Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

4masomo ya dakika
Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Naam, je ungependa kuoleka ama ushafunga ndoa tayari? Iwapo umefunga ndoa ama unaazimia kufunga ndoa hivi karibuni, najua kuna baadhi ya wanandoa wanao kufanya utamani kuwa kama wao. Nani celebrity couple goals in Kenya unaye enzi zaidi?

Baadhi ya Celebrity Couple Goals in Kenya

Wahu na Nameless

wahu na nameless

Nameless na bibiye Wahu. Picha shukrani kwa Standard Media

Wanandoa wanao wapa watu wengi Kenya usiku bila usingizi. Wanasherehekewa kwa kuwa watu wa kuigwa kwenye jamii. Safari yao ya mapenzi ilianza tangu siku zao za chuo kikuu kwani walikuwa chuo kimoja. Baada ya kuwa marafiki na kuonana miaka 7 walifunga pingu za maisha mwaka wa 2005. Wahu alipokubali mwito wa Nameless (jina lake la usanii) wa kuwa bibi yake, kwa mazuri na mabaya, utajiri na umasikini. Wawili hawa wamepitia matatizo kwenye ndoa yao, ila, wameionyesha dunia kuwa wawili walio kubaliana, wana nguvu ya kupambana na mambo yote ambayo maisha inawarushia. Wamebarikiwa na wasichana wawili warembo kupindukia kwa majina; Tumiso kifungua mimba chao na mwenye miaka 13 na kitinda mimba- Kio mwenye miaka 6.

Hivi majuzi, wamesherehekea miaka 14 kwenye ndoa. Kwa kweli mapenzi yao ni ya kuigwa na kuonewa wivu, huku tuki watakia kila la heri katika ndoa yao.

 

Lulu Hassan na Rashid Abdalla

Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Lulu Hassan na bibi yake Rashid Abdalla. Picha shukrani kwa Standard Media

Wawili hawa wanatupatia azimio za ndoa kila siku wanapo soma habari za saa moja kwenye runinga ya Citizen kila siku. Kutoka kwa mapenzi ya dhati hadi kwa tabasamu zao na hadithi yao ya mapenzi. Kwa kweli, kila mmoja angependa ndoa kama hii. Wiki mbili baada ya kujuana, Rashid alimchumbia Lulu Hassan, wao si wana ndoa tu, ila ni marafiki wa chanda na pete. Walifanya harusi mwaka wa 2013 na wame barikiwa na watoto watatu. Wavulana wawili na msichana mmoja. Hivi wamesherehekea miaka 10 tangu wajuane.

 

Njugush na Celestine

Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Njugush na Celestine/ Wakavinye. Picha shukrani kwa Pulselive

Safari ya mapenzi ya Celestine Ndinda na Njugush anayejulikana kwa ucheshi wake ilianza walipokuwa wangali wanafunzi wa chuo kikuu. Walianza kusaidiana kimaisha na kutoka wakati huo, hawaja kubali kuangalia nyuma. Wanaendelea kushikana mikono na kutiana nguvu katika maisha haya huku wakitimiza ndoto zao kwa pamoja. Licha ya Njugush kujulikana kwa ucheshi wake, yeye ni mwanafamilia na anampenda bibi yake kwa dhati. Wana mtoto mmoja wa kiume. Safari yao ya mapenzi inawatia wengi nguvu, kuwa iwapo unatatizika leo, kesho yako ni tofauti na pia kuwa mapenzi ya kweli yako.

 

Waihiga Mwaura na Joyce Omondi

Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Waihiga Mwaura na Joyce Omondi Waihiga. Picha shukrani kwa Pulselive

Joyce Omondi na bwana yake Waihiga Mwaura walipatana katika shughuli zao za hapa kule za kikazi. Waihiga alipomwona Joyce kwenye kipindi cha “Rauka” kwenye runinga ya Citizen, alijuwa bila shaka kuwa huyu ndiye angependa kuishi nayeye milele. Ila, kwa Joyce, hilo halikuwa swali kwani mapenzi yalikuwa kitu cha mwisho akilini mwake. Licha ya Waihiga kufanya juhudi za kupata angalau wasaa wa kuongea na binti huyu aliyeiteka roho yake, Joyce aliendelea kumpatia kisogo. Hadi walipo patina kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Joyce. Na kama wahenga wasemavyo, mengine ni historia, walibarikiwa na kufunga ndoa. Ndoa yao ni ya kuigwa kwani hawana visa na wanapenda kwa dhati.

 

Vivianne na Sam West

Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!

Sam West na Vivianne. Picha shukrani kwa Ghettoradio

Mwimbaji mashuhuri Vivianne na mchumba wake Sam West pia ni miongoni mwa wanandoa wanao pendwa na jamii ya Kenya. Mapenzi yao yatakutamanisha kufunga ndoa mbio iwezekanavyo uweze kuufurahikia muungano huu pia nawe. Ila, dunia ni kama mtihani na kila mtu ana maswali yake. Kinacho furahisha zaidi kati ya hawa wawili ni jinsi wanavyo ungana mkono na kutimiza ndoto zao maishani. Kama kitu kimoja na kuhakikisha kuwa wanainuana. Kwa muda mrefu sasa, tumekuwa tuki ngoja harusi yao, baada ya kifo cha baba yao, wali ahirisha harusi yao ambayo ilikuwa ifanyike mwisho wa mwaka uliopita. Tunazidi kuwaombea huku tuki ngoja siku hii kuu.

Je, ni ndoa gani nchini unayo ienzi sana? Tujulishe kwa kutuwachie ujumbe mfupi!

Vyanzo: Kenyanbuzz,youthvillage

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Baadhi Ya Wanandoa Nchini Kenya Watakao Kutamanisha Kufunga Ndoa!
Gawa:
  • Uraibu Wa Kutoka Nje ya Ndoa Nchini Kenya

    Uraibu Wa Kutoka Nje ya Ndoa Nchini Kenya

  • Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

    Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

  • Je, Sheria Inasema Nini Kuhusu Ndoa Nchini Nigeria?

    Je, Sheria Inasema Nini Kuhusu Ndoa Nchini Nigeria?

  • Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

    Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

  • Uraibu Wa Kutoka Nje ya Ndoa Nchini Kenya

    Uraibu Wa Kutoka Nje ya Ndoa Nchini Kenya

  • Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

    Aina Tofauti Ya Ndoa Zinazo Kubalika Nchini Kenya

  • Je, Sheria Inasema Nini Kuhusu Ndoa Nchini Nigeria?

    Je, Sheria Inasema Nini Kuhusu Ndoa Nchini Nigeria?

  • Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

    Watu 7 Mashuhuri Walio Zifufua Ndoa Zao Baada Ya Visa Vya Kutoka Nje Ya Ndoa

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it