Dalili 6 Za Mimba Za Kushangaza Zinazo Shangaza Zaidi

Dalili 6 Za Mimba Za Kushangaza Zinazo Shangaza Zaidi

Mfumo wako wa kuchakata chakula hupunguza utendaji kazi wakati wa mimba. Na kupatia virutubisho wakati tosha wa kuingia kwenye mfumo wa damu na kuifikia fetusi.

Punde tu unapo pata mimba na ianze kuonekana, utapokea ushauri tofauti kutoka kwa kila mtu kuhusu mimba. Watakujuza kuhusu ugonjwa wa asubuhi, mhemko wa hisia, hamu ya vyakula, zote ambazo ni dalili za mapema za mimba. Lakini familia na marafiki zako hawakutaja kuhusu dalili za kushangaza za mimba.

Kuna idadi ya ishara za mapema za mimba za mapema zinazo kuashiria kuwa huenda ukawa una tarajia. Kwa hivyo, makala haya dalili za kushangaza za mimba ambazo wanawake wengine wameshuhudia.

Hapa kuna baadhi ya dalili za mapema za mimba za kushangaza ambazo hakuna anaye kuonya kuhusu.

  • Vitu vya kushangaza hutoka

Dalili 6 Za Mimba Za Kushangaza Zinazo Shangaza Zaidi

Wanawake wengi hushuhudia uchafu wa uke. Lakini hau husishwi na mimba. Walakini, wanawake wengi wenye mimba watatoa kitu cheupe kinacho shikana ama kamasi la manjano mapema katika trimesta ya kwanza na katika safari yote ya mimba. Ikiwa una mimba, huyu atakuwa wewe pia.

Katika mimba, homoni huongezeka kulinda kizazi chako na uke kutokana na maambukizi. Mtembelee daktari wako ikiwa uchafu wa uke unaanza:

Huenda ukawa na maambukizi.

  • Joto mwilini kuongezeka

Unapo amka asubuhi baada ya kupevuka kwa yai, joto mwilini huwa imeongezeka kwa kiwango fulani. Hubaki hivyo hadi unapo pata kipindi chako cha hedhi kijacho. Lakini kama joto hii inayo fahamika kama BBM (basal body temperature), hubaki juu kwa zaidi ya wiki mbili, huenda ukawa na mimba.

  • Kuenda choo huwa kazi

dalili za mapema za mimba

Unaweza hisi kuwa tumbo yako imefura kana kwamba unataka kutoa gesi ama kuenda haja kubwa. Hii ni kwa sababu homoni za mimba hubadilika na huenda ukakosa kwenda msalani, kama vitamini kabla ya kujifungua.

Mfumo wako wa kuchakata chakula hupunguza utendaji kazi wakati wa mimba. Na kupatia virutubisho wakati tosha wa kuingia kwenye mfumo wa damu na kuifikia fetusi. Ikiwa huyu ni wewe, ongeza fiber zaidi kwenye lishe yako, viowevu kwa wingi na mazoezi mara kwa mara. Pia unaweza angalia na daktari wako kuhusu kuongeza dawa za kurahisisha kinya chako zilizo salama kwa mimba.

  • Sinuses zilizo ziba

Umegundua kuwa unaamka mapua yako yakiwa yameziba? Ama pengine umegundua kuwa unahitaji kupiga chafya mara nyingi zaidi kuliko ilivyo kawaida? Huku hufanyika kwa sababu ya ongezeko la snot na kamasi wakati wa mimba.

  • Ladha ya chuma mdomoni mwako

Hali hii kwa kimombo inafahamika kama dsygeusia, ni mabadiliko ya uwezo wa hisia mara nyingi huanza kufifia baada ya trimesta ya kwanza. Baadhi ya wakati huenda ikabaki safari yote ya mimba.

  • Fatulence

dalili za mimba

Umegundua watu wakiziba mapua kando yako? Ongezeko la homoni ya progesterone katika mimba linaweza punguza ufanyaji kazi wa mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula, na kukubalisha wakati zaidi wa gesi kuongezeka. Na gesi hizo zina hitaji kutolewa mwilini kwa njia moja ama nyingine.

Vyanzo: WebMd

Healthline

Soma Pia:Lishe Na Siha Ya Mama Mwenye Mimba: Vyakula Muhimu Katika Mimba

Written by

Risper Nyakio