Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo

3 min read
Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana NayoChangamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo

Mtoto wako anapo zidi kukua, utakumbana na changamoto ya kumwachilia apate uhuru wake. Na ni vigumu kwa mzazi kumwachilia.

Kuwa mama ama baba ni kusawasisha kuwatunza watoto wako huku ukiwapatia uhuru wa kukua na kusoma kutoka kwa makosa yao. Jukumu lako kama mzazi ni kuwapenda na kuwalinda kutokana na uchungu wa aina yoyote na mabadiliko yasiyo wafurahisha na kukubali kuwa, mtoto wako anayekua atahitaji kushuhudia athari za vitendo vyake. Wazazi hukumbana na changamoto nyingi za ulezi na hasa ambazo hawakufahamu kabla ya kupata watoto.

Baadhi ya changamoto za ulezi

changamoto za ulezi

  1. Jinsi ya kuwa mzazi kwa mtoto uliye naye, sio mtoto ambaye unatamani ungekuwa naye

Mara nyingi, huenda ukapata mzazi analea watoto wake kulingana na wazo alilo nalo kuhusu anavyo fikiria watoto wake wanapaswa kuwa na sio vile walivyo. Ni vigumu na kunachosha kulea watoto wasio na heshima na wasio kusikiza ama mtoto aliye na matatizo ya kimaumbile. Ama kuwa na mtoto aliye tofauti sana nawe. Kwa hivyo kuona anavyo fanya mambo yake kunaweza kuwa ni jukumu linalo kuchosha.

Mara kwa mara, mzazi atahitajika kukubali kuwa mwanawe hatakuwa alivyo kusudia angekuwa. Unapo mkubali mtoto wako jinsi alivyo, aina tofauti ya mapenzi hukua. Pia, kumkubali mtoto kutamfunza kujikubali alivyo.

2. Jinsi ya kumwacha mtoto ashuhudie athari za matendo yake kiasili

Sio wazo la busara kujaribu kumlinda mtoto wako kutoka kushuhudia athari za matendo yake. Kufanya hivi hakutampea mwanya wa kufahamu athari za uamuzi  usio wa busara wa matendo yake. Wanadamu husoma kutokana na matendo yao. Na ndiyo njia asili ya kusoma. Ukiadhibiwa mara ya kwanza baada ya kufanya tendo fulani, una gundua kuwa haupaswi kuli rudia.

Unapo mlinda sana mtoto wako, hatajua mambo asiyo paswa na anayo paswa kufanya. Ni vyema kuwapa mwanya wa kusoma haya, lakini hakikisha kuwa unawa shauri wakati wote.

3. Kulaumiwa na wengine

changamoto za ulezi

Ikiwa mtoto wako hujiingiza katika tabia zisizo kubalika kwa jamii, kubishana na watu ama vitendo vinavyo onyeshana kukosa heshima. Huenda ukawa ume pata watu wakikuangalia na kushangaa ni nini kina kusumbua? Kwa nini humfunzi mtoto wako tabia nzuri?

Kuangaliwa kwa njia hii kutamfanya mama ahisi kuwa hafanyi mambo tosha kumlea mwanawe. Hata unapo tia juhudi kuhakikisha kuwa mtoto anakua vyema. Ukweli ni kuwa, mara kwa mara, uta laumiwa na ni asili. Unapo hisi kuwa kila mtu ana kulaumu, jikumbushe kuwa huwezi soma akili zao, na huenda fikira zao zikiwa mbali sana.

4. Jinsi ya kuwaachilia watoto wako

Mtoto wako anapo zidi kukua, utakumbana na changamoto ya kumwachilia apate uhuru wake. Hili huenda likawa gumu ikiwa inaonekana kuwa mtoto wako anahitaji kusoma mambo kwa njia ngumu. Na mara kwa mara ata vunja sheria za nyumba na kufanya mambo tofauti na unavyo kusudia.

Hata kama ni jambo gumu kwa mzazi, elewa kuwa huwezi mshika mtoto wako hadi akomae, kuna mambo utamfuna na mengine atafunza na dunia.

Ni vigumu kwa wazazi kujua kilicho sawa wakati wote. Ukweli ni kuwa, hakuna jambo sawa. Ni muhimu kukubali kuwa hautakuwa sawa wakati wote, na ni sawa.

Soma Pia:Vidokezo Vya Kuwa Mzazi Bora

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Changamoto Za Ulezi: Mambo 4 Magumu Ambayo Wazazi Hukumbana Nayo
Share:
  • Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)

    Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)

  • Changamoto Za Kuwa Mzazi Mmoja Na Jinsi Ya Kuwa Mzazi Mmoja Bora

    Changamoto Za Kuwa Mzazi Mmoja Na Jinsi Ya Kuwa Mzazi Mmoja Bora

  • Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

    Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

  • Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

    Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

  • Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)

    Matatizo Ya Ulezi (Changamoto 3 Kuu Za Ulezi Katika 2021)

  • Changamoto Za Kuwa Mzazi Mmoja Na Jinsi Ya Kuwa Mzazi Mmoja Bora

    Changamoto Za Kuwa Mzazi Mmoja Na Jinsi Ya Kuwa Mzazi Mmoja Bora

  • Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

    Je, Unafahamu Mbinu Hatari Ya Ulezi Ya Sharenting?

  • Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

    Njia Ya Ulezi Ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it