Baada ya miezi tisa ya kungoja, mtoto kurusha miguu akiwa tumboni na mama kutamani kupatana naye, wakati wake unawadia. Kabla ya miezi tisa kutamatika, mama huwa amepanga mkoba wake wa kwenda kujifungua huwa tayari. Mkoba huu huwa na vitu muhimu atakavyo hitaji siku hiyo. Nguo safi za mtoto mchanga, mavazi yake ya kubadilisha, pamba, na vinginevyo. Kuna uamuzi muhimu ambao wanandoa wanapaswa kufanya. Nani atakaye kuwa katika chumba cha kujifungua? Uamuzi huu unapaswa kufanywa mapema na kuwajulisha watakao jiunga nanyi.
Mambo ya kuangalia kabla kufanya uamuzi

Kujadili na mchumba wako kuhusu marafiki ama wanajamii ambao ungependa wawe nawe ni muhimu. Tengenezeni orodha ya majina ya watu ambao wanaweza faa jukumu hili. Kufanya hivi kunampa imani kuwa hata kama hata weza kufika siku hiyo, mama ako mikononi mwa watu anao waamini. Hakikisha kuwa unamjuza daktari wako kuhusu nambari ya watu ambao ungependa wajiunge nawe katika chumba cha kujifungua.
- Uhusiano wenu na watu ulio wachagua
Wakati wote tunapokuwa na suala lolote, ni jambo la kawaida kuwaendea watu walio karibu nawe. Hasa watu unao hisi kuwa wanakuelewa, vivyo hivyo katika kujifungua. Wanandoa huchagua marafiki wa karibu ama wanafamilia walio na ushirikiano wa karibu. Hakikisha kuwa mna jadili na mchumba wako na kisha kuwa fahamisha kabla ya siku hiyo kufika. Wanastahili kupata wakati tosha wa kujipanga.

Hospitali nyingi hukubalisha wageni wakati mama anapo jifungua. Hata hivyo, sio kila mtu anaye kubalishwa kuingia katika chumba cha kujifungua. Mara nyingi huwa watu wawili wa ziada wanao kubalishwa kujiunga na mama anapo kuwa katika chumba cha kujifungua. Mama anahitaji nafasi bila kuhisi kana kwamba chumba hicho kimejaa zaidi. Pia madaktari wanahitaji nafasi tosha songa wanavyo hitajika. Hakikisha kuwa mnawasiliana na hospitali hiyo ili mfahamu sheria zake.
Kuna baadhi ya wanandoa ambao wangependa kuwa na mpiga picha katika chumba cha kujifungua. Ikiwa hili ni jambo ambao mngetaka, ni vyema kujipanga na kuchagua mpiga picha ambaye mngependa na kisha kumfahamisha muda kabla.
Chanzo: healthline
Soma Pia:Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua