea na bwanako ukiwa na fikira zozote.

2. Kukoroma huenda kukawa tatizo kubwa

Je, bwanako hukoroma kwa sauti? Kama yeye hufanya hivyo, huenda ikawa jambo hili linakufanya kuwa mgonjwa.

Wanaume wanao koroma kwa nguvu husababisha matatizo kwa wake zao kwani wake zao huwa na wakati mgumu kupata usingizi. Kukoroma kunaweza fanya watu wengine kuamka kutoka kwa usingizi mzito, ambao ni muhimu kwa mchakato wa kupona kwa mwili.

Cha zaidi ni kuwa, watu wanao koroma kwa nguvu wanaweza sababisha matatizo ya kusikia kwa wenzi wao.

Kwa hivyo ikiwa bwanako hukoroma kwa nguvu, jaribu kumtembelea daktari kuona atakavyo wasaidia.

3. Huenda ukawa na mzio wa ngono

Kuna watu walio na mzio wa ngono kifizikia. Wana tatizika na mzio wanapo patana na shahawa na kuwafanya wahisi uchungu ama kuwashwa. Kwa bahati nzuri, kuna matibabu kwa hali hii. Hakikisha kuwa unaongea na daktari wako.

4. Kukorofishana na kufilisika kimawazo kuna punguza uponaji

bwanako anakufanya ugonjeke

Wewe hukorofishana mara kwa mara na mwenzi wako? Una fikira nyingi kwa sababu ya kukosana? Nafasi nyingi ni kuwa, ina sababisha mwili wako kupona polepole.

Hii ni kwa sababu watu wanao korofishana ama kuwa na ugomvi huwa na kiwango cha chini cha homoni ya oxytocin mwilini. Oxytocin ina saidia kwa kulinda mwili wako na inakusaidia kupona haraka. Maarufu kama "homoni ya mapenzi."

5. Ndevu zinaweza sababisha maradhi ya ngozi

Ndevu za mume wako hata kama zina penda huenda zika sababisha maradhi ya ngozi.

Hii ni kwa sababu viini huenda baadhi ya wakati vikakwama kwenye ndevu zake. Hasa ikiwa ana uraibu wa kujigusa na mikono michafu. Na viini hivi kusambazwa unapo karibia uso wake ama kumbusu.

Hakikisha kuwa kuwa mume wako ana nyolewa mara kwa mara. Ikiwa anataka kuwa na ndevu, ana hitaji kuhakikisha ni safi na kunawa uso mara kwa mara.

6. Yeye ndiye sababu unalewa mara kwa mara

Kulingana na utafiti ulio fanywa, wanawake wanao lewa sana huathiriwa na waume wao. Waume walio funga ndoa hawalewi sana kama wanaume sio katika ndoa, lakini wanawake huwa na uraibu wa kujaribu kuwaiga bwana zao. Na bila shaka vileo vingi vita sababisha ugonjwa baadaye maishani.

Kwa hivyo, ikiwa bwanako hulewa sana, ni vyema kuwa na mazungumzo ya kupunguza vileo.

7. Bwanako anakufanya ugonjeke? Mumewako huenda akawa ana kufanya kuwa mnene

Kulingana na utafiti, watu katika ndoa zenye furaha huongeza uzito baada ya wakati.

Hii ni kwa sababu ikiwa uko peke yako, unajaribu kupendeza ili upate mchumba. Walakini, unapo funga ndoa, una uraibu wa kutupilia hilo mbali.

Kwa nini usijaribu kurudi kwa uzito wa ujana wako na umhimize bwanako kufanya mazoezi nawe? Nyote mtakuwa na afya na mpate wakati tosha wa kutangamana.

Vyanzo: Washington Post, CNN, Healthline, Psychology Today

Soma Pia:Jinsi Ya Kufurahia Maisha Yako Ya Ndoa Kama Mwafrika

Written by

Risper Nyakio