Changamoto Mama Anazo Kumbana Nazo Anapo Nyonyesha

Changamoto Mama Anazo Kumbana Nazo Anapo Nyonyesha

Mama anapo anza kunyonyesha, huenda akatatizika kutokana na ukavu na kupasuka kwa chuchu. Chuchu zilizo pasuka zitamfanya mama ahisi uchungu anapo nyonyesha.

Kuna changamoto nyingi ambazo mama anakumbana nazo wakati ambapo anaanza kunyonyesha mtoto. Tazama baadhi ya changamoto za kunyonyesha kwa mama.

  • Ukavu na chuchu kupasuka

Mama anapo anza kunyonyesha, huenda akatatizika kutokana na ukavu na kupasuka kwa chuchu. Chuchu zilizo pasuka zitamfanya mama ahisi uchungu anapo nyonyesha. Kwa mama wa mara ya kwanza, huenda akawa na hofu ya kunyonyesha ama kuchukia wakati huu.

Ni vyema kuwa mtulivu na kukumbuka kuwa uchungu huu utaisha. Tumia krimu zisizo na kemikali za vileo kupaka kwa chuchu zako. Epuka kupaka sabuni kwenye chuchu zako. Unapo tumia krimu kwa chuchu baada ya kunyonyesha kuwa makini kupanguza chuchu zako kabla ya kumnyonyesha mtoto tena.

  • Upungufu wa maziwa

kuumwa na chuchu

Hili ni jambo sugu linalo weza kuwaathiri wanawake. Mama anapo kuwa na mawazo mengi, kiwango cha maziwa kinacho tolewa kinapungua. Mama aliye jifungua anashauri kujitenga na mawazo mengi ili kuhakikisha kuwa ana maziwa tosha ya kumlisha mtoto.

Kwa mama anaye tatizika na kiwango kidogo cha maziwa, ni vyema kumnyonyesha mtoto mara nyingi. Kwa njia hii, uta chechemua homoni mwilini kutoa maziwa zaidi. Tatizo hili linapo zidi, ni vyema kuwa siliana na daktari wako.

  • Vidonda kwenye chuchu

Kuna uwezekano wa mama kupata vidonda kwenye chuchu wiki ya kwanza anapo anza kumnyonyesha mwanawe. Hakikisha kuwa unampakata mtoto vizuri na kumwekelea kwenye chuchu. Ili mdomo wake ushike chuchu inavyo paswa. Mtoto anapo maliza kunyonya, tumia kidole kimoja kuutoa mdomo wake kutoka kwa chuchu.

Mama anaye tatizika na vidonda ana shauriwa kuzidi kumnyonyesha mtoto. Uchungu unapo zidi na unashindwa kabisa kumnyonyesha, likamue ziwa kisha umlishe kutumia vichupa.

  • Kuziba kwa mifereji ya maziwa

changamoto za kunyonyesha

Hali hii ya kuziba kwa mifereji ya maziwa mara nyingi husababishwa na maziwa kuto toka kwa ufanisi. Mifereji ya maziwa inapo ziba, kiwango cha maziwa ambacho mtoto anapata kitapungua.

Mama aliye anza kunyonyesha huenda aka tatizika na kuwa na maziwa nyingi kwenye chuchu. Hii sio hali ya kutia kiwewe. Ni jambo la kawaida. Ikiwa maziwa ya mama ni mengi na sio magumu, usiwe na shaka. Ikiwa una tatizika na mojawapo kati ya changamoto za kunyonyesha tulizo angazia, hakikisha una wasiliana na daktari wako.

Soma Pia:Njia 9 Dhabiti Za Kuongeza Utoaji Wa Maziwa Ya Mama

Written by

Risper Nyakio