Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita

3 min read
Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi SitaRatiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita

Kulingana na Shirika la Madaktari la Umarekani, unapaswa kumnyonyesha mtoto pekee hadi pale anapo fikisha miezi 6.

Ikiwa mtoto wako wa miezi sita ako tayari kuanza kula vyakula vigumu, huenda ukawa unashangaa jinsi ya kuanza kumpatia chakula, kipi, wakati upi na jinsi ya kumlisha. Soma zaidi kuhusu chakula cha mtoto wako wa miezi sita.

Chakula cha mtoto wa miezi sita: Napaswa kumlisha mtoto wangu nini?

chakula cha mtoto wa miezi sita

Kumbuka kuwa katika umri huu, lishe yake kuu ni maziwa ya mama ama formula. Chakula kigumu ni cha kuongeza tu katika umri huu, na bado utahitajika kumlisha maziwa ya mama kwa wingi ama formula. Mara nyingi, chakula cha kwanza huwa nafaka za mtoto kama vile oatmeal ama wali. Baadhi ya watoto huenda waka kataa kula nafaka na ni sawa. Kumbuka kuwa haupaswi kuweka nafaka za mtoto kwenye chupa. Changanya na formula ama maji kisha umlishe kwa kijiko.

Epuka kuchanganya nafaka zake na maziwa yako. Hadi pale ambapo mtoto ataonekana kuwa anazipenda. Kufanya kabla, huenda mtoto akakosa kula na utakuwa umetumia vibaya maziwa ya mama. Hakikisha kuwa nafaka hizo ni majimaji na sio ngumu ili mtoto aweze kula kwa urahisi.

Vyakula vya kuto mlisha mtoto

Asali mbichi

Huenda mtoto akapata botulism. Ngoja hadi pale anapo fikisha miezi 12 kisha umlishe asali ya watoto.

Maziwa ya ng'ombe

Watoto hawapaswi kuwa wanakunywa maziwa ya ng'ombe wakiwa miezi sita. Lakini wanapo anza kula vyakula vigumu bila tatizo, wanaweza kunywa maziwa ya bururu ama cheese laini. Wanapo shindwa kuichakata vyema, huenda waka anza kutoa damu kwenye kinya chao.

Aina za samaki

Epuka kumlisha mtoto wako aina za samaki zilizo na viwango vingi vya mercury zaidi ya mara moja kwa mwezi. Ni sawa kumlisha salmon. Hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wake kujua aina ya samaki zilizo salama kwake.

Wakati wa kumlisha mtoto

chakula cha mtoto wa miezi sita

Kulingana na Shirika la Madaktari la Umarekani, unapaswa kumnyonyesha mtoto pekee hadi pale anapo fikisha miezi 6. Kumwanzishia mtoto chakula kigumu kabla ya wakati huo, huenda kukamfanya ale chakula kidogo na kufanya maziwa yako ya mama kuisha mapema. Kuanza mapema pia huenda kuka sababisha lishe iliyo na protini, ufuta na virutubisho vingine visivyo tosha. Hakikisha kuwa hautamwanzishia chakula kigumu baada ya miezi sita. Kwani kungoja sana huenda kukasababisha matatizo ya kula.

Kwa wakati huu, huenda mtoto wako akawa ana nyonya mara 6-8 kwa siku. Na lengo anapo fikisha mwaka mmoja ni kuwa akila angalau mara sita kwa siku:

  • Kiamsha kinywa
  • Asubuhi (saa 11)
  • Saa saba
  • Alfajiri
  • Chajio
  • Kabla ya kulala

Ikiwa una mwanzishia chakula kigumu, ni vyema kumlisha asubuhi ili uone ikiwa kitaibua matatizo yoyote mwilini. Epuka kumlisha akiwa na njaa sana ama anapo lia.

Jinsi ya kumlisha mtoto

Unapo mlisha mtoto chakula kigumu, hakikisha kuwa ameketi wima kwenye kiti na kikafungwa. Usimlazimishe mtoto wako kula. Weka chakula kwenye kijiko kisha uwekelee kwenye mdomo wake, huenda akafungua mdomo ama kuhitaji kupapaswa kidogo ili akubali.

Hakikisha kuwa mtoto wako anakula pamoja na wanafamilia wengine kwani jambo hili lime dhihirishwa kuwa na athari chanya katika ukuaji na utangamano wa familia.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Ukuaji Wa Mtoto Wako Wa Miezi Mitano

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Baby
  • /
  • Ratiba Ya Chakula Cha Mtoto Wa Miezi Sita
Share:
  • Aina Tofauti Ya Vyakula Vya Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

    Aina Tofauti Ya Vyakula Vya Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

  • Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

    Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

  • Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

    Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

  • Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

    Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

  • Aina Tofauti Ya Vyakula Vya Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

    Aina Tofauti Ya Vyakula Vya Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

  • Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

    Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

  • Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

    Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

  • Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

    Chakula Bora Cha Kumlisha Mtoto Wa Miezi Saba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it