Corazon Kwamboka ambaye ni mwanasheria na kidosho mashuhuri kwenye mitandao atangaza kuwa hawako pamoja tena na mpenziye Francis Kiarie Mukui, mashuhuri kama Frankie JustGymIt. Corazon na Frankie wametengana baada ya kuwa pamoja kwa kipindi cha miaka mitatu na kubarikiwa na watoto wawili. Wawili hawa walisemekana kuwa katika uhusiano katikati ya mwaka wa 2019. Miezi michache baada ya Frankie kuachana na mpenzi wake wa hapo awali Maureen Waititu.

Uvumi ulianza kusambaa kuwa wawili hawa walikuwa pamoja hata kabla ya Frankie na Maureen kuwachana. Jambo ambalo Frankie alipinga vikali, na kuweka kweli kuwa, alianza kumwona Corazon baada ya kuwachana na mama wa vijana wake wawili. Watu walianza kushuku kuwa kulikuwa na tatizo paradiso mwezi wa Aprili mwaka uliopita. Hata hivyo, Frankie na Corazon walipinga uvumi huu na kuonekana wakienda sherehe mara kwa mara wakiwa pamoja. Corazon Kwamboka na Francis Kiarie walipata kifungua mimba chao mwaka wa 2020 na kitinda mimba chao mwezi wa December 2021.
Mwezi wa Februari kwa kawaida huwa mwezi wa mapenzi. Wawili hawa wamekuwa kimya tofauti na ilivyo kawaida yao. Hata siku ya wapendanao ama valentines, hakukuwa na jumbe za mapenzi kati ya wawili hawa. Siku ya jumapili 20/2022, Corazon aliposti ua la rangi nyeusi kisha kuweka ujumbe: Nipo peke yangu. Najichagua. Maisha yanaendelea. Ua hili huenda likawa ishara fiche kuwa uhusiano wao ulikuwa na changamoto. Ikawa bayana kuwa, Corazon na Frankie wametengana.

Habari za kuhuzunisha kwani watu wengi walipongeza wapendanao hawa na kuwatakia dua nzuri katika uhusiano wao. Ujumbe wa Corazon kwenye kurasa yake ya Instagram ulikaribishwa na hisia tofauti kati ya wafuasi wake. Huku wengine wakimtaki mazuri maishani na kumpa moyo aendelee na maisha yake, wengine walimkumbusha kuwa wakati huu ulitarajiwa kufika. Kuwa njia aliyompata mtu ndiyo njia atakayompoteza.
Sawa na ndoa zingine, ni bayana kuwa uhusiano wao ulikuwa na nyakati za kutosikizana. Hata kama uhusiano wao ulifika tamati, tunawatakia wawili hawa mema maishani.
Soma Pia: Nyumba 5 Za Watu Mashuhuri Kenya Ambazo Lazima Utazame