Fibroids ni aina ya vidonda visivyo vya saratani vinavyo kua kwenye mji wa mtoto kwenye mwanamke. Wanawake wengi hupata vidonda hivi ila wengi wao hukosa kujua hata. Kwa visa vikali, huenda vidonda hivi vika athiri uwezo wa uzalishaji wa mwanamke ama kusababisha matatizo katika ujauzito wake. Je, dalili za fibroids katika mimba ni zipi?
Ni kawaida kwa mwanamke kukosa kufahamu anapo kuwa na fibroids. Kwani ni vidonda vidogo ambavyo havi athiri kitu chochote mwilini mwake. Ila, ikiwa vidonda hivi ni vikubwa, huenda vikamletea mwanamke matatizo mwilini. Kama vile ya kutunga mimba, ukuaji wa mtoto kwenye mji wa mtoto, safari ya ujauzito, kujifungua kabla ya mtoto kukua ama matatizo mwanamke anapo jifungua.
Dalili za kuwa na fibroids katika ujauzito

- Maumivu makali ya tumbo, sawa na uchungu wa tumbo wakati wa hedhi
- Kutatizika kuchakata chakula tumboni
- Kuhisi haja ya kwenda haja ndogo kila wakati
- Kuhisi uchungu unapo enda haja ndogo
- Kuumwa na mgongo
Fibroids zina athari gani kwa ujauzito?
Hata kama mara nyingi, vidonda hivi havi athiri ujauzito, vikiwa vikubwa huenda vikawa na athari zifuatazo kwa mimba:
- Kupoteza mimba
- Mtoto kukua tumboni kwa hali isiyo ya kawaida, miguu kuwa juu
- Uchungu wa mama usio komaa
- Obstructed labor
- Necrosis inayo sababisha kifo cha seli
- Kujifungua kabla ya wakati
Matibabu ya fibroids

Katika visa ambavyo mwanamke ana fibroids kubwa katika ujauzito, daktari anaweza fanya utaratibu wa kuzitoa. Hata hivyo, utaratibu huu huenda uka sababisha matatizo zaidi. Huku utaratibu wa fibroids kutolewa mama anapo jifungua kupitia upasuaji wa c-section una shika kasi. Hata hivyo, mama ako katika hatari ya kupata matatizo zaidi.
Wakati ulio salama kutoa fibroids ni mama anapo jifungua, kwani haku hatarishi maisha ya mtoto anaye kua tumboni.
Mwanamke anaweza fanya vitu hivi ili kupunguza hatari ya kupata fibroids:
- Upasuaji ili kutoa fibroids
- Kufanyiwa matibabu ya ultrasound kutumia joto jingi
- Matibabu ya vichocheo
Ni vyema kwa mwanamke kuwasiliana na daktari anapo panga kupata mimba. Kwa njia hii, daktari ataweza kumfanyia vipimo kudhihirisha ikiwa ana fibroids. Pia, kwa mwanamke aliye na fibroids, ni muhimu kuwasiliana na daktari katika safari yake ya ujauzito kuhakikisha kuwa hakuna matatizo yanayo ibuka katika ujauzito wake. Kufahamu dalili za fibroids ndiyo hatua ya kwanza katika kuzi dhibiti.
Soma Pia: Matibabu Asili Ya Fibroids Na Umuhimu Wa Lishe Bora