Je, Mama Atafahamu Vipi Anapo Karibia Kujifungua? Kubaini Leba Halisi

Je, Mama Atafahamu Vipi Anapo Karibia Kujifungua? Kubaini Leba Halisi

Katika siku za mwisho chache za ujauzito kabla ya mama kujifungua, mlango wa uke huanza kufunguka pole pole.

Leba ni mojawapo ya dalili ya kutaka kujifungua inayo fahamika sana. Je, nitafahamu vipi leba inapo anza? Tazama dalili zinazo kuashiria kuwa leba halisi imeanza.

Jinsi ya kufahamu leba inapo anza

 1. Mama hushuhudia mikazo ya uterasi

Mikazo ya uterasi huwa taratibu na kufuata mtindo maalum. Mikazo huzidi kuongezeka na haiwezi punguzwa kutumia dawa za kutuliza maumivu. Mama anapo tumia dawa za kutuliza maumivu, dalili za uchungu huenda zikapungua kidogo lakini leba halisi bado huendelea.

Mama anapo shuhudia leba halisi, mikazo tosha ya uterasi huibuka. Unaweza fahamu mikazo hii kwa kuangazia mambo matatu:

 • Mara ambazo mikazo ya uterasi inatendeka, mara 3-4 katika kila dakika 10
 • Muda wa mkazo mmoja huwa angalau sekunde 40-60
 • Makali ya mikazo, huja kwa kishindo

dalili ya kutaka kujifungua

2. Damu tetelezi

Katika siku za mwisho chache za ujauzito kabla ya mama kujifungua, mlango wa uke huanza kufunguka pole pole. Mama hushuhudia utelezi ulio na kiwango kidogo cha damu, hii ndiyo damu tetelezi. Damu hii inaweza toka mara moja kwa kishindo, ama kudondoka polepole. Unao shuhudia hali hii, fahamu kuwa mlango wako wa uke umeanza kuwa laini na kufunguka. Na uko karibu kushuhudia leba halisi wakati wowote.

3. Mfuko wa maji kupasuka

Kupasuka kwa mfuko wa maji ama membrani ya fetusi ndiyo ishara ya mwisho kabla ya uchungu wa mama. Kwa wamama wengi, mfuko huu hupasuka katika kipindi cha kwanza cha leba kisha uchungu wa mama uanze, hii ni dalili ya kutaka kujifungua. Leba isipo anza kabla ya masaa sita baada ya kuvunjika kwa fuko la maji, mama ako katika hatari ya kupata maambukizi.

Jinsi ya kutofautisha kati ya leba halisi na leba bandia

dalili ya kutaka kujifungua

Leba halisi

 • Mikazo ya uterasi hutokea ikifuata utaratibu halisi kisha kupungua polepole
 • Muda wa kila mkazo huzidi kuongezeka pole pole
 • Nguvu ya kila mkazo huongezeka
 • Mlango wa uke kufunguka ama kupanuka baada ya muda
 • Uchungu wa mgongo usio pungua hata baada ya kutumia dawa za kutuliza uchungu

Leba bandia

 • Mikazo ya uterasi haifuati utaratibu wowote
 • Muda wa mkazo wa uterasi haubadiliki, ni mrefu ama mfupi
 • Muda wa kila mkazo hauongezeki kwa vyovyote vile
 • Mlango wa uke haupanuki na kubaki chini ya sentimita mbili
 • Uchungu haupo mahali mahususi na hutulizwa kwa kutumia dawa za uchungu

Soma PiaFibroids Zina Athiri Uwezo Wako Wa Kupata Mimba?

Written by

Risper Nyakio