Daktari Ken Ouko Aaga Dunia Kufuatia Maradhi Ya Covid-19

Daktari Ken Ouko Aaga Dunia Kufuatia Maradhi Ya Covid-19

Habari za kuhuzunisha mitandaoni yote kuwa daktari Ken Ouko, mhadhiri mkuu wa Chuo Cha Nairobi ameaga dunia.

Asubuhi ya kuhuzunisha baada ya nchi kuamkia habari kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi daktari Ken Ouko ameaga dunia. Alikata kamba asubuhi ya Jumamosi tarehe moja 1 Agosti na vyanzo vinatujuza kuwa aliaga kufuatia kuugua maradhi ya Covid-19. Bw. Ken alilazwa hospitali ya Aga Khan siku chache zilizo pita kufuatia matatizo ya Covid-19.

Daktari Ken Ouko Aaga Dunia Kufuatia Maradhi Ya Covid-19

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Nairobi Daktari Ken Ouko Aaga Dunia Kufuatia Maradhi Ya Covid-19

Bwana Ken Ouko alikuwa maarufu sana kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi aliko funza masomo ya Kijamii na Saikolojia (Sociology and Psychology). Na alikuwa mhadhiri mkuu katika idara ya Socialogy katika Chuo Kikuu Cha Nairobi.  Alileta ucheshi wake darasani, jambo ambalo wanafunzi walipendelea kwani walifahamu kuwa darasa lake lingekuwa la kusisimua wakati wowote ule. Hadithi zake za kuchekesha, na mifano iliyo wafanya wanafunzi wacheke na waelewe alicho somesha ni jambo lililo wafanya wengi wampende na pia wapasi katika darasa zake na pia darasa zake zikawa maarufu sana.

daktari ken ouko

Ken Ouko amekuwa akifunza katika Chuo cha Nairobi kwa zaidi ya miaka 20. Na alisifika kwani hakuna wakati mmoja alipo enda darasani na kitabu kulingana na wanafunzi wake. Ila hata alipofanya hivi, alifunza na kutaja majina ya waandishi maarufu. Kabla ya kifo chake, sura yake ilikuwa maarufu sana kwa watu wengi kwani mara kwa mara alionekana kwenye televisheni akichangia mijadala kuhusu mada za familia na uhusiano. Wakenya wengi walienda kwa mitandao ya kijamii kusherehekea maisha yake na kumuaga baada ya kupokea habari za kifo chake. Wengi walimsifu daktari Ken Ouko kwa kufanya masomo ya Kijamii yaonekane rahisi sana. Pia walisema kuwa alikuwa mhadhiri bora zaidi wa masomo ya kijamii Kenya nzima. Na kuomboleza kifo chake kwani alikuwa mhadhiri na pia mtu wa kufana katika yote aliyo yafanya maishani mwake.

Viongozi wa nchi pia wametuma rambirambi zao kwa familia ya marehemu daktari Ouko. Mola ailinde na aifariji familia ya marehemu katika nyakati hizi ngumu.

Vyanzo: Standard media

Soma pia: Wasichana Wa Shule Kushiriki Ngono Ili Wapate Pedi Za Hedhi

Written by

Risper Nyakio