Aina Tofauti Ya Vyakula Vya Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

Aina Tofauti Ya Vyakula Vya Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

Iwapo mtoto wako mchanga amepita hatua ya miezi sita ya kula maziwa ya mama tupu, huenda ukahitajika kujua chakula cha mtoto wa miezi saba. Ni muhimu kujua kuwa mtoto anapofikisha miezi sita, wanaweza aina nyingi ya vyakula. Unacho paswa kuwa makini nacho ni ladha na ulaini wa chakula chochote unacho mlisha. Mtoto anapaswa kuweza kula chochote na kukichakata unacho mpa.

Chakula cha mtoto wa miezi saba cha kumlisha anapo maliza kunyonya:

Uji

baby food recipes 7 months

Corn pap ama uji wa mahindi ni mojawapo ya chakula maarufu zaidi cha watoto. Unapo chakata mahindi, unaweza iongeza virutubisho kwa kuchanganya na mtama. Huku kutafanya uji kuwa na ladha zaidi ikilinganishwa na uji wa mahindi tupu. Pia, hakikisha kuwa una weka mahindi kwa maji kwa muda na nafaka ili kuepuka kupata harufu mbaya. Huenda harufu ile ikawafanya watoto wakatae kuzila, pia unapo mtayarishia mtoto wako uji, hakikisha kuwa haija shikana sana.

Na chakula hiki cha mtoto wako wa miezi saba, unapaswa kuanzia kwa kumlisha mtoto wako uji wenye unyevu nyevu hadi pale watakapo zoea lishe hii. Lengo ni kuhakikisha kuwa ni laini kama maziwa ya mama, kadri iwezekanavyo.

Ili kupunguza fikira za kutengeneza uji kila mara mtoto anapo hisi njaa, unaweza kuwa ukitayarisha asubuhi na kuweka kwenye kontena inayo ifanya ibaki moto. Itahakikisha kuwa mtoto wako ana uji moto wa kunywa kila mara anapo hisi njaa.

Oatmeal

Chakula hiki kina ladha na afya na ni rahisi kutengeneza. Unapo tengeneza oatmeal, tafadhali epuka kutumia sukari. Unaweza ongeza formula ya mtoto ili kiwe na ladha zaidi.

Viazi na mihogo

chakula cha mtoto wa miezi saba

Picha shukrani kwa: Flickr

Viazi na viazi vitamu ni chakula bora cha mtoto wa miezi saba. mtoto anaweza kula viazi na viazi vitamu vilivyo chemshwa(ambazo hazijakauka sana). Wanaweza kula uji wa mihogo na viazi.

Unapomlisha mtoto uji wa viazi, changanya viazi na uhakikishe kuwa mtoto anakula sehemu ya uji inayo kuwa na unyevu nyevu. Njia nyingine bora ya kutengeneza uji wa watoto ni hii: nunua mifupa sokoni na uchanganye na chumvi. Tumia supu hiyo kutengeneza uji.

Unaweza mlisha mtoto wako supu hiyo kwa kutumia kijiko. Mtoto wako atafaidika kutokana na kalisi. Pia anaweza kula, kipande cha mhogo na kiazi ila kiwe laini aweze kumeza bila kutaabika.

Mchele

Mchele huliwa kwa sana. Unapo mlisha mtoto wa miezi saba mchele/wali, unapaswa kukibonda chakula kile kabla ya kumlisha. Ili kuhakikisha kuwa chakula kile ni laini na hakimnyongi mtoto.

Matunda

chakula cha mtoto wa miezi saba

Picha shukrani kwa: pixabay

Iwapo haujali sana mtoto wako kuchafuka anapokula, matunda ni vitamu tamu bora. Matunda yana afya ikilinganishwa na biskuti. Unaweza hakikisha kuwa mtoto wako ana kitu cha kula kwa kumpa machungwa, tikiti na tufaha(ambazo zimetolewa mbegu kwa makini) na matunda mengineyo.

Mboga

Faida za mboga haziwezi sisitizwa vya kutosha. Unapo mlisha mtoto wako wa miezi saba mboga zenye matawi mengi, hakikisha kuwa umekata kuwa sehemu ndogo kisha uchanganye na chakula chake. Jambo hili ni muhimu ili kuepuka kunyongwa na chakula kile. Karoti na mayai pia ni nzuri kwa mtoto wako, ila, huenda ukahitajika kuchemsha hizi ili kuzifanya ziwe rahisi kwa mtoto wako kumeza.

Supu

Watoto wanapenda ogbono na supu ya okra kwa sababu supu hizi zimenyooka na kuteremka kwa koo kwa urahisi. Unaweza zichanganya na fufu ama eba iwapo ungependa kumlisha mtoto wako. Kumbuka kufanya eba na fufu yako iwe nyororo kwa mtoto wako.

Chai na mkate

chakula cha mtoto wa miezi saba

Picha shukrani kwa: Flickr

Chai katika nchi kama Nigeria ni tofauti. Chai ni mchanganyiko wa chokleti na maziwa na mara nyingi hutengenezwa kwa kutumia maji vuguvugu. Unaweza tumbukiza pande za mikate kwenye chai na umlishe mtoto wako. Hakikisha kuwa haumlishi mtoto wako sukari nyingi ambayo sio njema kwa mtoto aliye na umri chini ya mwaka mmoja.

Kwa sasa kwani mtoto wako amewacha kunywa maziwa pekee na akaanza kula vyakula, utahitaji kuongeza chakula cha watu wazima kwenye maziwa ya mama. Orodha ya vyakula rahisi vitakavyo kusaidia kufanya uamuzi ufaao katika kumlisha mtoto wako wa miezi saba.

Soma pia: Garlic benefits for men: Why should you really consume it?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio