Kuna baadhi ya changamoto za kiafya zinazo ibuka katika idadi kubwa ya mimba. Kwa wanawake wengi ila sio wote wanao pata matatizo haya. Tazama baadhi ya changamoto za kiafya katika mimba zilizo maarufu zaidi.
Matatizo ya kiafya yanayo ibuka katika ujauzito
Ukosefu wa maji mwilini

Tatizo hili mara nyingi husababishwa na tembe za vitamini za kabla ya kujifungua ambazo mjamzito anachukua. Kuchukua chakula kilicho na fiber nyingi kunasaidia kukabiliana na tatizo hili. Jaribu kula vyakula kama vile matunda na mboga freshi, mkate wa hudhurungi na nafaka nzima. Kuna tembe za fiber ambazo mama anaweza kutumia ila ni vyema wakati wote kuwasiliana na daktari kabla ya kuzitumia.
Mwanamke anapo zidiwa na tatizo la constipation, kuna dawa zinazo tumika kulegeza choo chake. Kunywa viowevu vingi kuna saidia na tatizo hili. Kuhakikisha kuwa ana kunywa maji siku yote na baada ya kila lishe.
Kichefu chefu
Kichefu chefu husababishwa na mabadiliko ya homoni ya mimba mwilini. Mara nyingi hushuhudiwa asubuhi, ila pia kinaweza kushuhudiwa wakati wowote ule. Kupunguza athari za kichefu chefu katika mimba, mama anaweza kula crackers anapo amka kabla ya kutoka kwenye kitanda. Kunywa maji yenye tangawizi hupunguza athari hizi. Kula chakula kidogo kwa mara zaidi.
Gesi
Kuna wanawake wanao pata gesi na kiungulia baada ya kula chakula fulani. Chakula kama mchicha, chakula kilicho kaangwa na ufuta mwingi, broccoli na vinywaji kama soda. Ni vyema kula chakula kilicho sawasishwa na kuwasiliana na daktari ili akupatie mbadala bora.
Vyakula vya kujitenga navyo katika mimba

Kuna baadhi ya vyakula vinavyo ongeza hatari ya mwanamke mjamzito kuugua matatizo yanayo ambatana na chakula. Kama vile:
- Maziwa ambayo haijapikwa
- Siki ya apple cider
- Nyama mbichi ama ambayo haija iva vizuri
- Nyama iliyo chakatwa kama hot dogs, hakikisha imeiva vya kutosha
- Samaki walio na viwango vya juu vya mercury kama swordfish
- Mayai mbichi ama chakula kilicho na mayai mbichi kama mayoinnaise
Soma Pia:Jinsi Ya Kuzuia Kutunga Mimba Kiasili Baada Ya Ngono