Je, Kuna Idadi Ya Upasuaji Wa C-Section Ambayo Hustahili Kupitisha?

Je, Kuna Idadi Ya Upasuaji Wa C-Section Ambayo Hustahili Kupitisha?

Na kwa mama ambaye mtoto wake wa kwanza alizaliwa kupitia upasuaji wa C-section, kuna nafasi ya asilimia 90 kuwa mtoto wake wa pili pia atazaliwa kupitia njia sawa.

Siku hizi, kujifungua kupitia njia ya upasuaji wa C-section inazidi kuwa maarufu na wanadada zaidi wana amua kuenda njia hii ya kujifungua ikilinganishwa na kujifungua kwa kawaida. Kwa hivyo, ni idadi gani ya upasuaji wa C-section salama kwa mama kupata?

Na kwa mama ambaye mtoto wake wa kwanza alizaliwa kupitia upasuaji wa C-section, kuna nafasi ya asilimia 90 kuwa mtoto wake wa pili pia atazaliwa kupitia njia sawa.

Ni C-section ngapi salama kwa mama kupata?

 

Je, Kuna Idadi Ya Upasuaji Wa C-Section Ambayo Hustahili Kupitisha?

Kwa kiwango kikubwa, hakuna jibu hasa la swali hilo la idadi ya C-section salama kwa mama.

Walakini, madaktari wanakubaliana kuwa kadri mama anavyo pata C-section nyingi, ndivyo anavyo kuwa kwa hatari zaidi.

Daktari Marra Francis alisema, "Kwa kawaida, upasuaji mmoja ama mara mbili hakuna hatari iliyo ongezeka kwa mama ama mtoto." Pia, zahanati ya Mayo Clinic ilisema kuwa hatari ina ongezeka baada ya mama kupokea upasuaji mara ya tatu, lakini hakuna nambari hasa ya upasuaji wa c-section iliyo salama.

Hatari ni zipi?

signs of infection after c section

Hapa kuna hatari zinazo husishwa na upasuaji mara nyingi:

  1. Alama -  kila mara unapo pata upasuaji wa C-section, kutakuwa na alama za nje na ndani. Idadi nyingi ya alama hizi kunaweza fanya upasuaji ujao wa C-section uwe na matatizo.
  2. Matatizo ya placenta - baada ya upasuaji wa aina hii mara nyingi, placenta yako huenda baadhi ya wakati ikajipandikiza sana kwenye uterasi yako, ama baadhi ya wakati hata kwenye mlango wa kizazi chako.
  3. Majeraha ya kibofu - wakati ambapo sio jambo linalo tendeka mara kwa mara, hili huja na kupata C-sections nyingi.
  4. Kuvuja damu sana -  kuvuja damu sana ni hatari inayo andamana na C-sections, idadi ya c-sections inapo ongezeka, sawa na hatari ya kuvuja damu sana. Katika baadhi ya visa, huenda ika hitaji hysterectomy ambapo uterasi inatolewa.

Katika mwisho wa siku, ni muhimu mazungumzo marefu na daktari wako na uwaze kuhusu maoni yao unapo fanya uamuzi wa kupata upasuaji wa C-section ama kujifungua kwa njia asili. Kwa njia hiyo, unaweza fanya uamuzi wa njia itakayo wafaa zaidi, wewe na mtoto wako.

Chanzo: familyshare.com

Soma Pia:Jinsi Ya Kujitayarisha Usiku Kabla Ya Upasuaji Wa C-Section

Written by

Risper Nyakio