Wanawake wengi wanaopata hedhi hupata dalili za kabla ya kuingia kwenye hedhi ama premenstrual syndrome (PMS). Hufanyika kati ya siku 5 ama 14 kabla ya kipindi cha hedhi kuanza. Ishara hizi huwa za kawaida, lakini kwa wanawake wengine, huenda zikafanya iwe vigumu kufanya kazi za kawaida.
Dalili za kuingia kwenye hedhi
Ishara hizi zinadhibitisha kuwa umeingia kwenye hedhi ama unakaribia kuanzia kipindi chako cha hedhi.
- Chunusi

Chunusi kutokea kwenye uso siku chache kabla ama siku ambapo hedhi inaanza huwa kawaida kwa wanawake wengi.
Chunusi hutokea usoni mwa wanawake wiki moja kabla ya kipindi cha hedhi kuanza. Kufuatia mabadiliko ya homoni mwilini. Uso hurudi kawaida baada ya kipindi cha hedhi kuisha.
2. Maumivu ya tumbo
Maumivu ya tumbo katika na kabla ya kipindi cha hedhi huwa maarufu kwa wanawake. Maumivu haya huenda yakawa mepesi ama makali zaidi. Wanawake walio na fibroids ama endometriosis huhisi uchungu mwingi zaidi.
3. Uchovu

Kipindi cha hedhi kinapokaribia, mwili hujitayarisha kupoteza damu. Mabadiliko ya viwango vya homoni hufanya uchovu kuingia na hisia kubadilika kwa kasi.
4. Maziwa laini
Viwango vya homoni ya progesterone huongezeka katika kipindi cha kupevuka kwa yai ama ovulation. Maziwa ya mama huongezeka kwa saizi na kufura. Mabadiliko haya hufanya chuchu kuwasha na kuonekana kufura kabla ya kipindi cha hedhi kuanza. Baada ya hedhi kuisha, progesterone mwilini hupunguka na maziwa kurejelea saizi ya kawaida.
5. Maumivu ya kichwa

Mabadiliko ya homoni mwilini husababisha maumivu ya kichwa siku mbili ama tatu kabla ya kipindi kuingia.
6. Kufura tumbo
Siku chache kabla ya kipindi cha hedhi kuanza, huenda ukagundua kuwa unatatizika kufunga kaptura yako. Ama kupata kuwa tumbo inaonekana kuliko kawaida yake unapovalia rinda. Hii ni ishara ya kufura tumbo kwa PMS. Huenda hisia hii ikadumu katika wakati wote wa hedhi, kisha kuisha baada ya hedhi kuisha.
7. Mhemko wa hisia
Kabla ya hedhi kuingia, mwanamke huenda akagundua kuwa anapata hisia nyingi tofauti kwa mara moja. Huenda akahisi kulia baada ya vitu vidogo kutokea. Ongezeko la progesterone na estrogen vinachangia katika mhemko wa hisia.
Dalili zingine za kuingia kwenye hedhi ni maumivu ya mgongo, kutatizika kulala kufuatia ongezeko la temprecha mwilini. Ila, usiwe na hofu, mwili hurejelea kawaida baada ya kipindi cha hedhi kuisha na homoni kurejelea viwango vya kawaida.
Chanzo: WebMD
Soma pia: Epuka Kufanya Vitu Hivi 7 Unapokuwa Katika Kipindi cha Hedhi