Chuchu kuuma baada ya hedhi huwa ishara ya PMS na ni jambo linaloshuhudiwa na wanawake wengi duniani kote. Maumivu haya ya chuchu huenda yakawa ishara kabla ya hedhi, baada ya hedhi ama kufuatia sababu zingine.
Kuna aina mbili ya maumivu ya chuchu. Aina ya mzunguko na yasiyo ya mzunguko. Aina ya maumivu ya mzunguko huja kabla ya kipindi cha hedhi, huku maumivu yasiyo ya mzunguko yakishuhudiwa baada ya hedhi kuisha.
Vyanzo vya chuchu kuuma baada ya hedhi

Sawa na viungo vingine vya mwili, kuna sababu nyingi za kuumwa na chuchu. Kufahamu chanzo cha maumivu haya kunasaidia kujua matibabu dhabiti na jinsi ya kutuliza uchungu huo.
- Ujauzito
Mojawapo ya vyanzo vya maumivu ya chuchu baada ya hedhi ni kuwa na mimba. Kuumwa na chuchu huenda kukaashiria kuwa mwanamke ana ujauzito. Maumivu ya aina hii husababishwa na mabadiliko ya homoni mwilini kufuatia kushika mimba.
2. Kunyonyesha
Sababu nyingine ya kuumwa na chuchu ni mama anaponyonyesha. Kulingana na baadhi ya wanawake, uchungu wa kunyonyesha siku za kwanza huwa mwingi kuliko wa kujifungua. Hata hivyo, mama anaweza kupunguza uchungu huu kwa kupiga chuchu masi kutumia maji ya vuguvugu kisha kupaka maziwa ya nazi.
3. Chuchu kuwa nzito
Wanawake walio na maziwa kubwa na nzito wanaweza kupata uchungu kufuatia mishipa iliyonyooka zaidi. Wanawake wasiofahamu saizi za sindiria zinazowafaa pia wako katika hatari ya kuumwa na chuchu.

4. Mastitis
Kukauka na kupasuka kwa chuchu mama anaponyonyesha kunaweza sababisha maambukizi kama ya mastitis. Mama huhisi uchungu mkali kwenye chuchu zilizofura. Daktari atampatia dawa za kuponya ugonjwa huu.
5. Upasuaji wa maziwa
Mwanamke anaweza kupata maumivu ya maziwa katika shughuli zake za kila siku. Kwa mfano anapogongwa ama hata kujiumiza akicheza ama kufanya mazoezi. Enda kwenye kituo cha afya unapogundua kuwa chuchu zimefura ama zinatoa usaha.
Kuna sababu nyingi zinazosababisha chuchu kuuma baada ya hedhi. Iwapo swali lako kuu lilikuwa chuchu kuwasha baada ya hedhi ni dalili ya nini? Tuna tarajia kuwa sasa hivi una maarifa zaidi. Unapopata maumivu kwenye maziwa, hakikisha kufanyiwa vipimo kudhibitisha chanzo chake kabla ya kuchukua dawa zozote.
Soma Pia: Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo