Chakula Cha Mama Mjamzito: Je, Mjamzito Anapaswa Kula Nini?

Chakula Cha Mama Mjamzito: Je, Mjamzito Anapaswa Kula Nini?

Iodine ni muhimu sana unapokuwa na mimba. Una stahili kuchukua 220 mg za iodine kwa siku unapokuwa na mimba. Chakula chenye afya ni muhimu sana katika mimba.

Lishe na siha nzuri ni muhimu sana katika ujauzito ili kuhimiza ukuaji na maendeleo ya kiinitete kinacho kua tumboni mwako. Unastahili kuhakikisha kuwa unapata angalau kalori 300 zaidi mwilini mwako kila siku zaidi ya ulivyo pata hapo mbeleni kabla ya kupata mimba.

Hata kama kutapika na kichefu chefu katika miezi ya kwanza ya ujauzito inaweza fanya jambo hili kuwa gumu. Jaribu kula lishe iliyo sawasishwa na yenye afya na unywe vitamini za utunzaji kabla ya kujifungua. Vidokezo vifuatavyo vitakusaidia kukuweka wewe na mwanao mkiwa na nguvu, siha na afya nzuri.

Chakula Cha Mama Mjamzito

chakula cha mama mjamzito

Unapokuwa na mimba, hakikisha kuwa una jikakamua kutimiza mambo haya katika lishe yako:

  • Kula vyakula tofauti ili kupata virutubisho vyote vinavyo hitajika. Ongeza nafaka na mkate kwenye lishe yako, matunda, mboga nyingi, bidhaa za maziwa na protini. Vyanzo vya protini ni kama vile nyama, ndege wa nyumbani, mayai na njugu. Punguza ulaji mwingi wa ufuta na switi.
  • Chagua vyakula vilivyo na fibre nyingi. Hivi ni kama vile mkate wa nafaka nzima, maharagwe, wali, matunda na mboga kwa wingi. Una himizwa kupata fiber yako kutoka kwa chakula, lakini, unaweza kunywa tembe zitakazo kusaidia kupata kiwango tosha cha fiber mwilini. Daktari uliye naye katika kipindi hiki atakusaidia kujua tembe bora za fiber za kuchukua. Hakikisha kuwa unapata viowevu tosha.

chakula cha mama mjamzito

  • Ukiwa na mimba, vitamini na madini ni muhimu sana. Hakikisha kuwa unapata viwango tosha kwa kuongeza viwango unavyo kula katika chakula chako. Chukua tembe za vitamini za utunzaji kabla ya kujifungua kuhakikisha kuwa unapata vitamini na madini tosha kila siku. Daktari wako ata shauri tembe zitakazo kufaa zaidi.
  • Ongeza vyakula vyenye iron kama vile nyama laini, mchicha, maharagwe ya aina zote na vyakula vya kiamsha kinywa kama vile oats. Unastahili kuchukua 27 mg za iron kwa siku.
  • Kunywa bidhaa za maziwa angalau mara nne, pamoja na vyakula vilivyo na kalisi nyingi kila siku kukusaidia kupata 1000-1300 mg za kalisi kwenye chakula chako cha mama mjamzito.
  • Iodine ni muhimu sana unapokuwa na mimba. Una stahili kuchukua 220 mg za iodine kwa siku unapokuwa na mimba. Ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa akili ya mfumo wa neva wa mtoto unakua inavyo paswa. Vyanzo vyake ni maziwa ya bururu, maziwa, cheese, viazi vilivyo okwa, vyakula vya baharini kama vile salmon na shrimps.
  • Chagua angalau chanzo kimoja cha vitamini C kila siku, kama vile machungwa, papai, pilipili za kijani, cauliflower, nyanya na zinginezo. Mjamzito ana stahili kupata gramu 80-85 za vitamini C kila siku.
  • Chagua angalau chanzo kimoja kizuri cha folate kama vile mboga za kijani, legumes kama vile maharagwe nyeusi ama chickpeas. Folate ina saidia kuepusha mtoto kupata matatizo ya neural tube kama spina bifida.
  • Chagua angalau chanzo kimoja cha vitamini A kila siku. Vyanzo vya vitamini A ni kama vile karoti, viazi vitamu, mchicha na malenge.

Vyanzo: healthline,Tuko

Soma PiaTrimesta Ya Kwanza Ya Mimba: Matunda Usiyo Kubaliwa Kula Katika Ujauzito

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio