Kuna wanawake wanao shuhudia dalili za kabla ya hedhi, huku wengine wakikosa. Kwa wanao pata dalili hizi, huenda wakazipata muda wa wiki moja kabla ya vipindi vyao vya hedhi kuanza, ama siku tatu kabla. Kulingana na utafiti uliofanyika, wanawake wanao shuhudia dalili kabla ya kupata vipindi vyao ni asilimia 10 peke yake.
Hata na teknolojia ya kisasa, hakuna uwezo wa kupima dalili kabla ya hedhi. Ila, kwa kuusikiza mwili na kuwa makini, mwanamke ataweza kung'amua mabadiliko. Kuna uwezekano wa kupata dalili hizi katika kipindi kimoja na kukosa katika kipindi kingine. Mara nyingi wanao shuhudia dalili hizi ni wanawake walio na umri kutoka miaka 30 na zaidi.
Dalili za kabla ya hedhi

Wanawake wanao shuhudia ishara za kabla ya hedhi huwa na changamoto tofauti. Dalili za kabla ya hedhi ni kama vile:
- Kuongeza uzito wa mwili
- Kukasirika ovyo
- Kubadilika kwa viwango vya homoni mwilini
- Kuhisi kuumwa na matiti
- Kuumwa na kichwa
- Kuumwa na mgongo
Mchakato wa hedhi
Hedhi ama menstruation hufanyika baada ya seli moja ama yai kuachiliwa kutoka kwa ovari ya mwanamke. Yai hilo lina safiri kutoka kwa ovari zinapo tengenezewa hadi kwenye mirija ya ovari ama fallopian tubes. Yai hilo linapo tungishwa ama kurutubishwa na mbegu za kiume, mwanamke ana tunga mimba. Yai lisipo tungishwa, homoni zinazo saidia katika mchakato wa kupata mimba zinapungua mwilini. Na kusababisha kuta za uterasi kuporomoka na kuachiliwa kama damu.
Ishara za hedhi ni kama zipi?

- Kuhisi tumbo imejaa
- Kuhisi uchungu kwenye chuchu
- Kuhisi uchovu
- Uchungu kwenye tumbo
- Kuumwa na mgongo
Mabadiliko yanayo tokea mwilini mwa mwanamke anapokuwa na hedhi ama kabla ni kufuatia mabadiliko ya homoni mwilini. Homoni inayo husika na vipindi vya hedhi ni estrojeni na ndiyo inayo athiri mwanamke na kumfanya kuwa na mhemko wa hisia na kukasirika ovyo.
Dalili za hedhi tulizo angazia ndizo ambazo wanawake wengi wana pata wanapokuwa katika vipindi vyao vya kila mwezi. Kumbuka kuwa, huku wengine wakiumwa na tumbo katika kipindi hicho, kuna baadhi yao ambao hawahisi chochote.
Soma Pia: Kupima Mimba Kutumia Siki {Vipimo Vya Mimba Vya Kinyumbani}