Madaktari Wasimulia Hadithi Jinsi Mwanao Wa Miaka 4 Alikumbana Na Covid-19

Madaktari Wasimulia Hadithi Jinsi Mwanao Wa Miaka 4 Alikumbana Na Covid-19

Nilipo anza 'Mighty Littles', sikuwai tarajia kuandika kuhusu watoto wangu wakiwa hospitalini. Nilipanga kuandika kuhusu nguvu ambazo wazazi wanazo kuwa nazo wakiwa NICU, jinsi ulezi unavyo badilika kadri muda unavyo songa, na jinsi matukio makubwa yana tubadili tulivyo kama wazazi. Walakini, tukiona jinsi dunia ime ongozwa na janga la COVID-19, na sasa pia familia nyingi, ninazo paswa kuandika juu yake. Lazima niandike kulihusu. Covid-19 kwa watoto imechukua kiwango kikubwa cha akili zangu na hofu kwa wiki iliyo pita, na siyuko peke yangu.

Madaktari Wasimulia Hadithi Jinsi Mwanao Wa Miaka 4 Alikumbana Na Covid-19

COVID-19 kwa watoto: Jinsi ishara za Lincoln zilivyo onekana

Kama mwuguzi, nilifuatilia mlipuko wa janga la Covid-19 Uchina na Italiano kwa karibu. Hata kama hakuna maagizo yaliyo kuwa yamewekwa, tuliwatoa watoto wetu kutoka kwa Jiujitsu na madarasa ya kuogelea mapema. Kwa sababu tuliamini kuwa virusi hivi vilikuwa hatari kabla ya watu wengi waanza kuvichukulia kwa makini. Watoto waliendelea kuenda shule ya watoto na siku yao ya mwisho shuleni ilikuwa Machi 21. Utaifa wa Colorado ulifunga mashule kuanza tarehe 16 mwezi wa tatu. Kutoka tarehe 12, watoto hawakutoka nyumbani. Bwanangu alienda Costco mara moja. Nilienda Target mara moja. Watoto wangu hawakuenda tarehe za michezo. Singewaruhusu wapite barabarani wakienda kwa marafiki wao. Tulikumbatia ushauri wa kubaki nyumbani mapema na tukafuata ushauri huo. Tulifanya kila kitu vizuri.

Ila Lincoln akigonjeka. Katika mwezi wa tatu tarehe 21, Lincoln alichemua mara chache, nikadhani ni mito. Siku iliyo fuata alipata homa kisha kuhoa. Hakuwa na joto jingi na sikuwa na shaka sana. Nili dhania kuwa alipata homa kidogo. Tarehe 27, alipata joto jingi ya mwili hadi 104.5. Alikuwa katika hali ya kuhuzunisha. Nikaanza kutia shaka. Tulimtembelea daktari wa afya ya watoto kitu cha kwanza asubuhi ya Mechi tarehe 28 na akapatikana ana pneumonia baada ya kugonjeka sana (jambo linalo eleweka) na tukachukua antibiotics na oxygen za masaa 48 yajayo. Alikuwa na wakati ambapo alikaa kana kwamba yuko sawa kabisa, dakika zingine alikaa mgonjwa. Ila kwa ujumla, alikuwa sawa. Siku ya jumatano, alikuwa anahitaji egemeo zaidi na zaidi na oxygen na akalazwa hospitalini.

COVID-19 in kids

Nilijua kuingia hospitalini kuwa tungekuwa huko kwa siku kadhaa -  nilidhani tatu, zikizidi sana nne. Nilijua kuwa angewekwa kwa masharti ya "COVID rule out" - ambako wanamtibu kana kwamba ana virusi hivyo hadi vipimo virudi vikiwa hasi. Na kwa sababu najua masharti ya hospitali kuhusu COVID kwa watoto, nilijua kuwa singeweza kutoka kwenye chumba chake hadi vipimo viwe hasi. Kwa hivyo nikiingia hospitalini, nilikuwa na mtoto mmoja wa miaka minne, tanki mbili za oxygen zilizo kuwa karibu kuisha na begi tatu, - moja ya manguo, moja ya vifaa vya kutosheleza na vyakula vichache na begi ya kompyuta. Pia mimi nilikuwa na masaa manne ya wasi wasi kwenye kichwa changu nikijiuliza kilichokuwa kina endelea na mtoto wangu na kwa nini hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi.

Kusajiliwa kwake kulikuwa laini na tuliweza kuingia chumbani mwetu: IV, maabara, swabs, madawa, oxygen yote yalifanywa na wafanya kazi wake. Katika wakati ule wa kusajiliwa, alihitaji lita 2 za oxygen. Usiku huo, aliendelea hadi kuhitaji lita 4. Kwa siku iliyofuata, alihitaji lita 6 na kisha 9. Alikuwa anafanya kazi sana apumue - akitumia misuli yote ya kifua chake, tumbo na shingo kumsaidia kupumua. Kama daktari, nilijua alikuwa ana kazana sana kupumua. Majina ya kimatibabu yanayo tumika kueleza kuteseka kwa mfumo wa kupumua - kupumua kwa seesaw, nasal flaring, grunting, retracting, tachypneic -  alikuwa nayo yote.

Kama mama, yalikuwa mateso kumwona akiteseka kupumua.

COVID-19 in kids

COVID-19 kwa watoto: hospitalini

Siku za kwanza mbili hospitalini, maabara na ujumbe ulianza kurudi. Kipimo chake cha damu kwa kimombo Complete Blood Count (CBC) haikuonyesha ishara hasa za maradhi ya COVID. Vipimo vingine vya maambukizo ni CRP na Procalcitonin ambazo ziliongezeka. Picha ya X-ray ya kifua haikuwa mbaya. Ali badilishwa IV antibiotics mbili- Ampicillin na Azithromycin. Alianza kupata matibabu ya Albuterol. Na vipimo vyake vya virusi vilikuwa bado kufika. Siku za kwanza mbili aliendelea kuwa na hali mbaya zaidi. Maabara yake na X-ray haikukaa kanakwamba ni homa ya corona lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya zaidi.

Wakati karibu 7.00pm usiku wetu wa pili hospitalini, tulipata habari. Daktari wa wakati wa usiku aliingia na kujitambulisha kisha kumwangalia Lincoln. Aliniambia, - Lincoln ana virusi vya COVID-19. Nilianza kulia. Hali yak ilikuwa inazidi kuwa mbaya kwa kasi na nilikuwa na hofu nyingi.

Wakati wake haukuwa sawa. Vipimo vyake vya maabara havikutoshana. Tulichukua tahadhari zote.

Hiki kilitendeka vipi? Kwa nini haya yalitendeka? Sielewi.

Je, atakuwa mgonjwa kiasi gani? Itachukua muda upi? Atakuwa hospitalini kwa muda upi? Na je, wanafamilia wengine wakigonjeka kama vile Lincoln?

Nilifanya kila kitu sawa. Nilipaswa kuwaweka wanafamilia wangu salama na nili feli. Na ndio, najua sikuweza. Ila, fikira hizo zitakosaje kupita akilini mwangu wakati ambapo mtoto wangu mdogo ana virusi hatari zaidi ulimwenguni huu wakati huu?

Hiki kili tendeka vipi? Kivipi? Bado sielewei. Nili lia kwa karibu masaa manne usiku huo. Singeweza kulala. Nilishindwa kuzima akili zangu. Nilikuwa na hofu nyingi sana.

Katika wakati huo huo, nilihisi nimepungukiwa na mawazo. Iwapo kipimo chake cha COVID kingekuwa hasi, ningekuwa nimeshtuka sana kwenda nyumbani na mara kwa mara kushangaa, "itakuwaje akipata COVID sasa?" Angalau sasa nilijua kuwa ana virusi hivyo. Na najua hawezi vipata tena.

Habari njema

Kwa sasa imekuwa zaidi ya siku 5 tangu tulipofika hospitalini, Lincoln ameanza kuhisi vyema zaidi. Ishara za furaha kwa mtoto wangu zina anza kuonekana baada ya kila dakika 30. Analala zaidi ya masaa 16 kwa siku na kwa mara ya kwanza, alikula kitu (ndizi na apple sauce). Siwezi mpatia hongo ili ale chocolate pudding ama maziwa ya chocolate ama krimu ya chocolate - na huyu ni mtoto wangu ambaye huniuliza kila asubuhi "Mama je, unanifichia chocolate nisione?" karibu kila asubuhi.

Tumeanza kuwean egemeo lake na kwa sasa ziko chini hadi 4L. Ila bado ana kikohozi kibaya zaidi. Atakohoa sana na hana hewa anapo kohoa. Saturations zake zitashuka na mpigo wake wa moyo kuongezeka. "Mama huku hakuna maana". "Mama, huku kutakoma lini?" "Mama, si hisi vyema." "Mama, hakuna haja." "Mama, sitaenda nyumbani."

Tazama na usikize jinsi kikohozi cha COVID-19 kinavyo sikika

Kuwa hospitalini kumekuwa jambo la kututenga. Sikubalishwi kutoka chumbani chake. Hakuna anaye ruhusiwa kuja chumbani chake. Wauguzi na madaktari wanakuja kuangalia maendeleo yake huku wamevalia vifaa vya kujikinga maarufu kama PPE, ila wanapunguza nambari wa mara wanazo kuja chumbani mwake ili kuhifadhi nguo zao. Bwanangu ako nyumbani na mabinti wetu. Hatuwezi kumbatiana. Siwezi wakumbatia mabinti wangu. Familia imetawanyika na tuna hisi vibaya sana.

Mbali na kutengwa kuliko hospitalini hii, karibu nami, kumekuwa na msaada mwingi kutoka kwa jamii. Wafanya kazi wetu wamekuwa egemeo kubwa. Jamii yetu ya shule waliweka lishe pamoja ili kufunza jinsi ya kumpelekea Chris na mabinti wetu chakula kila usiku- jambo ambalo ni kama kutumwa na Mungu kwani hawawezi toka nyumbani. Majirani wetu pia wanapeleka berries safi nyumbani mwetu na kunitumia bidhaa za utunzi pamoja na vitambaa vya kujipanguza baada ya kuoga, vya kujisafisha na shampoo ya nywele. Nili taja kuwa sikuwa nimeoga???

Tunaishi kwa dunia ambapo watu wana zidi kutengana kila mara. Wana tawanyishwa zaidi na - hali za kijamii, utajiri, siasa na dini. Iwapo kuna jambo moja chanya kuhusu safari yetu ya COVID kwa watoto, ni kuwa jamii yetu ilikuja pamoja kutuegemeza. Watu ambao hatukuwajua vyema. Watu ambao hatukuwajua. Marafiki wa marafiki wa marafiki. Tuna washukuru sana na tumebarikiwa kwa sababu jamii yetu ilitu egemeza. Na hakuna aliyetulaumu kwa kijana wetu kuwa na kipimo chanya. Natumai kuwa utangamano huu wa jamii utaendelea hata baada ya kurudi kwa maisha yetu ya kila siku baada ya COVID.

COVID-19 kwa watoto

Ombi la Daktari Zimmerman

Tafadhali kuweni salama, kuweni na afya na mvichukulie virusi hivi kwa makini- sio mzaha. Na tafadhali mfanye utafiti kuwafikia marafiki wenu na majirani na marafiki wa marafiki wenu ambao wana teseka wakati huu wa janga hili.

Habari za hivi punde: Siku ya 6 hospitalini. Ameanza kula vyema zaidi na pia IV fluids zimetolewa. Kwa sasa chini ya lita 1 na tuna tarajia kuenda nyumbani hivi karibuni.

 

Katika wakati wa kuchapisha makala haya, Lincoln bado ako hospitalini.

Daktari Anna Zimmerman ni mama na pia Neonatologist, kwa sasa, anaishi Denver, huko Colorado na bwanake na watoto wao watatu.

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye kurasa ya MightyLittles na yame chapishwa tena na idhini ya Africaparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio