Lishe ni muhimu sana katika kudumisha afya bora. Wataalum wana shauri kuwa sahani yako inapaswa kuvutia na kuwa na rangi za upinde mvua. Rangi ya kijani, nyeupe, nyekundu na kadhalika. Kula chakula kinacho vutia kutakufanya uwe na hamu ya kula chakula. Pia, chakula hiki kitakuwa cha vikundi tofauti na kuongeza nguvu na virutubisho muhimu mwilini. Tuna angazia chakula katika mimba ambacho mama ana stahili kula.
Kumbuka kuwa lishe ya mama sio ya afya yake peke yake, mbali pia ya fetusi inayo zidi kukua kwenye uterasi yake.
Chakula muhimu kwa mama mjamzito

Ufuta wenye afya ni muhimu sana katika ujauzito. Na mama ana stahili kuhakikisha kuwa ana kula bidhaa zinazo ongeza virutubisho mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha ufuta wenye afya. Kina wingi wa vitamini, fiber, vitamini C, E na copper.
Ni muhimu katika kuboresha na ubora wa ngozi ya mama ambayo huenda ika athiriwa na upele katika mimba. Kukuza tishu, ubongo na ngozi ya fetusi.

Nafaka nzima zina ongeza virutubisho vingi ikilinganishwa na nafaka zilizo chakatwa. Nafaka nzima ni kama vile mkate wa hudhurungi, viazi vitamu na oats.
Huwa na vitamini B, magnesium na hata fiber kwa wingi.

Bidhaa za maziwa ni bora katika kuongeza kalisi na protini mwilini. Muhimu kwa ukuaji wa mtoto na mama. Pia zina ongeza kalisi, vitamini B, phosphorus na zinc mwilini.
Bidhaa kama maziwa, maziwa ya bururu na cheese ni bora. Zina saidia na afya ya mfumo wa kuchakata chakula.

Nyama ya ng'ombe iliyo laini, kuku, pamoja na nyama ya nguruwe ni mojawapo ya vyanzo vyema zaidi vya protini. Zote zina wingi wa iron na vitamini B ambazo ni muhimu sana kwa mama mwenye mimba. Iron ina saidia katika kutengeneza kwa seli nyekundu. Mama anapo kosa seli nyekundu tosha katika mimba, huenda aka tatizika na hali ya anemia.
Hali ya anemia inamweka mama katika hatari ya kujifungua kabla ya wakati kuwadia ama kujifungua mtoto aliye na uzani wa chini.
Mbali na chakula katika mimba tulicho angazia, mama mjamzito ana stahili kuhakikisha kuwa ana kula mboga za kijani. Ni bora katika kuongeza damu mwilini. Zingatia kunywa kipimo cha maji ulicho shauriwa na daktari wako, ama kinacho ambatana na uzani wako wa mwili.
Soma Pia:Umuhimu Wa Lishe Bora Mapema Katika Mimba Ni Upi?