Baadhi ya changamoto 11 zinazo ukumba uzazi katika nchi ya kenya

Baadhi ya changamoto 11 zinazo ukumba uzazi katika nchi ya kenya

Ni muhimu kwa kila jamii kuelimishwa jinsi tofauti za kupanga uzazi. Kuna changa moto mbali mbali zinazo ikumba familia na kufanya wengi wao kutofuata njia hizi. Kama vile tamaduni za familia.

Changamoto 11 Zinazo Ukumba Uzazi Kenya 

Je, changamoto za uzazi ni zipi, haswa nchini Kenya? Uzazi ni njia ya kibiolojia ambapo kiumbe kilicho uhai chaweza kupata kiumbe chingine. Ya kujilakana kama kuzaa miongoni mwa wanyama na kujifungua katika watu. Uwezo wa kuzaa na kupata watoto ni moja wapo wa sifa kuu zinazo tambulisha uhai miongoni mwa binadamu. Viumbe vyote duniani vimetokana na tendo hili la uzazi. Uzazi unachangia katika uongezefu wa idadi ya watu katika nchi. Nchi ya Kenya inasemekana kuwa na zaidi ya watu million arobaini na mbili. Njia za kupanga uzazi ni muhimu katika kila nchi kupunguza idadi ya watu. Pia ni muhimu kuhakikisha pia hakuna watoto wanaozaliwa bila ya kupangia. Inasaidia watu kujipanga kwanza kabla kupata watoto. Na kupunguza idadi ya watoto walio kwa mitaa kufuatia kuwachwa na wazazi wao Kwani hawana cha kuliwasha nacho. Nchi pia inaweza kuwapa watoto walio zaliwa mahitaji ya kimsingi. Kufuatia haya masomo bora ya upangaji uzazi ni muhimu katika nchi.

Masuala ya upangaji uzazi kwa wanawake na wanaume limekua wazi kwa muda. Iwapo kuna watu bado hawataki kuwa na mjadala kuhusu jambo hili. Kufuatia maadili yao ama ata dini wanazo zifuata. Licha ya dini ya mtu, ni muhimu kukabiliana na mjadala huu Kwani ni jambo la muhimu kwa maisha yetu na nchi pia.

Kuna njia tofauti za upangaji uzazi ambazo watu wanaweza kutumia. Miongoni mwao ni:-

  • Kutumia vidonge
  • Kutumia kizuizi cha julikana kama kondom
  • Kudungwa sindano kwa mabinti
  • Kuweka kijiti ama kwa jina linguine kipandikizi

Baadhi ni changamoto zinazo ukabidhi upangaji uzazi Kenya

changamoto za uzazi

1. Utamaduni

Utamaduni ni mojawapo wa changamoto zinazo changia katika watu kuto tumia njia tofauti za upangaji uzazi.

2. Shida za kiafya

Iwapo upangaji uzazi ni mwema, unaleta madhara tofauti kwa wanao tumia njia hizi. Na kuathiri afya zao kwa njia hasi.

3. Viwango vya chini vya kimasomo

Wananchi wengine haswa wanao ishi kwa vijiji wana viwango duni vya kimasomo. Hawana elimu inayotosha na hawaelewi faida za kutumia njia za kupanga uzazi. Unapata ni sehemu ndogo ya watu wanaoishi huko wanao tumia njia hizi.

4. Dini tofauti

Kuna dini tofauti katika nchi. Miongoni mwa dini hizi, kuna baadhi zao ambazo wanapinga Utumiaji wa njia za kupanga uzazi. Wengine wasema kuwa haiambatani na neno la Mungu la kuzaa na kujaza dunia. 

5. Kukosa elimu bora

Japo kuwa serikali inafanya jitahada za kuwa elimisha wananchi wake kuhusu njia tofauti za kupanga uzazi. Sio kila mja katika nchi hii ya Kenya anapata elimu hii. Uongozi wa nchi hili wahitajika kuimarisha njia za kuelimisha wanawake na pia wanaume kuhusu jambo hili.

6. Maadali tofauti

Wananchi katika nchi hili la Kenya wana maadali tofauti. Kwa sehemu zingine za nchi, ni vibaya kufanya mapenzi kabla kuolewa. Jambo hili lina leta kero kwa wazee wao wanapo jua. Kufuata hii, wanao jihusisha na jambo hili hawana elimu ya kutosha ya kujikinga kutokana na maradhi ama kupata mimba bila ya kupanga.

7. Kutokua huru kati ya familia

Elimu ya kupanga uzazi inafaa kuanza kwa familia. Miongoni mwa familia nyingi katika nchi hii hawako huru. Wazazi hawajui kua ni jukumu lao kuwa funza watoto wao kuhusu njia hizi. Wana litwika jukumu hili kwa walimu. Ni muhimu elimu hii kuanza kwa wazazi.

8. Kuto husisha wanaume

Wanaume wamejitenga na jambo hili la kupanga uzazi na kuwaachia wanawake. Wanaume wanafaa kuelimishwa kuhusu kupanga uzazi na wafahamu kuwa pia wanafaa kuchangia katika jambo hili.

9. Imani zisizo faa

Baadhi ya watu bado wanashikilia Imani zilizo pitwa na Wakati kuhusu kupanga uzazi. Miongoni mwao wana amini kuwa zina wafanya wanawake kuwa tasa na pia kuchangia kupata kansa kwa wanawake ambalo si kweli.

10. Upatikanaji wa tembe kwa urahisi

Tembe zinazo kunywiwa asubuhi baada ya kujihusisha kwa mapenzi yana patikana kwa urahisi. Unapata kuwa ma binti katika nchi hii wanameza tembe hizi zaidi ya mara inayo hitajika.

11. Ndoa za mapema

Miongoni mwa mabinti katika nchi ya Kenya wanaoleka kwa umri mdogo. Jambo hili ni mojawapo wa changamoto za upangaji uzazi katika nchi hili.

Upangaji uzazi ni suala muhimu katika nchi. Uongozi wa nchi unachangia pakubwa katika wananchi wake kuelimishwa na kutumia njia bora za upangaji uzazi. Kuhimizwa kwa wanawake na waume ni muhimu na lafaa kupewa kipao mbele. 

Read Also: Who Does Serena Williams Turn To For Parenting Advice?

 

Written by

Risper Nyakio