Kufahamu dalili za hatari kwa mtoto mchanga kunamsaidia mzazi kujua wakati anapopaswa kumpeleka mtoto hospitalini ili apate matibabu ya dharura. Mzazi anapompeleka mtoto hospitalini, daktari atampeleleza ili kufahamu zaidi kuhusu hali ya mtoto. Baadhi ya masuala ambayo daktari atagusia ni kama vile:
- Iwapo mtoto anatapika anapolishwa
- Ikiwa mtoto anashindwa kunyonya ama kula
- Iwapo mtoto ana choka ovyo ama kupoteza fahamu
Dalili zinazohitaji matibabu ya dharura

Dalili hizi zinahitaji huduma za kimatibabu kwa kasi, kwani mtoto huenda akapoteza maisha yake mzazi asipomfikisha kwenye kituo cha afya mapema iwezekanavyo.
- Mtoto kutatizika kupumua
- Rangi ya ulimi kubadilika na kuwa ya buluu
- Mtoto kuzirai
- Mikono ya mtoto kuganda, kuwa baridi, kucha kubadili rangi na kuwa nyeusi, kana kwamba damu kwenye kucha imeisha
- Mdundo wa kasi wa moyo na shinikizo la damu la chini zaidi
- Mtoto kupoteza kiwango kikubwa cha damu na kudhihirisha dalili kama vile, kuhara sana, kuchoka ovyo na ngozi kuvutika ndani
Dalili za kupatiwa kipaumbele kwenye kituo cha afya

- Mtoto mchanga chini ya umri wa miezi miwili anayekuwa na maumivu makali
- Mtoto mchanga aliyejeruhiwa na kuhitaji kufanyiwa upasuaji wa dharura
- Kunywa sumu
- Anayetatizika kupumua
- Anayeshuhudia joto jingi mwilini
- Pungukiwa na damu mwilini, dhahiri kwenye rangi ya kucha, kuwa nyeupe zaidi, macho na ulimi kubadili rangi
- Mtoto anayeumwa kwa sana
- Kulia ovyo bila kisa kwa muda mrefu
- Kufura miguu kufuatia maji
- Kuchomeka vibaya
- Kutatizika kupumua
Mtoto anayetapika kila anapolishwa hataweza kunywa dawa, pia hupoteza maji mengi kila anapotapika na kupunguza viwango vyake vya maji mwilini. Mtoto anayekuwa na dalili hii hawezi wekwa nyumbani kuangalia iwapo hali yake itabadilika. Mtoto aliye katika hali hii anapaswa kupelekwa kwenye kituo cha hospitali apate matibabu ya dharura.
Mzazi anaposhuhudia dalili za hatari kwa mtoto mchanga, asingoje kuona iwapo hali ya mtoto itakuwa bora kwa kumpa maji moto ama matibabu ya kinyumbani. Kwani haelewi hali yake, na kukaa kwa muda huenda kukamfanya mtoto kupoteza maisha yake.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Jinsi Ya Kutengeneza Chakula Chenye Afya Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja