Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

Mtoto anapo fikisha mwaka mmoja wa umri, kuna vitu muhimu ambavyo vinabadilika kama vile lishe yake. Tazama makala yetu ya chakula cha mtoto wa mwaka mmoja!

Hongera mama! Mtoto wako amefikisha mwaka mmoja katika maisha yake. Bila shaka haijakuwa safari rahisi kwako. Kujua kuwa umetwikwa jukumu la kuchunga kiumbe chingine na. Wasaa wako wa kufanya mambo yako umepunguka na wakati mwingi unamchunga mwanao. Hongera kwa juhudi zote ulizo tia katika mwaka huo mmoja. Kutabasamu na mwanao, kumlisha, kushuhudia mhemko wa hisia mara kwa mara, tazama umbali uliofika. Kufahamu chakula cha mtoto wa mwaka mmoja unacho paswa kuwa ukimlisha ni muhimu katika kipindi hiki.

Mwanao anazidi kukua na kushuhudia mabadiliko mengi mwilini kwa kasi sana. Na kuhakikisha kuwa anapata chakula anacho hitaji ni muhimu katika kipindi hiki. Ila, usiwe na shaka kwani huenda mtoto wako akakataa kula mara kwa mara ama kukataa aina fulani ya chakula.

Mahitaji ya chakula ya mtoto wa mwaka mmoja

Mtoto anapo fikisha umri wa mwaka mmoja, anahitaji kalori 1,000, kalisi 700mg, na vitamini D 600 IU kila siku ili aweze kukua inavyo stahili. Wataalum wa afya na lishe ya watoto walishauri.

Tazama orodha yetu ya chakula cha mtoto wa mwaka mmoja

Vyakula hivi vinakusaidia kumlisha mtoto wako kwa urahisi bila kuwa jikoni wakati wote.

  1. Maziwa na maziwa ya bururu

Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

Katika umri wa mwaka mmoja, kwa upole, mtoto wako anakoma kunyonya ama kupunguza kiwango cha maziwa ya mama anacho kunywa kwa siku. Na huu ni wakati bora wa kumwanzishia maziwa. Maziwa na maziwa ya bururu ni vyanzo vyema vya protini na kalisi ambayo ni muhimu sana katika ukuaji wa meno na mifupa. Hakikisha kuwa una mpa mwanao glasi moja kila siku. Huku ukiendelea kumpa maziwa ya mama.

2. Mandizi na matunda laini

matunda salama kwa mjamzito

Kumlisha mtoto wako vyakula vyenye afya kama matunda katika wakati huu anapo zidi kukuza uwezo wake wa ladha. Kutamsaidia kula vyakula vyenye afya katika siku za usoni. Kata ndizi na matunda mengine kama maembe kwa vipande vidogo kisha umlishe mtoto wako. Epuka kumpa vipande vikubwa kwani huenda akanyongwa.

3. Mayai

chakula cha mtoto wa mwaka mmoja

Mojawapo ya chakula cha mtoto wa mwaka mmoja kinacho himizwa zaidi ni mayai. Na ni bora kwa wote, wakubwa kwa wadogo. Yana wingi wa protini na virutubisho muhimu katika afya ya macho, ukuaji wa akili.

Kuwa makini kuona kama mtoto wako anapata mzio baada ya kula mayai. Ikiwa una shaka kuwa huenda mwanao akapata mzio baada ya kula mayai, wasiliana na daktari wa lishe ya watoto akushauri zaidi.

4. Parachichi

avocado

Hili ni tunda nzuri kwa mtoto. Na linalo egemeza ukuaji wa mtoto wako. Kulingana na Shirika la Afya ya Moyo la Umarekani, asilimia 30-40 ya kalori za mtoto zinapaswa kutoka kwa ufuta. Na parachichi lina sifika kwa kiwango chake cha juu cha ufuta wenye afya unao faidi ukuaji wa ubongo na moyo wa mtoto.

5. Maji

Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

Maji ni muhimu sana kwa watu wakubwa na watoto pia. Hakikisha kuwa mtoto anakunywa angalau glasi moja ya maji kila siku.

Hitimisho

Mengi yana endelea katika maisha ya mtoto wako anapokuwa katika umri wa mwaka mmoja. Ikiwa una shaka zozote kuhusu lishe yake, wasiliana na daktari wa lishe ya watoto.

Soma Pia: Jinsi Ya Kutengeneza Ratiba Ya Lishe Nchini Kenya

Written by

Risper Nyakio