Wanawake wengi hushuhudia aina ya maumivu kwenye chuchu katika wakati mmoja maishani mwao. Chuchu kuuma ni dalili ya mimba? Swali maarufu kwa wanawake wanapopata aina yoyote ya maumivu ya chuchu. Chuchu kuuma ni mojawapo ya dalili za mimba kwa baadhi ya wanawake, ila, sio kwa wanawake wote. Maumivu haya sio ishara ya kuwa na mimba wakati wote, kuna sababu tofauti zinazosababisha maumivu haya.
Sababu Za Chuchu Kuuma

- Mabadiliko ya homoni mwilini
Chanzo kikubwa katika maumivu ya chuchu kwa wanawake. Siku chache kabla ya kuanza kwa hedhi, mwanamke hushuhudia mabadiliko kwenye maziwa, kama vile maumivu ya chuchu ama kuhisi kana kwamba yamefura. Maumivu ya chuchu wakati wa hedhi ni jambo la kawaida na wala sio chanzo cha shaka kwa mwanamke. Ili kupunguza maumivu wakati huu, ni vyema kupunguza unywaji wa kaffeini na bidhaa zake, kula lishe yenye ufuta wa chini, na kujitenga na uvutaji wa sigara.
2. Kutumia sindiria zisizofaa
Kuvalia saizi ya sindiria isiyofaa humfanya mwanamke kupata maumivu kwenye chuchu. Mwanamke anapaswa kupimwa ili kufahamu saizi inayomfaa ya sindiria kuepuka maumivu hasa anapofanya mazoezi.
3. Maumivu kwenye maziwa

Sawa na sehemu yoyote ya mwili, kupata ajali kwenye maziwa kutasababisha maumivu makali. Huenda mwanamke akagongwa akifanya mazoezi na kusababisha maumivu ya siku ama wiki chache baada ya ajali. Kuwa na ishara kama kufura kwa maziwa, kuwa rangi nyekundu ama kidonda kwenye maziwa ni ishara ya maumivu kwenye maziwa, wasiliana na daktari wako.
4. Kunyonyesha
Maumivu ya chuchu kufuatia kunyonyesha husababishwa na jinsi mtoto anavyonyonya maziwa. Kuumwa kwa chuchu ama kupasuka kufuatia kukauka kwa ngozi. Mama anayenyonyesha anaposhuhudia maumivu ya chuchu, ni vyema kuwasiliana na daktari wake.
5. Maambukizi kwenye maziwa
Wanawake wanaonyonyesha wana nafasi zaidi ya kupata maambukizi kwenye maziwa. Ishara zake ni maumivu, chuchu kugeuka rangi kuwa nyekundu na kufura. Wasiliana na daktari unapogundua kuwa una ishara hizi.
Hata kama chuchu kuuma inafahamika ni dalili ya mimba wakati mwingi, huenda ikaashiria suala sugu mwilini. Unapokuwa na uhakika kuwa hauna mimba na bado unapata maumivu makali kwenye chuchu, wasiliana na mtaalum wa afya.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Faida 7 Za Kufanya Yoga Kwa Afya Yako