Mwigizaji Nyota Maarufu Chadwick Boseman Aaga Dunia

Mwigizaji Nyota Maarufu Chadwick Boseman Aaga Dunia

Taanzia yatanda baada ya dunia kuamkia habari za kuhuzunisha za kifo cha Chadwick Boseman,

Dunia iliamkia habari za kuhuzunisha kuwa Chadwick Boseman mwigizaji mkuu wa filamu ya Black Panther maarufu kama 'Wakanda Forever' siku ya 29/08/2020. Alitangazwa kufariki kutokana na saratani ya tumbo ambayo imekuwa ikitatiza afya yake kwa miaka minne sasa.

chadwick boseman

Ni jambo lililo wahuzunisha wengi baada ya kusikia habari kuwa amekuwa akiugua saratani kwa miaka minne, jambo ambalo hakuwahi tangaza hadharani. Alinyamaza kimya na kuendelea kuigiza katika filamu. Katika kipindi hicho, ame igiza katika filamu nne zilizo tamba na zingine hata kuzawadiwa katika Oscars.

Filamu aliyo kuwa mwigizaji mkuu ya Black Panther iliwapa waafrika fahari kwa tamaduni zao kutambulika duniani kote. Aliigiza filamu hii kando na Lupita Nyong'o ambaye ni Mkenya anaye ishi Marekani na Michael B. Jordan na wengineo. Wote ambao walifanya kazi ya kupendeza na hata filamu hiyo kuteuliwa katika filamu zilizo kuwa na picha bora zaidi katika zawadi za Oscars.

chadwick boseman

Filamu zingine alizo igiza bado akipambana na saratani ni Marshall, Da 5 Bloods, August Wilson's Ma Rainey's Black Bottom na zinginezo.

Ila nyota yake haikuanza hapo, katika mwaka wa 2013, aliigiza katika filamu ya '42' iliyo kuwa na mada kuhusu maisha ya mchezaji wa baseball Jackie Robinson. Katika mwaka wa 2014, aliigiza katika 'Get on Up' kuhusu maisha ya James Brown ambaye ni mwimbaji.

Kifo cha Chadwick Boseman kilitokeo nyumbani mwake huko Los Angeles alipokuwa na bibi yake na wanafamilia wengine. Amefariki akiwa na miaka 43.

Watu maarufu walituma rambi rambi zao kwa familia yake na kumshukuru kwa kung'ara kwenye tasnia ya filamu na kushirikisha dunia katika kipaji chake cha uigizaji. Wapenda filamu zake pia walituma risala zao kwa familia yake.

Bila shaka dunia imepoteza nyota katika tasnia ya uigizaji. Kamwe hata saulika kwa kazi njema aloifanya na kuishiriki dunia katika kipaji chake na kutupatia mojawapo ya filamu bora zaidi nchini. Mungu amlaze mahali pema peponi.

Soma pia: Black Panther 2 Trailer : Plot, Cast, Release Date

Written by

Risper Nyakio