Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

Unapomwanzisha mtoto chakula cha nje, hakikisha kuna ratiba ya kufuata kila siku. Vyakula vyenye madini vinashauriwa sana.

Pindi mtoto anapozaliwa, wataalamu hushauri atumie maziwa ya mama pekee kwa miezi sita.  Haya maziwa huwa chakula tosha kwa mtoto. Hii ni kwa sababu haya maziwa yana virutubishi ambavyo ni muhimu kwa mtoto. Husaidia katika kukua na pia huwa kinga kutokana na maradhi yanayowapata watoto wangali wachanga. Pia mfumo wa usagaji chakula wa mtoto bado hauwezi kusaga chakula kigumu. Iwapo, ata baada ya kuanzisha chakula cha nje hukomi kumnyonyesha mtoto. Hili huendelea mpaka akamilishe miaka miwili unusu.  Ila mtoto anapozidi kukua huhitaji vyakula vingine ili kukidhi mahitaji yake afikiapo miezi saba. Tuna angazia mahitaji ya chakula cha mtoto wa miezi saba.

Vyakula vyenye madini ya zinki kama vile nyama, madini ya chuma kama vile spinach na mayai, madini ya calcium na vitamini D, vyakula vyenye Omega 3 kama vile samaki, vyakula vyenye vitamin A ,B, C, E huwa muhimu sana.

Dalili zinazoashiria kuwa mtoto yuko tayari kuanza chakula cha nje ni kama vile:

chakula cha mtoto wa miezi saba

 • Amekamilisha miezi sita
 • Ana uwezo wa kukaa chini
 • Unapomwelekeza chakula anakipokea kwa kupanua mdomo ama kukataa
 • Shingo yako imekaza
 • Anajaribu kumeza chakula na sio kutema nje

Chakula cha mtoto wa miezi saba:

Unapomwanzisha mtoto chakula cha nje, hakikisha kuna ratiba ya kufuata kila siku. Vyakula vyenye madini vinashauriwa sana. Hakikisha vyakula vimepondwa kabisa ikiwezekana kutumia blender. Pia mtoto anafaa kupata lishe kamili hii kumaanisha matunda, nafaka, nyama,mboga na vinginevyo.

Jinsi ya kutayarisha chakula cha mtoto wa miezi saba:

 • Matunda - mwanzo osha kwa maji vuguvugu ili kuondoa uchafu, toa ganda la nje, katakata katika vipande vidogo au pia  umpe kwa kijiko
 • Mboga – osha kwa maji ya vuguvugu, katakata vipande vidogo kisha pandika jikoni kwa muda mchache. Ikiwa tayari tua kwenye blender ama ponda mpaka ziwe laini
 • Nyama – kata kwenye vipande vidogo, chemsha kwa moto wa kiasi hadi zilainike. Saga kwenye mashine ya chakula food processor. Samaki haina haja ya kusagwa kwani ikiiva huwa imelainika ila utazingatia kuondoa mifupi.
 • Mbegu – hizi ni kama vile maharagwe, choroko. Pika hadi zilainike kisha upondeponde. Viazi na ndizi pia ni chakula cha muhimu sana kwa watoto.
 • Nafaka – ni vyema kutochanganya nafaka nyingi kwa wakati mmoja. Ni bora kuwa na unga tofauti tofauti kwa kila nafaka.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza chakula:

Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

 • Elewa kuwa kila mtoto ni tofauti kwa hivyo usijaribu kumlinganisha na mwingine
 • Jaribu kumpa vyakula tofauti, kuna uwezekano kuna kile atapenda na vingine akatae
 • Zingatia uzito wake unawiana na umri wake na unaongezeka inavyostahili
 • Ratibisha wakati wa chakula cha mtoto kuwiana na chenu ili kumpa hamu ya chakula.
 • Huu wakati si mwafaka kuchanganya chakula ili kutambua chakula gani kinampendeza ana kilicho na madhara kwake.
 • Pia ni muhimu kumpa chakula kimoja kwa siku nne mfululizo ili aweza kukizoea na pia kugundua kama kuna madhara
 • Mpe mtoto chakula anapokuwa na njaa na pia tengeneza mazingira ya furaha ili mtoto afurahie chakula chake.

Usalama wakati wa kumpa  mtoto wa miezi saba chakula;

 • Usafi wa chakula cha mtoto ni jambo la Kimsingi
 • Angalia joto la chakula cha mtoto asichomeke mdomo
 • Hakikisha huachi mtoto na chakula bila ya uangalizi wowote
 • Pia usimpe mtoto chakula kama amelala, anacheka ama analia
 • Usimpe mtoto chakula ambacho hakijalainika vizuri ili kisimkabe koo

Chanzo: Healthline

Soma Pia: Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako wa Miaka Mitano na Miezi Mitatu

Written by

Risper Nyakio