Kwa kawaida ngozi ya mwanamke huwa tofauti na ya mwanamume. Hutakiwa kuwa laini, nyororo na isiyo na madoa wala ukavu. Hii ni kutokana na kuwepo kwa homoni ya estrogeni inayozalisha vichocheo kwa ajili ya ngozi nzuri. Je, chunusi ni dalili ya ujauzito?
Chunusi Ni Nini?

Chunusi hutokea pale ambapo vinyweleo vinapozibwa na mafuta pamoja na seli za ngozi zilizokufa. Kwa kawaida hutokea usoni, kifuani, mabegani na mgongoni. Chunusi hutokea zaidi kwenye umri wa kubalehe ingawa inaathiri watu wa rika lolote.
Nini Husababisha Chunusi?
Kuna sababu nne kuu zinazosababisha chunusi kutokea:
- Kuzalisha mafuta kwa wingi
- Bakteria
- Vinyweleo kuzibwa na mafuta na ngozi iliyokufa
- Kuzidi kwa homoni kama vile androgen
Chunusi Ni Dalili Ya Ujauzito?
Wakati wa ujauzito homoni huongezeka na kuongeza kiwango cha sebum kwenye ngozi. Hii husababisha ngozi ya mafuta. Mafuta haya pamoja na ngozi iliyokufa huziba vijitundu vya vinyweleo na kusababisha mafuta kujirundika ndani ya ngozi.
Na hapo ndipo bakteria huingia na kutengeneza aina ya usaha unaotoka kwenye chunusi. Hii aina ya chunusi sio tofauti na zile zingine kama wakati vijana wanabalehe. Asilimia 50 ya wanawake wajawazito hupatwa na chunusi ila sio jambo la kuogopa.
Cha kuzingatia ni utaratibu wa usafi zaidi ili kuepuka makovu na alama za baadaye. Kadri miezi ya ujauzito inavyopita mwili huanza kutulia. Viwango vya estrogeni huanza kuongezeka na kupunguza athari za homoni. Kwa hivyo bila shaka chunusi ni dalili ya ujauzito. Na kina mama walio na shida ya chunusi wana uwezekano mkubwa wa chunusi wakati wa ujauzito.
Sababu Zinazochochea Chunusi Kutokea Na Kuongezeka

- Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango husababisha chunusi. Pia kuwepo kwa homoni androgen wakati vijana wanabalehe
- Tafiti zinaonyesha kuwa vyakula vya wanga kama mkate, chips huongeza makali ya chunusi
- Msongo wa Mawazo. Msongo wa Mawazo huchochea tatizo la chunusi
- Mazingira yenye mafuta. Mazingira kama ya jikoni yanaweza kuchochea chunusi
- Vipodozi vyenye mafuta mengi huchochea chunusi
Jinsi Ya Kuondoa Chunusi
- Osha uso wako kwa mara mbili kwa siku kuondoa uchafu na mafuta kutoka kwenye ngozi
- Usisugue uso wako kwani inaweza kusababisha chunusi kuwa mbaya zaidi
- Tunza nywele zako katika hali ya usafi kwani mafuta kutoka kwa nywele yakifika usoni husababisha chunusi
- Jihadhari na kutumbua chunusi hii husababisha uvimbe na makovu
- Pata ushauri wa daktari ili kupambana na chunusi
- Punguza vyakula vinavyohusishwa na chunusi
- Usitumie vipodozi ama bidhaa za mafuta kwa sababu unaweza kuwa na chunusi zaidi
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Mabadiliko Mwilini Mama Anapokuwa Na Mimba Ya Mwezi Mmoja