Bwanangu Anapuuza Mahitaji Yangu Ya Ngono, Nitafanyaje?

Bwanangu Anapuuza Mahitaji Yangu Ya Ngono, Nitafanyaje?

Iwapo bwanangu anapuuza mahitaji yangu ya ngono ni suala unalo pitia, huenda ukahitaji msaada kupata ladha iliyopotea ya chumba chenu cha kulala.

Sababu kwanini hakuna ngono kwenye ndoa yenu

Badala ya kuhisi vibaya kuhusu bwanako kutokuwa na haja yako ya kimapenzi, unapaswa kujua kwa nini unashuhudia ndoa bila ngono. Ukifahamu chanzo cha tatizo, utafahamu hatua unazo paswa kuchukua kutatua shida hiyo.

Hizi ndizo baadhi ya vitu zinazo ua ngono kwenye ndoa:

1. Uchovu na Kukwazwa Kimawazo

Iwapo mara kwa mara unatafuta "bwanangu anapuuza mahitaji yangu ya kingono" kwenye mtandao, utahitaji kuangalia kwa kina na urefu viwango vyake vya kukwazwa kimawazo. Huenda fikira hizi zikawa hazitoki nyumbani; huenda ikamaanisha kuwa anaweka masaa mengi kwenye kazi yake, na kufanya achoke zaidi kujihusisha na ngono anapo fika nyumbani.

my husband ignores me sexually

2. Kutokua Salama

Huenda bwanako akawa anaepuka kufanya ngono na wewe kwasababu anahisi hana usalama na wewe. Unaweka jitihada kumwonyesha kuwa unafurahia ngono na yeye? Huenda akajitenga anapo hisi kuwa hakufanyii chochote kingono.

3. Migogoro ambayo  haijatatuliwa

Huenda ngono ikakosa hisia mnapokuwa mmekosana. Kadri unavyo kubalisha chuki na kutoskizana kuendelea, ndivyo vitu vitazidi kuharibika. Unaweza kubaliana nasi kuwa kuchukiana kutapunguza uwezo wenu kufurahia ngono.

my husband ignores me sexually

4. Kukemeana na Kukosa uwezo wa kujieleza

Unaweza badili wimbo wako kutoka kwa, bwanangu hupuuza mahitaji yangu ya kingono uwe, hatuwezi shibana. Ila lazima utafute njia ya kukabiliana na matatizo mnayo yapitia kwa sasa. Ni muhimu kujua jinsi ya kujieleza usipotosheka na jambo fulani. Iwapo kuna kitu ungependa akufanyie cha kingono, ongea, ila usipo jieleza vyema, huenda likawa tatizo.

Bwanangu anapuuza mahitaji yangu ya ngono- jinsi ya kusuluhisha tatizo hili

Ladha inaweza rudi chumbani chenu cha kulala, ila, lazima utie bidii!

my husband ignores me sexually

Jinsi za kumfanya bwanako awe na hamu yako:

1. Ongea kulihusu

Lazima ukubali kuwa kuna tatizo kabla ya kutafuta mbinu za kulitatua. Huenda bwanako akakosa kujua kuwa anapuuza mahitaji yako ya kingono. Mwambie unavyo hisi, ila, kumbuka kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kuwa kwa upole na kuelewana, sio vita.

2. Sikiza ana yapi ya kusema

Kwa sasa kwani umemweleza kuhusu kuto tosheleka kwako kingono, lazima usikize sababu zake ni zipi. Kuwa mtulivu na umsikize. Jaribu kuto ingilia mazungumzo yake hadi pale anapo maliza. Nyote wawili mnaweza pata suluhu za matatizo yoyote yale anayokuwa akiyapitia.

3. Jaribu kurudiana

Kurudiana mlivyo kuwa hapo awali haitakuwa rahisi, hasa iwapo hamu yenu ya ngono imetatizika kwa muda. Tieni bidii kurejesha hamu ya kingono. Jaribu kuangalia mchumba wako anavyo endelea kila siku. Baada ya kazi, kaeni chini mjadiliane siku zenu zilivyo kuwa. Kutoka hapo, mnaweza kuwa na mazungumzo ya hisia zenu. Tafuteni siku hasa ya ngono, kwa matumaini kuwa hamu ya siku hiyo kufika itarejesha uhusiano wenu.

4. Mchumba wako anapaswa kujua matarajio yako ya kingono na vitu unavyo vipendelea.

Kwa kisa ambacho na hisi kuwa bwanangu anapuuza mahitaji yangu ya ngono, huenda shida ikawa, hajui kinacho kupendeza wakati wa ngono. Chukua muda kumweleza fikira zako fiche kuhusu ngono na kuchukua jukumu tofauti mnapokuwa mkifanya mapenzi.

5. Wacha mapenzi yajaze nyumbani mwenu

Kutengeneza mazingira yenye amani na upendo yata ongeza nafasi za kuwa na uhusiano wa karibu wa kingono na mumeo. Ngono itatendeka pale ambapo mazingara yako sawa, kwa hivyo, fanya juhudi!

Kwa hitimisho, kunawezekana kubadili ndoa yako kutoka kwa muungano usio na ngono uwe muungano uliojazwa na mapenzi. Unahitaji kufuata vidokezo hivi kurejesha ladha iliyokuwa hapo awali ya mapenzi na ngono. kwa bahati njema, wewe na mumeo mtarudi mlipokuwa hapo awali.

Chanzo: The Guardian

Soma pia: Safe Sex without Protection: How to UP your game!

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio