Mambo Yanayo Fanyika Mwilini Mwako Lango La Uzazi Linapo Panuka

Mambo Yanayo Fanyika Mwilini Mwako Lango La Uzazi Linapo Panuka

The process of Cervical dilation near delivery usually happens at the end of the third trimester. Do you know what needs be done, mums?

Unapo karibia kupata uchungu wa uzazi, mlango wa tumbo la uzazi hupanuka – ishara nzuri kuwa mtoto ako tayari kuzaliwa. Wakati unaohitajika ili kupanuka kutoka kwa sentimeta moja hadi kumi hutofautiana:  Kila mama huchukua muda tofauti.  Kina mama wengine huchukua masaa – ama siku – ili mlango wa uzazi kupanuka kikamilifu. Kupanuka kwake hulingana na hali ya mwili ya mama. Pia uwezo wa mwili kupanuka ili kufanya mwanya wa mtoto kuzaliwa. Katika makala haya tumetia ndani chati ya kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi ili uweze kujua unacho tarajia kabla ya kujifungua.

Nini hutendeka mlango wa tumbo la uzazi unapopanuka kutoka sentimeta moja hadi kumi: Chati ya kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi.

Kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi wa sentimeta moja kuna maanisha kuwa unafaa kuelekea hospitali karibuni.

tumbo la uzazi kupanuka

Cervical dilation chart: The first sign of your cervix dilating during delivery is when your water breaks. | Image Source: Stock Photo

Daktari wako wa wanawake atakwambia kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi unafaa kuanza lini. Kupanuka kwa sentimeta moja inamaanisha mwili wako uko tayari kujifungua, lakini haina maana kuwa utapatwa na uchungu wa uzazi mara moja.

Wakati mlango wa tumbo la uzazi umepanuka kwa sentimeta moja, kunaweza kuwa hakutakuwa na kupanuka zaidi  ila baada ya wiki kadhaa.

Daktari. Robert Atlas, daktari wa mambo ya ukunga na wanawake kutoka kituo cha Mercy Medical Center huko USA, asema kuwa kila mgonjwa huwa tofauti. Unapo jifungua, upanukaji huu huenda ukachukua muda mrefu iwapo ni mimba yako ya kwanza.  Hii ni kwa sababu mwili wako unahitaji kujirekebisha, na awamu za kwanza za uchungu wa mtoto.

Tarajia kubanwa mlango wa tumbo la uzazi unapopanuka kwa sentimeta 5

tumbo la uzazi

Cervical dilation chart: When your cervix dilates past 5cm, you will start to feel contractions to help you push the baby out. | Image Source: Stock Photo

Mara mlango wa tumbo la uzazi unapopanuka kwa sentimeta tano na umeanza kuhisi kubanwa, umiengia kwa awamu ya kwanza ya uchungu wa uzazi.

Kulingana na Daktari Atlas, awamu ya kwanza ya uchungu wa uzazi ni ishara kuwa mama anajitayarisha kupata mtoto.  Walakini, kupanuka kwa sentimeta tano haimaanishi kuwa mtoto atazaliwa hivi karibuni.

Habari njema ni kuwa kubanwa katika hii awamu hutofautiana kati ya uchungu kidogo hadi ule wa wastani.  Kwa hivyo unaweza kuwa mtulivu. Pia, kubanwa huja baada ya kila dakika chache.  Mara nyingi unaweza kuendelea na kazi zingine kati ya kubanwa, kina mama.

Kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi wa sentimeta tano pia unamaanisha kuwa mlango wa uzazi unanyooka na kulainika. Ili kuwezesha mtoto kutoka kwa tumbo lake, kwenda kwa uke na hatimaye kuzaliwa.

Kupanuka kwa sentimeta 6  kunamaanisha mtoto anajitayarisha kuzaliwa!

chati ya tumbo la uzazi kupanuka

Cervical dilation chart: Katika sentimeta  10, mtoto yu tayari kuzaliwa kufuatia msaada wa kusukuma kutoka kwa mama. | Image Source: Stock Photo

Sentimeta kumi: Sukuma!

Mlango wa tumbo la uzazi uliopanuka kwa sentimeta kumi unamaanisha kupanuka kumefika mwisho. Ina maana kuwa njia ya uzazi imefunguka na unaweza anza kusukuma. Mlango huu umerefuka na tumbo la uzazi limebana ili uweze kumzaa mtoto.

Daktari ataanza kukuelekeza kusukuma. Iwapo, mlango huu umepanuka kikamilifu na mtoto bado hajazaliwa baada ya muda, madaktari huingilia kati ili kuharakisha kuzaa mtoto.  Mifano ni kama kutumia koleo, vacuum, vifaa vya kumvuta mtoto ama upasuaji.

Kupanuka kwa tumbo la uzazi hutofautiana kwa kila mama

tumbo la uzazi

Kina mama, Daktari Atlas asisitiza kwa mara nyingi kuwa kupanuka kwa mlango huu wa uzazi hutofautiana kwa kila mama. Kwa hivyo hufai kuwa na wasiwasi kuhusu kupanuka kwa mlango wako wa uzazi.

Daktari Atlas mwenyewe mara nyingi hupatana na wagonjwa ambao huwa na kubanwa kwa wingi lakini mlango huu wa uzazi haupanuki. Na kwa upande mwingine, kina mama wengine hupanuka mlango wa tumbo la uzazi bila ya kubanwa au maumivu yoyote. Kuna wale ambao huwa hawapatwi na kubanwa au kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi lakini huweza kuzaa mtoto kwa wepesi.

Iwapo saa hizi uko mjamzito na unatarajia kujifungua hivi karibuni, tuliza akili yako.  Usiwaze juu ya kupanuka kwa mlango wa tumbo la uzazi na kadhalika.

Kumbuka kuwa kila mtu huwa na viwango vya upanukaji tofauti na mwingine.  kwa hivyo wewe pia unafaa kujitayarisha  kwa uwezekano wowote wakati wa uchungu wa uzazi baadaye.

Ni matumaini yetu kuwa haya maakala yamewasaidia kina mama.

Reference: American Pregnancy Association

Written by

Risper Nyakio