Lishe bora kwa mama ni muhimu sana wakati wa ujauzito. Humpa mama virutubishi muhimu kwa ajili ya maendeleo yake ya kiafya na yale ya mtoto aliye tumboni. Vyakula vyenye madini katika mimba huimarisha afya ya mama. Chakula bora katika mimba husaidia mtoto kukua vizuri kimwili na kiakili.
Chakula Bora Katika Mimba

Kipindi cha ujauzito ni chenye mabadiliko mengi sana kwa mama. Hii ni kwa sababu ya ongezeko la homoni mwilini. Mabadiliko haya hutofautiana kati ya mwanamke mmoja hadi mwingine na pia kutoka kwa kipindi kimoja cha ujauzito hadi kingine. Awamu ya kwanza ya ujauzito huwa na kichefuchefu sana. Ni vigumu kuzuia haya mabadiliko katika mama kwani mwili unajiandaa kupokea mtoto.
Vyakula bora katika mimba ni kama vile:
- Jamii kunde. Mbegu za makundekunde ni sehemu muhimu ya chakula cha mama mjamzito. kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. Kwa watu wasiotumia nyama, mbegu za Jamii ya kunde hutosheleza mahitaji yote ya protini
- Mayai husaidia kumpa mama protini mwilini. Vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi na magonjwa mbalimbali
- Maziwa na vyakula jamii ya maziwa. Maziwa huwa muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubishi vingi. Husaidia katika ukuaji wa mifupa na misuli
- Nafaka na vyakula vya wanga. Hivi huupa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto Hivi ni kama mahindi, mtama na mihogo
- Mboga za majani. Hizi mboga ni kama vile spinach,kabeji, mchicha. Zinafaa kuwa zenye rangi ya kijani iliyokolea. Hizi humpa mama vitamini A na B

- Mafuta ya samaki. Haya husaidia katika ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto
- Chipsi na viazi. Chumvi ilioko kwenye viazi husaidia kukausha mate ambayo huwafanya baadhi ya wajawazito kuhisi kutapika mara kwa mara. Wanga katika viazi husaidia kurekebisha kiwango cha sukari katika damu
- Limau na ndimu. Limau na ndimu huwa na uchachu ambao husaidia kukata hali ya kichefuchefu. Kunusha limau halikadhalika husaidia kupunguza hali ya kutapika. Pia unaweza kukamulia limau kwenye maji unao kunywa ama kwenye chai. Pia kunusa magada au majani ya limau husaidia kupunguza hali ya kichefuchefu
- Vyakula vyenye protini na vitamini B6. Vyakula vyenye protini kwa wingi na vitamini B6 husaidia mama kupunguza hali ya kichefuchefu. Hushauriwa kuwa mama mjamzito aepuke vyakula vyenye viungo na mafuta mingi. Hivi vyakula huzidisha hali ya kichefuchefu na hali ya kuhisi kutapika
- Tangawazi pia ni muhimu sana kwa kusaidia katika kupunguza kichefuchefu. Hii unaweza kuongeza kwenye chai
- Kunywa maji mengi. Kunywa maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji. Ni vizuri kunywa maji kwa wingi pamoja na juisi za matunda zisizo na sukari ya kuongezewa au kemikali za viwandani.
Ukosefu wa lishe bora husababisha matatizo kama vile:
- Mama kutoongeza uzito inavyotakikana
- Upungufu wa damu wakati wa ujauzito
- Kuharibika kwa mimba
- Kuzaa mtoto wenye uzito pungufu
- Mfumo wa kinga kuwa dhaifu
Vyakula huwa na nafasi kubwa sana katika ujauzito haswa kwa sababu ya mtoto anayekua tumboni. Kuzingatia chakula bora katika mimba inakuwa jambo la busara.
Soma Pia: Usiyafanye Haya Baada Ya Kupoteza Mimba: Afya Yako Baada Ya Kupoteza Mimba