Kutokuwa na maziwa tosha ni shaka kuu la mama wanao nyonyesha. Mama anaye mlisha mtoto wake kupitia kwa chupa anaweza pima kiwango hasa cha maziwa ama formula anacho mlisha mtoto wake. Lakini kama unamnyonyesha mtoto wako, hakuna njia dhabiti ya kupima na kufahamu kiwango cha maziwa ambacho mtoto wako anapata. Kwa hivyo, utajuaje ikiwa unachakata maziwa tosha ya mama ya kumtosheleza mtoto wako na kama anapata maziwa tosha kila anapo nyonya?
Wakati ambapo hauwezi pima na kufahamu, kuna njia zingine za kukusaidia kujua kama mtoto wako anapata maziwa tosha. Hapa kuna ishara za kuwa makini nazo kujua.
Uzito wa mtoto kama ishara bora ya kupata maziwa tosha ya mama

Katika siku za kwanza chache za maisha, ni kawaida kwa mtoto kupoteza uzito hadi asilimia 10 ya uzito alio zaliwa nao. Lakini baada ya wiki mbili, atarejesha uzito alio zaliwa nao. Na hii ndiyo njia dhabiti ya kuhakikisha kuwa mtoto wako anapata virutubisho tosha.
Ishara zingine
- Unambadili diaper zilizo chafuliwa. Baada ya siku ya tano ya maisha yake, mtoto wako ataanza kuwa na angalau diaper 6 ama 8 zilizo chafuliwa kwa siku.
- Mtoto wako ana shikilia chuchu vizuri na kunyonya wakati anaofaa- angalau mara 8 hadi 12 kwa siku, baada ya kila masaa mawili ama matatu.
- Unaweza sikia mtoto wako akinyonya na kumeza anapo nyonyesha, na unaweza ona maziwa ya mama kwenye mdomo wake.
- Baada ya kumlisha mtoto, matiti yako yanakuwa laini na hayaja jaa kama yalivyo kuwa kabla ya kunyonyesha.
- Mtoto wako anakaa ametosheleka na kushiba baada ya kunyonya, na kulala anapo nyonya.
Je, mwendo wa tumbo ni ishara dhabiti?
Kinya cha kwanza ambacho mtoto hupitisha kina fahamika kama meconium. Chenye rangi ya kijani ama cheusi na kilicho shikana. Kwa siku za kwanza mbili, watoto hupitisha kinya cha aina hii. Kisha baada ya hapo, kinya chake kitageuka na kuwa cha manjano. Kila mtoto ni tofauti na baada ya mwenzi mmoja, ni kawaida kwa mtoto huyo kuwa na diaper iliyo jaa kila mara unapo mbadilisha. Pia ni kawaida kwa mtoto kujaza diaper baada ya kila siku moja.

Kula na kulala kwa watoto
Katika miezi ya kwanza miwili ya maisha yake, mtoto anastahili kuwa akilishwa baada ya kila masaa mawili ama matatu na pia usiku. Baada ya miezi hii, baadhi ya watoto wataanza kunyonya baada ya muda zaidi. Na wanaanza kulala vyema usiku, kumbuka kuwa kila mtoto ni tofauti na baadhi ya watoto huenda bado wakasumbua kulala usiku wakiwa katika miezi mitatu ya maisha yao.
Wasiliana na daktari mtoto anapo:
- Asipo kula vyema
- Anapo lala kwa muda mrefu bila kuamka kunyonya
- Pitisha mkojo wa pinki, mwekundu ama wa manjano
- Lia akinyonya ama kuonyesha dalili za njaa hata baada ya kunyonya
Soma Pia: Kuwa Makini Kuona Hatua Hizi Katika Mtoto Wako Wa Miezi Mitatu