Cristiano Ronaldo apoteza mtoto wake wa kiume.
Nyota wa timu ya kadanda ya Manchester United, Cristiano Ronaldo na mke wake Georgina Rodriguez waliokuwa wakitarajia mapacha. Jumatatu walisema kuwa mtoto wao wa kiume alikuwa ameaga dunia.
Picha: Cristiano Ronaldo Instagram
Katika chapisho kwenye kurasa yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Ronaldo alisema, “Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha mtoto wetu wa kiume. Ni uchungu mkubwa zaidi ambao wazazi wanaweza kuhisi,” alisema katika kauli ya pamoja na mke wake Georgina.
Haijadhibitika chanzo cha kifo cha mtoto wao. Hata hivyo, walisema kuwa mtoto wao wa kike alisalimika na yuhai. Kauli yao iliendeleza kusema, “Kuzaliwa kwa mtoto wetu wa kike pekee ndiko kunatupa nguvu kuishi dakika hii na matumaini na furaha,” wawili hawa walisema.
Wanandoa hawa walishukuru madaktari na wauguzi kwa utunzaji wao na msaada na kuongeza kuwa walikuwa na majonzi na wangetaka muda wa kipekee katika muda huu mgumu kwao.
Picha: Georgina Rodriguez Instagram
“Mtoto wetu wa kiume, wewe ni malaika wetu. Daima tutakupenda,” walisema.
Wafuasi wake, wachezaji wenza, familia na marafiki walituma rambirambi zao baada ya habari kutokea kuwa Cristiano Ronaldo apoteza mtoto wa kiume.
Timu yake ilisema kuwa, kufuatia kifo cha mtoto wake, mchezaji huyu hangecheza katika mchezo dhidi ya Liverpool Jumanne kwani familia yake ilikuwa inaomboleza. “Familia ni muhimu kuliko kila kitu na Ronaldo anaegemeza wapendwa wake katika kipindi hiki kigumu kupindukia. Tunakufirikia katika wakati huu mgumu.” Timu ya Manchester United ilisema katika kauli yao.
Soma Pia:Mulamwah Na Carol Sonnie: Keilah Sio Mwanangu, Mulamwah Aliandika Kwenye Facebook Yake