Vyakula Bora Zaidi Kwa Mtu Anaye Kuwa Kazini Wakati Mwingi

Vyakula Bora Zaidi Kwa Mtu Anaye Kuwa Kazini Wakati Mwingi

Kufuatia vitu vingi vinavyo endelea kama vile kufanya kazi muda mrefu ama kuwa shuleni siku yote. Na kufanya wanafamilia kuto pata wakati tosha wa kula chakula wakiwa pamoja. Kuwa kazini siku yote hufanya wazazi wakakosa wakati tosha wa kula na watoto wao na kujipata wakikula chakula ofisini. Watoto hujipata wakila shuleni ama kwa hoteli. Makala haya yana ratiba ya chakula chepesi ambacho unaweza tayarisha kwa mbio.

Vyakula Bora Zaidi Kwa Mtu Anaye Kuwa Kazini Wakati Mwingi

Tazama ratiba hii ya chakula chepesi cha kutayarisha

chakula chepesi

Nchi nyingi za Afrika zina Kilimo. Shamba zina rutuba nyingi na sio rahisi kuathiriwa na matatizo ya anga. Kuna vyakula vingi sana ambavyo unaweza kula. Na pia kila tamaduni nchini huwa na lishe ambazo wanapenda kula.

Katika makala haya, tuna angazia ratiba ya vyakula ambavyo familia nyingi hula wakati mwingi na ambazo zina afya zaidi.

Kidokezo:Ni sawa kupika chakula kingi wiki inapo anza na kukiweka kwenye friji yako na kupasha joto kila mara unapo hisi njaa. Hakikisha kuwa chakula chako ni cha afya na kina lishe tosha.

food time table

Kama tunavyo fahamu, ratiba ya chakula hubadilika, hasa kwa watu ambao wana kuwa kazini ama shuleni muda mrefu. Ni vyema kuwa makini unapo tayarisha chakula.

Chochote ukifanyacho, hakikisha kuwa chakula chako kina kila aina ya chakula kinacho hitajika. Wakati mwingi, huenda ukawa unakula wanga tu na matunda na mboga kidogo. Ratiba yetu inakusaidia kula lishe iliyo sawasishwa.

Kula chakula chenye afya huwa na zaidi ya vitu vilivyo kwa ratiba hii. Pia ina viwango tosha vya mboga, matunda na kuhakikisha kuwa unakunywa maji tosha kila siku.

Vidokezo vya chakula chepesi cha kupika

chakula chepesi

  1. Kula matunda mengi. Zoea kununua matunda mengi nyumbani mwako hasa yanayo kuwa katika msimu. Wahimize watoto wako kula matunda kwa wingi na kula vyakula vya afya.
  2. Kunywa glasi moja ya maji punde tu unapo amka. Kisha unaweza kunywa kiamsha kinywa chako na bakuli ya matunda baada ya hapo. Pia, unaweza kunywa maji na matunda asubuhi ili kuboresha mchakato wa chakula tumboni.
  3. Kula lishe yako saa ama kabla ya saa moja. Ukihisi njaa baadaye, kunywa chai ama chokleti moto na matunda kama vitamu tamu.
  4. Kunywa maji dakika 30 kabla ama baada ya lishe.
  5. Hakikisha kuwa una kunywa maji badala ya vileo ili kukusaidia na uchakataji wa chakula.
  6. Tumia kiwango kidogo cha mafuta.
  7. Kula kiwango kinacho faa cha chakula.
  8. Epuka kunywa kahawa baada ya chajio kwani huenda utaratibu wako wa kulala uka haribika.
  9. Usilale ukikula.
  10. Kula chakula chako pole pole ili kichakatwe kwa urahisi.

1q Food Platter

Soma pia: Food timetable for students on a tight budget

Written by

Risper Nyakio