Jinsi Ya Kutayarisha Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wako Wa Mwaka Mmoja

Jinsi Ya Kutayarisha Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wako Wa Mwaka Mmoja

Vyakula vya afya ni bora sana kwa mtoto wako wa mwaka mmoja!

Kutengeneza chakula chenye lishe cha mtoto wa mwaka mmoja katika Nigeria kina kukubalisha kuwa makini na lishe ya mtoto wako. Lishe ya mtoto wako huenda ika athiri ukuaji na maendeleo, kwa hivyo unapaswa kuandika utaratibu wa lishe ambao utahakikisha kuwa mtoto wako anapata virutubisho vyote.

Hii haina maana kuwa mtoto wako atakula vyakula vyote unavyo mlisha. Lazima uwe mtulivu na uendelee kujaribu kumlisha hata akikutupia chakula chote ulichomtayarishia na mapenzi. Usikubali kukasirika baada ya haya yote! Hatimaye, mtoto wako atakubali.

1 year old meal plan

Kuanzisha Vyakula Vigumu: Lishe Ya Mtoto Wako Wa Mwaka Mmoja Nigeria

Wakati wa kumwanzishia mtoto wako vyakula vigumu

Katika nchi ya Nigeria, wamama wana shauriwa kuwa nyonyesha watoto wao kwa miezi sita. Unaweza anzisha vyakula vigumu kwenye lishe ya mtoto wako baada ya miezi sita. Ni sawa kumpa mtoto wako formula iwapo kwa sababu yoyote ile umeshindwa kumnyonyesha. Vyakula vigumu, vinapaswa kuandamanishwa na maziwa ya mama na formula ya watoto wachanga kuliko mwaka mmoja na zaidi ya miezi sita.

Jinsi ya kumwanzishia mtoto wako vyakula vigumu

Unapo mwanzishia mtoto wako vyakula vigumu - hivi ni vyakula vyovyote ambavyo si maziwa ya mama ama formula- unapaswa kuanza na chakula laini zaidi. Unaweza bonda chakula chochote ambacho sio laini zaidi kabla ya kumlisha mtoto wako. Iwapo hutaki kubonda, pika chakula hadi kiwe laini zaidi. Unapaswa kufanya hivi kwa sababu chakula chako cha mtoto wako wa mwaka mmoja kitakuwa na vyakula vingi sana vigumu!

1 year old meal plan

Ukiwa tayari kumwanzishia mtoto wako vyakula vigumu, unapaswa kuanza na vyakula ambavyo mtoto wako anaweza meza bila kutafuna. Watoto kutoka umri wa miezi 6-12 hawana meno yenye nguvu, na hiyo ndiyo sababu kwa nini wanameza vyakula bila kumeza ama ukibonde. Pia unaweza bonda wale wako, maharagwe na viazi.

Chakula bora zaidi mbadala wa maziwa ya mama na formula baada ya miezi 6 ni pap. Custard pia ni nzuri kwa watoto inapo fika umri wa kumwanzishia mwanao vyakula vigumu. Unapo mwanzishia mtoto wako pap, hakikisha kuwa ina maji maji na sio nene sana. Inapaswa kuwa na maji tosha ili mtoto wako anyonye kupitia kwa chupa. Unaweza fanya pap iwe nene vya kutosha ili umlishe mtoto wako kwa kutumia kijiko baada ya mtoto wako kujua kula vyakula vigumu vizuri.

chakula cha mtoto wa mwaka mmoja Nigeria

Vyakula vigumu maarufu zaidi vya mtoto wa mwaka mmoja katika Nigeria

Huwezi tengeneza chakula cha mtoto wa mwaka mmoja Nigeria bila kujua vyakula vigumu vya Nigeria. Kwa sababu Nigeria ina tamaduni nyingi, kuna aina nyingi za vyakula vigumu vya watoto. Unapaswa kujua tu jinsi tamaduni zingine zina tayarisha chakula chao cha watoto.

Vyakula vilivyo maarufu zaidi vya watoto Nigeria ni:

 • Pap
 • Custard
 • Nafaka
 • Viazi (vitamu na vya kawaida)
 • Mhogo
 • Maharagwe
 • Mchele
 • Soya beans
 • Kunde
 • Moi moi
 • Okpa
 • Soft swallow (hasa eba, semolina ama fufu)
 • Supu (hasa egusi, vegetable soup, okra na ogbono)
 • Ripe plantain (uji, kukaangwa, kuchemsha)
 • Noodles
 • Pasta
 • Fruit salad
 • Oatmeal
 • Mkate
 • Mhogo
 • Unripe plantain porridge
 • Mayai, ya kuaanga na kuchemsha
 • Akara
 • Uji wa ndizi zisizo iva
 • Ndizi zilizo iva
 • Bone broth

chakula cha mtoto wa mwaka mmoja Nigeria

Lishe ya mtoto wa mwaka mmoja huenda ikawa na vyote hivi ila mtoto wa chini ya miezi 12 hapaswi kula kila kitu kwenye orodha hii, hasa vyakula vilivyo vigumu kutafuna kama vimezeo (eba, semo na kadhalika).

Fanya juhudi zote kuepuka vyakula vilivyo chakatwa kwa mtoto wako. Unaweza mfunza mtoto wako kupenda vyakula asili na mbichi. Mwanzishie mtoto wako matunda yaliyo salama kwa mtoto kwenye lishe yake. Mlishe mtoto wako wa mwaka mmoja na sharubati za kinyumbani za kiasili na uanzishe ulimi wake kwa vyakula vya afya.

Jinsi ya kutengeneza chakula cha afya kwa mtoto wako wa mwaka mmoja Nigeria

Lishe ya kawaida ya mtoto wa mwaka mmoja inapaswa kuwa lishe bora na iliyo jazwa na aina tofauti za vyakula vyenye ladha kwa sababu hautaki kumfanya mwanao akose hamu. Kuwa mbunifu na vyakula utakavyo chagua! Hakikisha kuwa lishe yako ina virutubisho vya vyakula vyote- protini, wanga, ufuta, madini, vitamini na maji.

Sampuli ya vyakula vya kiamsha kinywa, chamcha na chajio vya mtoto wako wa mwaka mmoja
Kwa kiamsha kinywa, vyakula hivi vitasaidia:

Chokleti na mkate

pap

nafaka

oatmeal

kitoweo na mkate

mayai yaliyo kaangwa

okpa

noodles.

Unaweza changanya yolk ya mayai yako yaliyo chemshwa na uchanganye na pap, kisha uongeze maziwa na umlishe mtoto wako.

Chakula cha mchana, hivi vitasaida:

Lishe ya mtoto wa mwaka mmoja cha chamcha kwa mara nyingi kitakuwa na vyakula vigumu tu.

Unaweza mlisha mtoto kitu chochote unachokula cha chamcha ila uhakikishe hakina pilipili ama kigumu zaidi.

Pia unaweza mpatia mtoto kipande cha mhogo, mayai ya shambani, karoti, machungwa, tufaha ama matunda yoyote kati ya lishe zake.

Chajio, vyakula hivi vitasaidia:

Hiari za kiamsha kinywa cha mtoto wako wa mwaka mmoja ni bora kwa chajio pia.

Huenda pia uka changanya zote za chamcha na chajio kwa mtoto wako!

Pia kwa kiamsha kinywa, unaweza chemsha mchele na ama maharagwe hadi yawe laini, ongeza viungo kama kwamba unatayarisha Jollof; kisha upike mchele wako hadi utakapo kuwa laini kiasi cha mtoto wako kutafuna kwa urahisi. Uwache upoe kabla ya kumwaga chakula chako kwenye kifaa cha kusiaga na usiage. Usiongeze maji; kiasi kidogo cha maji kilichoko kwenye chakula kimetosha. Unaweza mlisha mtoto wako. Weka mabaki kwenye kifaa cha kuhifadhi na upakue siku nyingine. Pia unaweza chemsha na usiage viazi vya mtoto wako. Pika viazi hadi viwe laini, kisha uongeze samaki (aliye pikwa ama wa kukaushwa), chumvi na viungo vya ladha. Iwache ipoe, kisha usiage na umlishe mwanao.

Chajio hakipaswi kuwa kingi sana kwenye lishe ya mtoto wa mwaka mmoja. Iwapo chakula ni kingi sana, huenda mtoto akakosa kuwa na starehe na huenda akawa na matatizo ya kulala. Ila iwapo chakula ni kidogo sana, huenda mtoto akahisi njaa na kumlazimisha kuamka usiku na kulilia chakula.

 

Chanzo: British Nutrition Foundation 

Soma Pia: Top 8 foods to feed your child so that they grow taller and stronger

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio