Changamoto Za Mimba Kutokana Na Lishe Yenye Kiwango Kidogo Cha Wanga

Changamoto Za Mimba Kutokana Na Lishe Yenye Kiwango Kidogo Cha Wanga

Changamoto za mimba kutokana na kula lishe isiyo na wanga nyingi kunaweza sababisha matatizo ya maumbile kwa mtoto hasa maradhi ya neural tube defects (NTDS).

Wanawake wengi siku hizi wana amini lishe zilizo na viwango vidogo vya wanga (kama vile Atkins, Paleo, Keto ama bila gluten) zina manufaa kwa afya yao. Walakini, ikiwa wana panga kuwa na watoto, changamoto za mimba kutokana na lishe yenye wanga ndogo huenda zika ibuka, kulingana na utafiti mpya.

Utafiti wa hivi majuzi ulio chapishwa kwenye makala ya Birth Defects Research uli vumbua kuwa wanawake wanao zingatia lishe yenye wanga ndogo wana nafasi asilimia 30 zaidi za kujifungua mtoto mwenye changamoto za kiafya.

Somo lili angalia ujumbe kutoka zaidi ya wamama 11,000 walio jifungua katika kipindi cha miaka 13. Walicho pata watafiti hawa kutoka Chuo Kikuu cha North Carolina huko Chapel Hill ni cha kuhuzunisha.

Changamoto za mimba kutokana na lishe yenye wanga ndogo

changamoto za mimba kutokana na lishe

"Tuligundua kuwa wanawake wanao kula lishe isiyo na viwango tosha vya wanga kabla ya kujifungua walikuwa katika hatari zaidi ya kujifungua mtoto mwenye changamoto za neural tube ikilinganishwa na wanawake wengine," alisema mtafiti mkuu daktari Tania Desrosiers kutoka shule ya Afya ya Umma ya UNC Gillings.

"Haya ni muhimu kwa sababu yana elekeza kwa nafasi ya kuepuka baadhi ya changamoto za kuzaliwa katika siku za usoni."

Changamoto za mimba kutokana na kula lishe isiyo na wanga nyingi kunaweza sababisha matatizo ya maumbile kwa mtoto hasa maradhi ya neural tube defects (NTDS). Ama pia spina bifida ambapo uti wa mgongo una mea usivyo paswa ama anencephaly ambayo ni kutokuwepo kwa sehemu za ubongo.

Mwishowe changamoto hizi za kuzaliwa husababisha matatizo ya muda mrefu ama nyakati zingine kifo cha mtoto.

Ni kuhusu folic acid

changamoto za mimba kutokana na lishe

Watafiti wali ashiria uhusiano kati ya lishe yenye wanga ndogo na NTDS kuwa folic acid. Folic acid ni mojawapo ya virutubisho muhimu sana inayo julikana sana kwa kuepusha NTDs. Hii ndiyo sababu kwa nini vitamini za mama mjamzito zina wingi wa folic acid.

Hii ndiyo sababu kwa nini baadhi ya serikali zina himiza folic acid iongezwe kwa bidhaa za nafaka kama vile mkate, pasta, wali na nafaka.

Wanawake wanapo anza kuzingatia lishe yao na kupunguza wanga, wanakosa vyakula vilivyo ongezwa folic acid. Na kusababisha matatizo ya mimba kutokana na mwili kutopata wanga tosha.

"Kama jamii ya kisayansi, tume shangaa kama lishe zenye wanga ndogo huenda zika sababisha viwango vidogo vya ulaji wa folic acid na mwishowe kusababisha hatari za kupata mtoto aliye na neural tube defect," Desrosiers alisema. Somo hili ndilo la kwanza kutafiti swali hili.

Kiwango kinacho shauriwa

Somo hili lili onyesha kuwa wanawake wanao chukua lishe isiyo na wanga tosha wanapata nusu ya kiwango cha folic acid kinacho shauriwa ikilinganishwa na wanawake wengine wanao husisha wanga kwenye lishe zao.

"Wanawake wajawazito ama wanawake wanao jaribu kupata mimba wanapaswa kuwa na mazungumzo haya na wataalum wao wa afya kuhusu lishe na mitindo yoyote ile ya vyakula spesheli," aliongeza Desrosiers.

"Na waendelee kuchukua vitamini kila siku kabla na wanapokuwa na mimba zilizo na 400mg za folic acid," alisema.

Wamama wana hitaji lishe bora

Folate ni aina asili ya folic acid, kwa hivyo wamama watafanya vyema wakikula chakula kilicho na wingi wa folate. Hizi ni kama vile mboga za kijani, kunde, maharagwe, machungwa na parachichi.

Ni vyema kukumbuka kuwa wazazi wengi huwa hawapangi ujauzito wao. Kwa hivyo wanawake walio katika miaka yao ya uzazi wanapaswa kuwa makini na ulaji wao wa folate ama folic acid.

Soma Pia:Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

Written by

Risper Nyakio