Njia 9 Za Kutayarisha Chakula Cha Mtoto Cha Nyumbani

Njia 9 Za Kutayarisha Chakula Cha Mtoto Cha Nyumbani

Chakula hiki cha mtoto ni rahisi, chenye afya na virutubisho kwa mtoto wako. Kwa kutumia hizi, unahakikisha kuwa mtoto wako anapata lishe yenye afya wakati wote.

Chakula cha nyumbani cha mtoto kina faida, mojawapo ni kuwa kina bei ya chini na unaweza tengeneza chakula cha siku nyingi. Pia, kutengeneza chakula cha mtoto nyumbani kina kukubalisha kuchagua viungo vilivyo na afya.

Chakula cha mtoto cha nyumbani: Vyakula kutoka sehemu tofauti za bara la Afrika

Wakati huu tuna zunguka katika bara la Afrika kukuletea vyakula vinavyo tengenezewa nyumbani ambavyo ni vitamu na vyenye afya kwa mtoto wako.

 Chakula cha Mtoto Cha Nyumbani: Afrika ya Kusini

Aubergine delish

aubergine delish puree eggplant

Picha: Pinterest

Aubergine ina vitamini K na fibre zinazo saidia kuchunga mwendo wa tumbo wa mtoto wako.

       Viungo

 • 1 nyanya, iliyo tolewa ngozi, na kutolewa mbegu na kukatwa vipande
 • ⅓ aubergine, iliyo tolewa ngozi na kukatwa
 • 1 kijiko cha raisins
 • 2 kijiko cha wali
 • Finyo ya cinnamon (sio lazima)

       Maagizo

 • Weka aubergine na nyanya kwenye sufuria na maji kiwango kidogo yachemke
 • Ongeza raisins, ila sio kiwango kikubwa kwani zina nguzu nyingi ya ladha. Pika kwa angalau dakika 15 kisha uongeze cinnamon ipate ladha.
 • Mwaga maji na utenge mengine ya kufanya chakula kiwe chembamba ipasavyo.
 • Ongeza mchele na purée na viungo vyote vimewekwa na umemaliza. Pakua kiwango kidogo kisha uweke chakula kinacho baki kwenye friji.

Vegetable medley

 

Mboga zina umaarufu wa umuhimu wa kiafya. Vitamini, madini na antioxidants zinazo kuwa kwenye mboga hizi zinasaidia mtoto wako kukabiliana na magonjwa.

       Viungo

 • 2 viazi (vilivyo tolewa ngozi na kukatwa)
 • 1 courgette (iliyo oshwa na kukatwa)
 • 1 aubergine (Iliyo oshwa na kukatwa)
 • 5oz uyoga (ulio oshwa na kukatwa)
 • 1 kitunguu (kilicho tolewa ngozi na kukatwa)
 • Vipande vya kitunguu saumu
 • Vipande vya rosemary
 • Poda ya pilipili
 • Mafuta machache ya olive

       Maagizo

 • Pasha oven yako joto hadi 200°C kisha upake mafuta ya olive.
 • Weka viazi na mboga kwenye sahani. Ila ikiwa ni za watu wakubwa, unaweza ongeza idadi ya kitunguu saumu na rosemary kati kati. Lakini kwani chakula hiki ni cha mtoto mwaga kiwango kidogo cha mafuta ya olive.
 • Pika katikati ya oven kwa dakika 45, funika na foil ya aluminium kwa dakika za kwanza 30.
 • Kwa watoto, ongeza finyo la chumvi lakini usiongeze pilipili. Puree ama uchanganye kiwango cha mtoto.

Cod na broccoli

cod with broccoli

Broccoli ina idadi kubwa ya protini, kalisi na Vitamini C, zote ambazo zina saidia katika ukuaji wa mtoto wako.

       Viungo

 • 1 kiazi kidogo (kilicho tolewa ngozi na kika katwa)
 • 3oz broccoli, zilizo oshwa, kutolewa ngozi na kukatwa vyema
 • 1oz cod

Maagizo

 • Chemsha viazi vyako na broccoli, kisha ongeza cod na uwache iive kwa mvuke kwa angalau dakika 15.
 • Purée na uongeze baadhi ya maziwa ya mtoto wako hadi yawe vile unavyo taka.

Chakula cha Mtoto Cha Nyumbani: Afrika Mashariki

Uji wa Baobab na Unga wa Mahindi

Homemade baby food

Picha: Kiassa Kitchen

Baobab ni chanzo kikubwa cha kalisi na magnesium na inasaidia kuipa mifupa ya mtoto wako nguvu.

Viungo

 • 1 kijiko cha poda ya baobab
 • 2 vijiko vya asali
 • ½ kikombe cha unga wa mahindi
 • 1 kikombe cha maji

      Maagizo

 • Chemsha maji na kisha umwage unga wa mahindi na ukoroge kuhakikisha hakuna madonge makubwa.
 • Changanya baoba na maji kidogo yaliyo baridi na umwage kwenye unga wa mahindi na uchanganye vyema. Huku kutasaidia kuepuka madonge kwenye uji wako.
 • Changanya mara kwa mara uji wako unapo zidi kuchemka kuepuka vidonge ama uji kushika kwenye sufuria.
 • Zima moto na uwache chungu kiive kwa mvuke, kabla ya kumwaga uji wako kwenye bakuli ya mtoto. Pakua ingali moto.

Uji wa Shayiri

Kiwango kikubwa cha fibre kilichoko kwenye shayiri kinasaidia katika mwendo wa tumbo wa mtoto wako iwe rahisi iwezekanavyo.

       Viungo

 • 1 kikombe cha maziwa ya mama
 • 1 kikombe cha maji
 • Poda ya shayiri

       Maagizo

 • Osha shayiri na uikaushe. Baadaye, zikaange hadi ziwe rangi ya hudhurungi na uepuke kuzichoma. Kisha usiage kikombe kimoja cha shayiri.
 • Chemsha maji na uongeze shayiri iliyo siagwa kwenye maji yanayo chemka na uchanganye. Chemsha hadi zichanganyike.
 • Punguza moto hadi uwe mdogo kisha uchanganye kwa dakika 20. Kisha uzime moto na uache chungu chako papo hapo.
 • Mfanya mchanganyiko huo uwe mwembamba kwa kuongeza kikombe 1 cha maziwa ya mama. Ongeza maziwa kwa utaratibu huku ukikoroga hadi yawe na ulaini unao tamani.
 • Mwaga kwenye bakuli ya mtoto na upakue ingali moto.

homemade baby food

Supu ya malenge na karoti

Malenge na karoti zina wingi wa Vitamini A na carotenoids, zinazo saidia kuongeza uwezo wa mtoto wako wa kuona.

       Viungo

 • 1 kikombe cha maji
 • 1 kitunguu
 • 500g za chembe za malenge
 • Kikombe kimoja cha olive oil
 • 1 karoti
 • Stockcube

       Maagizo

 • Chemsha kikombe kimoja cha maji na uongeze gramu 500 za malenge. Chemsha hadi iive.
 • Pasha kaango ama sufuria yako joto na kijiko kimoja cha mafuta. Weka kitunguu na kisha karoti kwenye sufuria yako hadi ziwe laini.
 • Changanya lita moja ya maji moto na chembe za kuku na uchanganye vyema. Baadaye mwaga kuku wako kwenye sufuria na uchemshe kwa dakika 5.
 • Ongeza malenge kwenye mchanganyiko wa karoti na uwache zipike kwa dakika 5. Kisha uongeze 100 ml za krimu safi na uchanganye.
 • Mwaga kwenye chombo cha kusiaga na usiage hadi ziwe laini. Pakua kwenye bakuli ya mtoto.

Afrika Magharibi

Uji wa Ndizi Mbichi

Ndizi zina kiwango kikubwa cha vitamini kama vile Vitamini B6, Vitamini C na Vitamini B2. Pia, antacid ya asili iliyoko kwenye ndizi inamlinda mwanao kutokana na vidonda vya ulcer.

 • Ndizi mbichi (tumia grater ama chombo cha kusiaga)
 • Samaki wa Cray (Crayfish)
 • Kitunguu
 • Chembe za ladha
 • Chumvi
 • Majani ya Hot leaf ama mint leaves (ama mboga zozote za matawi ya kijani)
 • Mafuta ya mitende

Maagizo

 • Chota ndizi mbichi zilizo wavwa na ufunge na majani ya uziza, kisha utumbukize kwenye chungu na uweke kando.
 • Kaanga kitunguu kwenye chungu tofauti kisha umwage kwenye chungu kilicho na ndizi mbichi. Kuongeza maji yaliyo chemka kunasaidia mandizi yaliyo fungwa kuwa ngumu kidogo.
 • Ongeza viungo kisha uwache zichemke.

Maziwa Ya Nazi Ya Moi Moi Na Vipande Vya Tuna

coconut milk moi moi

Picha: Blogarama

Kiungo kikuu cha lishe hii ni maharagwe na yana umuhimu mwingi wa kiafya. Maharagwe yana idadi kubwa ya wanga, protini, kalisi, vitamini B na fiber zinazo saidia kurutubisha mwanao.

      Viungo

 • 3 vikombe vya maharagwe
 • 2 vijiko vya mafuta  (sio lazima)
 • 3 vitunguu vya wastani
 • 5 tatashe kubwa ( red bell peppers)
 • 2 bouillon cubes
 • 2 cans tuna chunks. (ama nyama ya ng’ombe iliyo corned)
 • ½ karatasi ya maziwa ya nazi. (Unaweza tumia zaidi ama idadi ndogo kulingana na jinsi unavyo taka moi moi yako iwe laini)
 • Majani mapana. Pia, unaweza pika kwa kutumia foil ama begi ya cellophane ama uoke kwenye oven na vikombe vya muffins.

       Maagizo

 • Wacha maharagwe kwenye maji kwa dakika 5 kisha uweke kwenye chombo cha kuchakata chakula. Hadi pale ngozi yote itakapo toka
 • Suuza ngozi itoke kwenye maharagwe kisha usiage na tatashe na vitunguu vilivyo katwa.
 • Baada ya hapo, ongeza chembe za ladha, maziwa ya nazi na ukoroge vyema huku ukiongeza tuna. Koroga kwa muda kisha uangalie iwapo chumvi imetosha kabla ya kufunga kwa majani yaliyo oshwa.
 • Hatimaye, wakati ambapo moi yako imefungwa vyema na kuwekwa kwenye chungu, ongeza kiwango kidogo cha maji yanayo chakata kabla ya kuwasha moto. Moi inapikwa kwa kutumia mvuke, kwa hivyo usiongeze maji mengi. Maji mengi kwa mara moja yataingia kwenye maharagwe yako yaliyo fungwa na kuharibu upishi wako.
 • Wacha chungu chako kitokote kwa dakika 45 kabla ya kuzima moto.

Smoothie ya Wali na Njugu

strawberry kunun gyada

Picha: JamilaoLawal

Njugu na maziwa tambarare ya bururu zina kiwango kikubwa cha protini, ndizi na strawberry ni vyanzo vikuu vya vitamini na madini.

       Viungo

 • Nafak: Mchele, mtama, oat
 • Matunda: Matunda mbichi na mbivu (kama vile mandizi na papai) ama yaliyo pikwa na laini (kama vile maembe na tufaha)
 • Mboga: Laini na zilizo pikwa (mahargwe ya kijani, karoti, viazi vitamu)
 • Maziwa ya bururu
 • Nyama laini (kuku, nyama ya utuki/turkey, samaki)

       Maagizo

 • Mwaga maziwa ya bururu yaliyo tambarare, kisha ndizi na strawberries na usiage hadi ziwe laini.
 • Kwa kutumia chombo cha kusiaga maarufu kama blender, siaga njugu hadi poda ambayo si laini sana ionekane.
 • Chemsha maji, weka kwenye chungu, ongeza unga wa wali hadi uchemke. Pika kwa dakika 10 huku ukichanganya hadi uwe laini. Ongeza maji kidogo hadi iwe laini kadri upendavyo.
 • Kisha, ongeza njugu, maziwa ya bururu kwenye wali wako. Changanya hadi ziwe laini utakavyo. Pakua kingali na joto.

Kitu kikuu zaidi kuhusu chakula cha mtoto kilicho tengenezewa nyumbani ni maarifa yako kuhusu kilicho tumika. Vyakula hivi ni vya afya na vyenye virutubisho vifaavyo kwa mtoto wako, na pia ni rahisi kutengeneza.

Soma piaEnergy-Packed Local Foods For Your Kids

Makala haya yali andikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume, kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio