Jinsi Ya Kutengeneza Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja

Jinsi Ya Kutengeneza Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja

Ni vyema kumwanzishia mtoto wako chakula chenye afya angali mchanga.

Kutengeneza chakula chenye ladha cha mtoto wako wa mwaka mmoja kuna kukubalisha kuwa makini na lishe yake. Lishe ya mtoto huenda ika athiri ukuaji na maendeleo yake, kwa hivyo, unapaswa kutengeneza ratiba ambayo itahakikisha kuwa mtoto wako anapata virutubisho vyote vifaavyo.

Hii si kusema kuwa mtoto wako atakula kila kitu unacho mtia mdomoni. Lazima uwe mtulivu na uendelee kumlisha hata akikumwagilia chakula ulicho mtayarishia kwa mapenzi. Usikubali kuvunjwa moyo! Mwishowe, mtoto wako atazoea.

1 year old meal plan

Kumwanzishi mtoto chakula: Chakula cha mtoto wa mwaka mmoja

Wakati wa kumwanzishia mtoto chakula kigumu

Katika nchi nyingi, wamama wanashauriwa kuwa nyonyesha watoto wako pekee kwa muda wa miezi sita. Unaweza mwanzishia vyakula vigumu kwa lishe yake baada ya miezi sita. Ni sawa kumpa mtoto formula iwapo kufuatia sababu yoyote ile umeshindwa kumnyonyesha. Chakula kigumu kwa kawaida kinapaswa kuandamana na maziwa ya mama na formula kwa watoto wa umri chini ya mwaka mmoja na wazee kuliko miezi sita.

Jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula kigumu

Unapo mwanzishia mtoto chakula kigumu - hiki ni chakula chochote ambacho sio formula ama maziwa ya mama- unapaswa kuanza na chakula laini kabisa. Unaweza bonda chakula ambacho sio laini kabisa kabla ya kumlisha mtoto. Iwapo hutaki kukibonda, pika hadi kiwe laini. Unahitaji kufanya hivi kwa sababu mtoto ratiba ya lishe ya mtoto wako itakuwa na vyakula vingi vigumu!

1 year old meal plan

Ukiwa tayari kumwanzishia chakula kigumu, unapaswa kuanza na chakula ambacho mtoto anaweza meza bila kutafuna. Watoto wenye umri wa miezi 6-12 hawana nguvu za meno, na hiyo ndiyo sababu kwa nini unawapatia chakula ambacho wanaweza meza bila kutafuna ama kubonda kabla ya kuwalisha. Kwa bahati nzuri, unaweza bonda wali, maharagwe na viazi na kadhalika.

Mbadala wa maziwa ya mama na formula baada ya miezi sita ni uji. Custard pia ni nzuri kwa watoto inapofika wakati wa kuwaanzishia chakula kigumu. Unapomwanzishia mtoto wako uji, hakikisha kuwa haijashikana ama iwe nyembamba. Ili mtoto aweze kuinyonya kutoka kwa chupa. Unaweza ifanya iwe nene vya kutosha kumlisha mtoto kwa kutumia kijiko punde anapo anza kuzoea kula vyakula vigumu.

nigerian food for 1 year old

Vyakula vigumu vilivyo maarufu kwa watoto wa mwaka mmoja

Ni vigumu kumtayarishia mtoto wako wa mwaka moja ratiba ya lishe bila kujua hiari za vyakula vigumu nchini unako ishi. Kwa sababu kuna tamaduni nyingi na vyakula vigumu vingi ambavyo watoto wako wanaweza kula! Unacho hitajika kufanya ni kujua jinsi tamaduni zingine zinavyo tayarisha vyakula vyao vya watoto.

Orodha ya baadhi ya vyakula vigumu vilivyo maarufu zaidi vya watoto:

 • Uji
 • Custard
 • Nafaka
 • Viazi
 • Mhogo
 • Maharagwe
 • Wali
 • Soya beans
 • Kunde
 • Moi moi
 • Okpa
 • Soft swallow
 • Supu
 • Ndizi mbivu
 • Noodles
 • Pasta
 • Fruit salad
 • Oatmeal
 • Mkate
 • Ndizi mbichi za kupika
 • Mayai, ya kukaanga ama kuchemsha
 • Akara

chakula cha mtoto wa mwaka mmoja

Lishe ya mtoto wa mwaka mmoja inaweza husisha vyakula tulivyo taja hapo juu vyote ila mtoto aliye na miezi chini ya 12 hapaswi kula vitu vyote vilivyo kwenye orodha hiyo, hasa vyakula vilivyo vigumu kutafuna.

Fanya kadri uwezavyo kupunguza vyakula vilivyo chakatwa vya mtoto wako. Unaweza mfunza kula vyakula freshi, ambavyo havija chakatwa. Mwanzishie matunda yanayo wafaa watoto kwenye lishe yake. Mlishe mtoto wako wa mwaka mmoja sharubati za kujitengenezea na ufunze ulimi wake kula vyakula vya afya.

Jinsi ya kutengeneza chakula cha mtoto wa mwaka mmoja chenye afya

Lishe ya mtoto wa mwaka mmoja inapaswa kuwa imesawasishwa na kujazwa na vyakula vitamu kwa sababu hutaki kumfanya mtoto wako aboeke. Kuwa mbunifu na chaguo lako! Hakikisha kuwa ratiba yako ya lishe ina virutubisho vyote, protini, wanga, ufuta, madini, vitamini na maji.

Vyakula vya kiamsha kinywa, chamcha na chajio vya mtoto wa mwaka mmoja
Kiamsha kinywa, mojawapo ya vyakula hivi vitafaa:

Chai ya chokleti na mkate Uji

Nafaka

oatmeal

supu kwa mkate

mayai ya kukaanga

okpa

noodles.

Unaweza bonda sehemu nyeupe ya mayai ya kuchemsha na uchanganye kwa pap uliyo mtengenezea, ongeza maziwa na kisha umlishe mtoto.

Kwa chamcha, mojawapo ya hizi zitafaa:

Lishe ya mtoto wa mwaka moja ya chamcha itakuwa na vyakula vigumu.

Unaweza mlisha mtoto chochote unacho kula kama chamcha ili kisiwe na pilipili nyingi ama kigumu sana.

Pia unaweza mpa mtoto kipande cha mhogo, maharagwe, karoti, machungwa, tufaha ama matunda yoyote kati ya lishe zake.

Kwa chajio, mojawapo ya vyakula hivi vitafaa:

Hiari za kiamsha kinywa kwenye ratiba hii ya mtoto wa mwaka mmoja zinaweza faa kuwa chajio chake.

 

Unaweza changanya chamcha na chajio cha mtoto wako!

Pia kwa kiamsha kinywa, unaweza chemsha mchele na maharagwe hadi iwe laini, ongeza viungo vyako kana kwamba unapika wali wa jollof kisha upike mchele hadi uwe laini kiasi kwamba mtoto wako anaweza tafuna kwa urahisi. Wacha kipoe kabla ya kumwaga chakula kwenye kifaa cha kusiaga chakula kisha u blend. Usiongeze maji; maji kidogo yaliyo baki kwenye chakula kimetosha. Unaweza mlisha mtoto wako hicho. Vitakavyo baki, hifadhi kwenye friji umlishe siku ingine. Pia unaweza chemsha na usiage viazi vya mtoto wako. Pika viazi hadi viwe laini, kisha uongeze samaki, na chumvi kidogo. Kubali kipoe kisha usiage na umlishe mtoto wako.

Chajio hakipaswi kuwa kingi ama kizito sana unapotengeneza ratiba ya mtoto wako. Ikiwa chakula chako ni kizito sana, huenda mtoto wako aka tatizika kulala. Na iwapo chakula ni chepesi sana, mtoto wako anaweza hisi njaa na kuamka usiku kulilia chakula.

 

Kumbukumbu: British Nutrition Foundation 

Soma pia: Top 8 foods to feed your child so that they grow taller and stronger

Written by

Risper Nyakio