Kwa kawaida mtoto wa kike na yule wa kiume huwa na utofauti kabisa. Hizi tofauti sio tu kwa sura mbali pia mwelekeo. Ni bora pia kuelewa kuwa hizi tabia huanza pindi wanapokuwa tumboni mwa mama yao. Hivyo, dalili kuu za mimba ya mtoto wa kiume ni zipi?
Dalili Kuu Za Mimba Ya Mtoto Wa Kiume

Kama nilivyotanguliza, ni kuwa mtoto wa kike huwa na utofauti sana na yule wa kiume. Hizi tabia huonekana kupitia kwa mama na ni kama vile:
Ni wazi kuwa kila mama huweza kupatwa ni kichefu ama morning sickness. Hii huwa ni mojawapo wa ishara kuwa unatarajia mtoto wa kiume.
Ishara moja inayojulikana zaidi huwa kutokwa na chunusi usoni. Hii kwa mara nyingi huwa ni dalili ya mtoto wa kiume.
Wakati wa ujauzito wa kiume utakuwa na hamu sana ya vyakula chachu na vilivyo na chumvi nyingi.
Kwa sababu ya mabadiliko ya homoni, mama wajawazito huwa na mabadiliko ya hisia. Wengi watakuwa wenye hasira.

Mkojo huwa kipimo maalum cha ujauzito mbali kinaweza kutumika kutambua jinsia ya mtoto. Rangi ya mkojo iliyokolea ni ishara ya kutarajiwa mtoto wa kiume.
Kwa kawaida mama anapokuwa mjamzito matiti huongezeka kujitayarisha kwa kunyonyesha. Ila iwapo unatarajia mtoto wa kiume titi la kulia huwa kubwa kuliko la kushoto.
Mkao wa tumbo huwa njia moja ya kutambua jinsia ya mtoto. Iwapo tumbo lako laelekea chini ni ishara ya kuwa na mtoto wa kiume.
Unapotarajia mtoto wa kiume nywele hukua ata maradufu. Pia ngozi huwa na mgao kuliko kawaida.
Ishara nyingine ya kubeba mtoto wa kiume ni kuwa na hisia kama miguu baridi mara kwa mara. Pia kuna wale ambao miguu yao hufura.
Machovu wakati wa ujauzito huwa kawaida sana. Ila unapolala ili kupumzika iwapo unatumia kwa mara nyingi ubavu wa kushoto ni shara ya mtoto wa kiume.
Kila mama mjamzito huweza kuongeza uzani kipindi cha ujauzito. Kuwako na tumbo duara na kuongeza uzani ni dalili ya mtoto wa kiume ikilinganishwa na mtoto wa kike ambaye uzani husambaa mwili wote.
Kila ujauzito huwa tofauti ila ishara za kutarajia jinsia fulani huwa hazibadiliki. Iwapo wakati mwingine zitaoana na zile za mtoto wa kike hizi ndizo dalili kuu za mimba ya mtoto wa kiume.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Asali Kwa Mtoto Mchanga: Jinsi Asali Inavyosababisha Botulism Kwa Watoto