Lishe yenye afya kwa mama mjamzito inapaswa kuwa na wanga, protini, ufuta, madini, vitamini na maji. Madaktari huwashauri wanawake wajawazito wanacho paswa kukula kila siku. Kuhakikisha kuwa sahani ina rangi zote na kila kundi la chakula. Ili wawe na virutubisho tosha kutosheleza mahitaji yao na ya fetusi. Tuna angazia chakula muhimu katika ujauzito.
Tazama virutubisho tofauti na chakula kinacho kuwa na virutubisho hivi:
Protini

Ni muhimu kwa ukuaji wa seli na kuchakata damu. Protini ina patikana kwa vyakula kama nyama, samaki, mayai, maharagwe na nyama kutoka kwa ndege wa kinyumbani.
Wanga
Virutubisho muhimu katika kupata nishati ya kila siku. Zinapatikana kwenye vyakula kama vile mchele, mkate, viazi, matunda na mboga.
Iron
Muhimu katika kutengeneza seli nyekundu za damu. Zina epusha kuugua kutokana na anaemia ama upungufu wa damu mwilini. Vyanzo vikuu vya iron ni kama vile nyama nyekundu laini, mchicha na nafaka nzima.
Kalisi
Inasaidia katika kutengeneza mifupa yenye nguvu, meno, misuli na kuboresha utendaji kazi wa neva mwilini. Inapatikana kwenye vyakula kama vile, cheese, maziwa, maziwa ya bururu, na mchicha na sardines.
Vitamini A

Vitamini A inasaidia kuwa na ngozi laini, kuboresha uwezo wa kuona na ukuaji wa mifupa. Inapatikana kwenye mimea kama vile viazi vitamu, karoti, na mboga za kijani.
Vitamini B6
Inatumika katika kutengeneza seli nyekundu za damu, kuboresha uchakataji wa protini, wanga na ufuta mwilini. Inapatikana kwenye nyama ya nguruwe, ndizi na nafaka nzima ambazo hazija chakatwa.
Vitamini B12

Ina dumisha mfumo wa neva na kuhakikisha una afya. Pia inatumika katika kutengeneza seli nyekundu za damu. Inapatikana kwenye nyama, samaki, maziwa, na wanyama wa nyumbani.
Vitamini C
Ufizi na mifupa yenye afya zina egemezwa na vitamini C. Inatumika kuboresha utumikaji wa iron mwilini. Matunda, nyanya na sharubati za matunda na broccoli ni vyanzo vikuu vya vitamini C.
Vitamini D
Ina saidia kuwa na mifupa na meno yenye nguvu na pia kusaidia katika utumizi mwilini wa kalisi. Vitamini D inapatikana kwenye bidhaa za maziwa, nafaka na mikate.
Ufuta

Hifadhi ya ufuta unao tumika kutoa nishati baada ya vipindi virefu bila kupata chakula. Vyanzo vyake ni kama vile nyama, maziwa, njugu, bidhaa za maziwa na siagi.
Folic acid
Muhimu sana katika mimba. Inasaidia katika kutengenezwa kwa protini na damu. Mboga za kijani na matunda ya kinjano, mboga, njugu na maharagwe huwa na viwango vya juu vya folic acid.
Maji ni sehemu ya lishe. Mama anapaswa kuchukua maji angalau glasi nane kila siku. Kuna virutubisho ambavyo havipatikani kwa idadi tosha kwenye chakula. Na mwanamke hupatiwa tembe anazo paswa kumeza ili kutimiza viwango vya virutubisho vinavyo hitajika mwilini. Ikiwa mama ana tatizika kuchagua chakula muhimu katika ujauzito, ni vyema kuwasiliana na mtaalum wa mlo. Amwagize anacho paswa kula na katika viwango gani.
Soma Pia: Vyakula Visivyo Na Acid Vinavyo Paswa Kuwa Kwenye Lishe Yako Wakati Wote!