Je, Kwa Nini Kipindi Changu Cha Hedhi Kimechelewa? Mambo Yanayo Sababisha

Je, Kwa Nini Kipindi Changu Cha Hedhi Kimechelewa? Mambo Yanayo Sababisha

Huenda ukawa miongoni mwa asilimia ya watu wanao kimbilia kutumia chumvi kupima mimba ama mbinu nyingine ili kudhihirisha iwapo wana tarajia mara tu wanapo kosa kushuhudia kipindi chao cha mimba. Ila, je, kuwa na mimba ndiyo sababu pekee inayo sababisha kipindi cha hedhi kuchelewa? La, hasha. Makala haya yana angazia sababu tofauti ambazo husababisha kipindi cha hedhi kuchelewa.

Kuna vipindi viwili katika maisha ya wanawake ambapo ni kawaida kwa vipindi vyake vya hedhi kutokuwa vya kawaida. Kipindi cha kwanza ni pale anapo anza kushuhudia vipindi vyake vya hedhi. Na pili, vipindi vya hedhi vinapo isha, al maarufu kama menopause kwa kimombo. Kabla ya umri huu kuwadia katika maisha ya mwanamke, hedhi yake huja baada ya siku 28. Ila siku hizi huwa tofauti kwa kila mwanamke, kati ya siku 21 hadi 35.

Kipindi chako kinapo chelewa na kuwa zaidi ya siku tulizo angazia. Huenda ikawa ni kwa sababu ya mambo yafuatayo.

Sababu Za Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi

  1. Uzito Mdogo Wa Mwili

Wanawake walio na matatizo ya kula, kama vile anorexia huenda wakakosa kushuhudia vipindi vyao vya hedhi. Uzito chini ya asilimia 10 ya uzito wa kawaida huenda ukabadilisha jinsi mwili unavyo fanya kazi na kukomesha kupevuka kwa yai. Ni vyema kupata ushauri wa kimatibabu kukusaidia kusuluhisha kasoro zako za kula. Kuongeza uzito kwa njia yenye afya kutakusaidia na kipindi chako. Wanawake wanao husika katika mbio za masafa marefu pia huenda waka kosa kushuhudia vipindi vyao vya hedhi mara kwa mara.

2. Uzito Mwingi Wa Mwili

Sawa na uzito mdogo wa mwili, uzito mwingi unasababisha mabadiliko ya homoni mwilini. Ili kusawasisha homoni mwilini mwako, daktari anaweza kushauri kubadilisha lishe yako na kula vyakula vyenye afya na pia kufanya mazoezi.

chumvi kupima mimba

3. Kukwazwa kimawazo/ fikira nyingi

Fikira nyingi huchangia pakubwa katika kubadili homoni mwilini mwako. Shughuli zako za kila siku na pia kuathiri ubongo wako. Kubadilika kwa homoni mwilini mwako kunasababisha kipindi chako cha hedhi kuchelewa. Kukwazwa na fikira kwa muda mrefu husababisha kupunguka kwa uzito. Ni vyema kujaribu mbinu za kupunguza fikira nyingi ili kusawasisha homoni mwilini mwako.

Je, Kwa Nini Kipindi Changu Cha Hedhi Kimechelewa? Mambo Yanayo Sababisha

4. Mbinu za kudhibiti uzalishaji

Huenda ukashuhudia mabadiliko katika kipindi chako cha hedhi ukitumia baadhi ya mbinu za kudhibiti uzalishaji ama unapo koma kuzitumia. Huenda ikachukua hadi miezi sita ili kipindi chako cha hedhi kusawasishwa.

5. Maradhi sugu

Maradhi kama kisukari huenda yaka athiri kipindi chako cha hedhi na kufanya kichelewe. Mabadiliko katika viwango vyako vya sukari mwilini vina husishwa na kuchelewa kwa kipindi chako ama kukifanya kisiwe cha kawaida.

Wakati wa kumwona daktari.

Ukishuhudia ishara hizi, hakikisha kuwa unamtembelea daktari wako bila kukawia:

  • Kutoa damu nyingi
  • Uchungu mwingi
  • Joto jingi mwilini
  • Kichefu chefu na kutapika
  • Kutoa damu zaidi ya siku saba
  • Kutoa damu hata baada ya kufikisha umri

Kwa hivyo unapokosa kipindi chako cha hedhi, usikue na mbio kutumia chumvi kupima mimba ama mbinu yoyote ile. Ila, hakikisha kuwa unafika kwenye kituo cha matibabu kufanyiwa vipimo kudhibitisha chanzo cha kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi.

Soma PiaMatatizo Ambayo Wanafunzi Wa Kike Wanakumbana Nayo Wanaposhuhudia Hedhi

Written by

Risper Nyakio